Kufungiwa Raia Mwema: Je, kosa ni kunukuu kauli za Rais Magufuli tu au kuna makosa mengine?

Akitamka hajui katamka nini lakini akinukuliwa na kurudia kuzisoma anatambua kakosea na kumchukia aliyemnukuu!!!
Yanapita tu ... Sawa na mtu Anayesikiliza Mziki akiwa na furaha..yakimkuta Anakumbuka Lyrics zake
 
Zifutazo ni nukuu za Rais Magufuli zenye utata tangu aingie madarakani ambazo amewahi kuzitoa MUBASHARA kwenye mikutano ya HADHARA. Twende pamoja halafu tuone kama kosa ni nukuu au kuna kitu kingine nyuma yake.
  1. ''Wale mishahara mikubwa wanaoishi kama Malaika nitawashusha chini waishi kama Mashetani..'' Rais JPM kwenye moja ya mikutano yake.
  2. ''Serikali haitatoa chakula kwa Mwananchi yeyote maana Serikali haina shamba...". Rais Magufuli akiongelea athari ya njaa na uhaba wa chakula nchini,
  3. ''Serikali haitatoa mchango wala kuwajengea nyumba raia ambao nyumba zao zimeangushwa na tetemeko. Serikali haileti matetemeko.....'' Hapa Rais alikuwa akiongelea tetemeko la Ardhi Kagera.
  4. ''Fyatueni watoto kwa wingi sana Serikali yangu itawasomesha bure...''Rais akiongea kwenye mkutano wa hadhara huko Mwanza.
  5. ''Serikali haitajenga nyumba kwa Wananchi wa Kahama ambao nyumba zao ziliezuliwa na mwua na upepo mkali maana Msema kweli ni mpeznSerikali haileti majanga ya mvua....'' Magufuli akizungumza na Wananchi wa Kahama ambao Serikali ya Awamu ya 4 ya JMK iliahidi kuwajengea lakini yeye akafuta mpango huo.
  6. ''Dk. Shein kwanini unakubali kuidhinsha pesa ya safari ya mtu ambaye hataki kukupa mkono tena kwenye msiba...? Kataa na wewe kuidhinisha malipo yake ili aone thamani ya mkono wako.
  7. ''Mzee Kikwete wewe una moyo wa huruma sana. Naomba Mungu anisaidie na mimi niwe na moyo huo jao kwa nusu. Kama siku ile kwenye Mkutano Mkuu wale wajumbe waliokuwa wanaimba sijui wana imani na mtu fulani, ingelikuwa mimi nafikiri nusu ya Wajumbe wale ingepotea...''!!! Rais Magufuli alipokuwa akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa kukabidhiwa Mwenyekiti wa CCM(T).
  8. ''Kwenye vita vya kawaida MSALITI huwa hawezi kuruhusiwa ku-SURVIVE. askari mnajua ambacho huwa mnafanya. Lakini kwenye hivi vita vya KIUCHUMI msaliti anaachwa tu ana survive. Kuna mmoja alikuwa napiga kelele kwelikweli lakini tulipofuatilia e-mail zake tukagundua alikuwa anawasiliana na ACASIA akiomba niltee data hii, niletee data hii...tunamwangalia tu....!! Rais akiongea kwenye kupokea ripoti ya Tanzanite na Almasi Dar.
  9. ''Mimi sijaribiwi....kama wanataka kuandamana wale viongozi wa upinzani wawe wa kwanza na watangulie mbele.....! Rais Magufuli akizungumzia maandamano ya UKUTA..!
  10. '' Mimi siyo mwanasiasa ndiyo maana siwapendi wanasiasa...'' Rais akiongea kwenye mkutano wa hadhara
  11. ''Mimi ni Rais ninayejiamini.......hakuna aliyenishawishi kuchukua fomu za kugombea nilikwenda mwenyewe.....!....Mtu ukijaribu kunishauri kitu ndiyo unapoteza kabisa..'' Rais Magufuli akiongea kwenye uwekaji wa jiwe la msingi Ubungo.
  12. ''Urais ni kazi ngumu sana sasa najuta kwanini niliomba kazi hii. Mimi nilijaribu tu nikakutwa nasukumizwa huko...sikuwa nimejiandaa..'' Rais Magufuli akiongea Arusha kwenye sherehe za Kamisheni kwa Maofisa wa Jeshi.
Kauli za Rais Magufuli ambazo zimesabibisha Raia Mwema lipewe likizo ya miezi 3 haziko kwenye orodha hapo juu. Kauli hizo ni:
  1. ''Watanzania wakaobakia Dar baada ya mwezi Julai basi hao ni wanaume kweli kweli''
  2. ''Zile suruale za zamani msizitupe maana mtazihitaji naadaye''
Sasa hebu wewe kama GT jaribu kulinganisha hizi kauli 2 na zile 12 kule juu useme ni zipi kauli nzito zinazoweza kusababisha Gazeti kufungiwa?? Je, hizi kauli za Rais anapozungumza jukwaani na zikanukuliwa na media zinageukaje tena kuwa ni UCHOCHEZI zinapoandikwa na Raia Mwema??Je, uchochezi ni pale chombo cha habari kinaponukuu hotuba ya Rais lakini Rais anapokuwa anazungumza siyo Uchochezi...??
TAFAKURI JADIDI.....

