Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,697
- 9,048
Zifutazo ni nukuu za Rais Magufuli zenye utata tangu aingie madarakani ambazo amewahi kuzitoa MUBASHARA kwenye mikutano ya HADHARA. Twende pamoja halafu tuone kama kosa ni nukuu au kuna kitu kingine nyuma yake.
TAFAKURI JADIDI.....
- ''Wale mishahara mikubwa wanaoishi kama Malaika nitawashusha chini waishi kama Mashetani..'' Rais JPM kwenye moja ya mikutano yake.
- ''Serikali haitatoa chakula kwa Mwananchi yeyote maana Serikali haina shamba...". Rais Magufuli akiongelea athari ya njaa na uhaba wa chakula nchini,
- ''Serikali haitatoa mchango wala kuwajengea nyumba raia ambao nyumba zao zimeangushwa na tetemeko. Serikali haileti matetemeko.....'' Hapa Rais alikuwa akiongelea tetemeko la Ardhi Kagera.
- ''Fyatueni watoto kwa wingi sana Serikali yangu itawasomesha bure...''Rais akiongea kwenye mkutano wa hadhara huko Mwanza.
- ''Serikali haitajenga nyumba kwa Wananchi wa Kahama ambao nyumba zao ziliezuliwa na mwua na upepo mkali maana Msema kweli ni mpeznSerikali haileti majanga ya mvua....'' Magufuli akizungumza na Wananchi wa Kahama ambao Serikali ya Awamu ya 4 ya JMK iliahidi kuwajengea lakini yeye akafuta mpango huo.
- ''Dk. Shein kwanini unakubali kuidhinsha pesa ya safari ya mtu ambaye hataki kukupa mkono tena kwenye msiba...? Kataa na wewe kuidhinisha malipo yake ili aone thamani ya mkono wako.
- ''Mzee Kikwete wewe una moyo wa huruma sana. Naomba Mungu anisaidie na mimi niwe na moyo huo jao kwa nusu. Kama siku ile kwenye Mkutano Mkuu wale wajumbe waliokuwa wanaimba sijui wana imani na mtu fulani, ingelikuwa mimi nafikiri nusu ya Wajumbe wale ingepotea...''!!! Rais Magufuli alipokuwa akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa kukabidhiwa Mwenyekiti wa CCM(T).
- ''Kwenye vita vya kawaida MSALITI huwa hawezi kuruhusiwa ku-SURVIVE. askari mnajua ambacho huwa mnafanya. Lakini kwenye hivi vita vya KIUCHUMI msaliti anaachwa tu ana survive. Kuna mmoja alikuwa napiga kelele kwelikweli lakini tulipofuatilia e-mail zake tukagundua alikuwa anawasiliana na ACASIA akiomba niltee data hii, niletee data hii...tunamwangalia tu....!! Rais akiongea kwenye kupokea ripoti ya Tanzanite na Almasi Dar.
- ''Mimi sijaribiwi....kama wanataka kuandamana wale viongozi wa upinzani wawe wa kwanza na watangulie mbele.....! Rais Magufuli akizungumzia maandamano ya UKUTA..!
- '' Mimi siyo mwanasiasa ndiyo maana siwapendi wanasiasa...'' Rais akiongea kwenye mkutano wa hadhara
- ''Mimi ni Rais ninayejiamini.......hakuna aliyenishawishi kuchukua fomu za kugombea nilikwenda mwenyewe.....!....Mtu ukijaribu kunishauri kitu ndiyo unapoteza kabisa..'' Rais Magufuli akiongea kwenye uwekaji wa jiwe la msingi Ubungo.
- ''Urais ni kazi ngumu sana sasa najuta kwanini niliomba kazi hii. Mimi nilijaribu tu nikakutwa nasukumizwa huko...sikuwa nimejiandaa..'' Rais Magufuli akiongea Arusha kwenye sherehe za Kamisheni kwa Maofisa wa Jeshi.
- ''Watanzania wakaobakia Dar baada ya mwezi Julai basi hao ni wanaume kweli kweli''
- ''Zile suruale za zamani msizitupe maana mtazihitaji naadaye''
TAFAKURI JADIDI.....