sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Ofcourse, ndiyo maana wameiasi CCM mchana kweupe. Kasema Njelu Kasaka vizuri kabisa, leo hii ukiwa wananchi wanashangilia wapinzani na kuzomea CCM.
Leo hii Watanzania wanafurahia kuona wasiokuwa na sauti, wanasemewa bungeni na nje ya bunge. Watanzania wa leo si wa miaka hiyo kama ulivyosema, ndiyo maana wanaweza kumuuliza Kinana kwenye mkutano wa hadhara, kuhusu tuhuma za yeye na viongozi wenzake waandamizi, wakiwemo waNEC, kushiriki ujangili na kumaliza rasilimali zetu (ref. Ruaha).
Watanzania wa leo wakienda baa, ile bia ya 'Ndovu', wameipatia jina zuri la kiongozi mmoja wa CCM anayetuhumiwa kumaliza tembo kwenye mbuga zetu.
Umesema kweli kabisa. Watanzania wa leo wameijua kweli. Wanatekeleza wosia wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, kuyatafuta mabadiliko nje ya CCM.
Turudi kwenye hoja. Katiba ya CHADEMA ndiyo hiyo ya mwaka 2006. Karibu.
Kila kitu kipo wazi kaka Makene,huwezi mridhisha kila mmoja.Tumepewa akili za kufikiri na za kiutambuzi,ikiwa watu hawatambui upeo wao wa kufikiri utapasua kichwa bure.Jambo jingine yapaswa ujue kuwa unabishana na watu wa aina gani,kama una bishana na Mtani wa CDM hakika utapasua kichwa pia.Cha msingi tusubiri ushahidi utakaoanikwa wazi hiyo kesho then tutahoji kutokana na ushahidi huo.