nadhan tatizo ni ukweli wa kauli zenyewe
hoja ni kama alitamka kweli au la...!
gazeti lako waliombwa wapeleke ushahidi. ajabu wao wakakiri kwamba hawana. hapo serikali utawahukumu kwa kosa gani?
ukipenda kuwasaidia, basi, ni vema wewe uweke clips zinazoonyesha baba jesca akitamka maneno hayo. hapo utakuwa umewaokoa. vinginevo funga mdomo. maana Gazeti lilikubaki kushindwa na zaidi waliomba kuhurumiwa au kusamehewa basi......, mpaka hapo tuihukumu serikali kwa kukataa kuwasemehe lakini hawajawaonea
kilichopo sasa ni magazeti yetu kugeuza social media kuwa chanzo cha habari. hii ni hatari kubwa sana
hii sio hadhi ya gazeti kama raia mwema, tungeelewa sana kama makala ya namna hiyo ingeandikwa na sani au ijumaa wikienda kiu na kadhalika.
mimi kama GT nataka facts sio kulinganisha
eti kwa vile mkeo aliwahi kutembea na kichaa sasa kila akipita mwenye timamu basi lazima katemnea nae...!!!????
FACTS sio KULINGANISHA
Lete ushahidi wa video, lini, wapi alikuwa kwenye shughulu gani wakati anatamka hayo......???? sio eti GTB linganisha...
Humu humu tunamoita home of GTs ndio kumejaa uongo na uzushi, nikukumbushe mifano michache
1. Nape kafukuzwa eti tetesi
2. nyalandu kaitwa kuonywa baada ya kwenda msalimia Lissu
3. nyalandu alimezeshwa maneno juzi akakanusha
4. JK alimezeshwa maneno juzi akakanusha

sasa pamoja na hali hii gazeti linamua kuandika kwa ushahidi kutoka JF ...
 
kumnukuu rais ni kosa ?
mkuu nakuongezea nyengine..
"asiefanya kazi na asile na usipokula si ufe "
"nafuu njaa ikuue kuliko mimi nikuletee chakula"
"huyo mngemtumbukiza kisimani "
"mimi ninavyojua marehemu alikua na wanawake zaidi ya watano, nyinyi mnamjua huyu mmoja tu"
"wakija badilisheni debe moja la mahindi kwa ng'ombe watatu"
"mwaka 2015 sukari kilo ilikua elf tano..." hapa ni dhahiri huyu ni miongoni mwa malaika wachache wanaofaidi keki ya taifa...hata bei ya sukari haijui? twaijua sisi mashetani tu.
CCM ni shetani
 
Back
Top Bottom