Kufan ya usafi wa mwili vizuri/wanawake

Jpinduzi

Senior Member
Feb 26, 2011
136
68
Uke na SEHEM YA KUNYEA vinapaswa kuoshwa mara kwa mara na kubakia vikavu. Ni jambo zuri kuepuka
kuchangia mataulo na ndugu wengine katika familia au marafiki kwani yanaweza kusababisha
kuenea kwa maambukizi ya magonjwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Baada ya kuoga vaa
chupi za pamba zilizo safi. Katika kipindi cha joto, epuka kuvaa chupi za nailoni kwa sababu huwa
zinahifadhi unyevunyevu na joto, hali ambayo husababisha kuota bakteria. Kama huwezi kupata
chupi za pamba, vaa zilizozungushiwa kitambaa cha pamba.

Baada ya kukojoa au kwenda haja kubwa, unapaswa kujisafisha mwenyewe kwa kusafisha
kuanzia mbele ya sehemu zako za siri mpaka kwenye SEHEM YA KUNYEA. Kama ukitumia karatasi la chooni,
karatasi, maji, majani au matawi ya miti kujisafisha, epuka kujisafisha kutoka nyuma kwenda
mbele. Ukijisafisha kutoka nyuma kwenda mbele, kuna hatari ya kuvuta vijidudu vya maradhi
kutoka kwenye SEHEM YA KUNYEA kwenda kwenye uke na kwenye njia ya mkojo. Hii inaweza kukupa
maambukizi ya magonjwa.

Kamwe usijaribu kuosha ndani ya uke labda tu kama umeshauriwa na daktari.
Kwa bahati mbaya wasichana na wanawake wengine wanaosha ndani ya uke kwa kutumia sabuni
kali. Wanawake wengine wanapenda kupaka odorono au kupuliza manukato. Haya yote hayana
umuhimu, na yanaweza kukuletea madhara kwa sababu sabuni, na manukato vikitumiwa ukeni
vinaweza kubadilisha mfumo wa kawaida wa majimaji ndani ya uke na kusababisha ngozi ndani
ya uke kuwasha.
Katika nchi nyingine, kama vile, Zimbambwe na Zambia, wanawake huweka mitishamba, vipande
vya nguo, na vitu vingine ndani ya uke ili kusafisha au kuufanya ubane. Kiafya, hii sio njia nzuri
kwa sababu ngozi ndani ya uke ni laini mno. Unapoingiza vitu vigeni, vinaweza kusababisha
majeraha madogo madogo au michumbuko na uvimbe mambo ambayo yanaweza kukufanya kuwa
na maambukizi na uwezekano wa kukuweka kwenye hatari ya kupata VVU.

Kwa ujumla, ni vizuri kutokuweka kitu chochote ndani ya uke wako, isipokuwa pamba za damu na
dawa kama umeandikiwa na dakitari. Hakikisha tu unafuata maelekezo kwa makini.
Ni vizuri kuchunguza kwa makini majimaji yanayotoka ukeni wakati wa mzunguko wa kila mwezi
ili kuweza kuona dalili na mabadiliko yasiyo ya kawaida. Ukiwa makini , utagundua kwamba
majimaji yanayotoka ukeni sio sawa wakati wote. Wakati mwingine yanaweza kuwa meupe
wakati mwingine yanaweza kuwa meupe kidogo kama ute mweupe wa yai. Wakati wa uovishaji,
majimaji ya ukeni yanaweza kuwa na utelezi zaidi na angavu. Vilevile majimaji ya ukeni yanaweza
kubadilika iwapo mwanamke atashikwa ashiki.

Iwapo majimaji ya ukeni yatakuwa mazito na kubadilika rangi kuwa njano, kijani au kahawia au
yanasababisha muwasho sehemu za siri, unaweza kuwa umeambukizwa maradhi. Harufu mbaya
ya majimaji toka ukeni, maumivu ndani ya uke na damu kutoka wakati hauko katika siku zako
za hedhi ni dalili pia za maambukizi ya ugonjwa. Iwapo utapata mabadiliko yoyote kati ya haya,
itabidi umwone daktari.

Iwapo hushiriki ngono isiyo salama, na kama unazingatia usafi, huwezi kupata matatizo haya.
Ukiutunza vizuri uke wako utajikamilisha kulingana na mazingira. Unachotakiwa kufanya ni
kuosha kwa uangalifu eneo la via vya uzazi kila siku na maji safi au osha kwa sabuni ya kuogea.
Tenganisha mashavu ya nje ili kusafisha uchafu unaojikusanya sehemu hizo.(SOURCE-doctor)
 
TRUE THAT.Natamani wanawake wengi waisome na kuielewa hii mada kwa manufaa yao.Wengi wanafanya usafi kwa kufuata ushauri wa marafiki na jamaa , na ushauri huo hauzingatii kanuni ulizoelezea. Hasa usafi wa kuingiza vitu au vidole kunako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom