Kufuatia ajali ya Lift Millenioum Tower nimekumbuka yaliyotokea Hall 5 UDSM

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
10,053
24,446
Yes! Kufuatia ajali ya Lift iliyotokea Millenium tower imenifanya nikumbuke miaka kadhaa iliyopita yaliyokuwa yanatokea kwenye Lift ya yale mabweni ya udsm hasa Hall 5! Kwa waliopita hapo watakubaliana kuwa lift ilikuwa ni tatizo sugu!

Nakumbuka siku moja tumeipanda mara ikakwama katikati ya njia! Tulikaa kule ndani tunalowa jasho karibu lisaa, tukampigia mhusika akasema yupo posta tumsubiri, tulimiss lecture ile siku! Imagine ingekuwa UE.

Hakika watu waliriipoti lile tatizo lakini wala halikuwahi kushughulikiwa hadi namaliza, japokuwa nilihamia hostel za mabibo ila waliokiwa wanaishi pale walikuwa wakilalamika kila wakati!

Tunashukuru halijasikika tukio baya lakini kama tatizo lile bado lipo uongozi uchukue hatua stahiki mapema kurekebisha kabla hayajatokea mambo mabaya!

Na hili si kwa udsm bali kwa majengo yote marefu yanayotumia lift, kama zipo zenye shida sifanyiwe marekebisho ya uhakika la sivyo tutamsingizia mtu mchawi bure.
 
Udsm wazee wa main campus wanajua balaa ya zile hostel gorofa ndefu kama twiga. Kipindi cha UE walikua wanakataza kutumia zile lift mana wengne wasiokua waaminifu walikua wanatumia huo mwanya kukwepa kufanya mitihani kwa kisingizio wamekwama kwenye lift
 
Acha kabisa!!!
Hivi hadi hivi sasa lile tatizo lipo ama lishatatuliwa…? Maana yasije yakatokea makubwa zaidi ya yaliyotokea Millenium tower!
 
Sijawahi kupanda lift Dar
Bora nipande ngazi maana kwanza kuna wakati zinasimama ghafla na ile simu ya ndani mtapiga mpaka basi

Sasa yote hayo ya nini? Na kama mpo wengi mnaweza kuzimia kwa kukosa hewa
 
Acha kabisa!!!
Hivi hadi hivi sasa lile tatizo lipo ama lishatatuliwa…? Maana yasije yakatokea makubwa zaidi ya yaliyotokea Millenium tower!
Zile ghorofa zilikuwa zinakarabatiwa mwaka jana sijui kama zimeisha
 
Acha kabisa!!!
Hivi hadi hivi sasa lile tatizo lipo ama lishatatuliwa…? Maana yasije yakatokea makubwa zaidi ya yaliyotokea Millenium tower!
Nadhani bdo, ile yale majengo imagine toka miaka ya 60 huko mbka leo hta nyufa hayana na yapo vzuri. Alafu yanabeba uzito zaidi mana watu chumba cha watu nane wanalala zaidi ya ishirini kubebanaa
 
Hizi lifti za dar ziliwahi kuondoka na ndugu yangu mmoja. Kwani wataalamu wa hizi makitu wanasemaje? Zinatakiwa kufanyiwa matengenezo/service kila baada ya muda gani? Na je zina wakaguzi wake? Na je wanakagua? Mbongo bila kumfuatilia hawezi kuwajibika.
 
Kuna siku ilileta taflani, wadau walidai eti lile jengo linacheza (hall 2). Sijui kama ilikua kweli au uongo au ni minor earthquake ilipita,
All in all hall 2 na hall 5 sijawahi kua na imani nayo
 
Yes! Kufuatia ajali ya Lift iliyotokea Millenium tower imenifanya nikumbuke miaka kadhaa iliyopita yaliyokuwa yanatokea kwenye Lift ya yale mabweni ya udsm hasa Hall 5! Kwa waliopita hapo watakubaliana kuwa lift ilikuwa ni tatizo sugu!

Nakumbuka siku moja tumeipanda mara ikakwama katikati ya njia! Tulikaa kule ndani tunalowa jasho karibu lisaa, tukampigia mhusika akasema yupo posta tumsubiri, tulimiss lecture ile siku! Imagine ingekuwa UE.

Hakika watu waliriipoti lile tatizo lakini wala halikuwahi kushughulikiwa hadi namaliza, japokuwa nilihamia hostel za mabibo ila waliokiwa wanaishi pale walikuwa wakilalamika kila wakati!

Tunashukuru halijasikika tukio baya lakini kama tatizo lile bado lipo uongozi uchukue hatua stahiki mapema kurekebisha kabla hayajatokea mambo mabaya!

Na hili si kwa udsm bali kwa majengo yote marefu yanayotumia lift, kama zipo zenye shida sifanyiwe marekebisho ya uhakika la sivyo tutamsingizia mtu mchawi bure.
Sisi tulio graduate UDSM mwaka 1972 na kina Museveni wakati wa UE tulikuwa hatupandi lift kabisa
''Akili za kuambiwa changanya na zako''-----------------Mhe flani mstaafu
mwisho wa kunukuu
 
Back
Top Bottom