Kuhama mabondeni

Mwanyasi

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
7,955
7,101
"Ni rahisi sana serikali kuhamia Dom kuliko sisi kuhama mabondeni" wakazi dar
 
Serikali ikihamia Dom utafaidikaje wewe binafsi ? acha tubanane hapahapa hata Hayati alitishhia lakini mwisho wa siku ???
 
Serikali ikihamia Dom utafaidikaje wewe binafsi ? acha tubanane hapahapa hata Hayati alitishhia lakini mwisho wa siku ???

Hapo kwenye red, mimi sihitaji kufaidika binafsi bali kuona kila mtu anatimiza wajibu wake, wao (Serikali) wapo kwenye vyombo vya habari wakisema tumewaambia wananchi waondoke mabondeni lakini hawakusikia yaani wamegoma! Sasa kwanini walaumiwe wananchi pekee kuwa hawtii maagizo wakati hata wao wamegoma?
 
Sweety hata mimi nimefurahi kukuona lakini rudi kwenye mada kwanza.

Hii imetulia sana mzee wa uporoto01 kwenye kabeji na vitunguu; sweetlady, embu toa maoni yako juu ya kulaumiwa wananchi (wakaazi) wakati anaelaumu nae hataki kutekeleza!
 
Hapo kwenye red, mimi sihitaji kufaidika binafsi bali kuona kila mtu anatimiza wajibu wake, wao (Serikali) wapo kwenye vyombo vya habari wakisema tumewaambia wananchi waondoke mabondeni lakini hawakusikia yaani wamegoma! Sasa kwanini walaumiwe wananchi pekee kuwa hawtii maagizo wakati hata wao wamegoma?

sisi tumeigomea serikali kuhama mabondeni,na wao wamemgomea nani kuhamia Dodoma?
 
Kulinganisha Dodoma na bondeni ni sawa na kulinganisha mafuta na maji. Wa bondeni asipohama anaweza poteza uhai wake.WA magogoni hata asipohamia Dodoma maisha yanaendelea
 
@ fe lady
hivi ile msimbazi hadi salenda ni fault au ancient river?
Ina jina lake nimelisahau, nimejitahidi kulikumbuka nimesahau
 
Back
Top Bottom