Kuepuka Utekaji Polisi wasikamate watuhumiwa bila Shaidi kuwepo!

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,584
2,898
Kila ukisikiliza taarifa za watu waliopotelewa na ndugu, utashangaa sana, Polisi, wanawaelekeza wamempeleka mtuhumiwa kituoni, Wakienda kituoni Baadae hayupo!

Wizara iweke Kanuni ya kutoruhusu Mtuhumiwa kukamatwa bila Mtuhumiwa kuwa na Shahidi atakayejiridhisha wapi mtuhumiwa amepelekwa.Hususani wale wanaowafuata kwenye majumba yao/ Biashara zao. Vibaka wa mtaani, washughulike nao kadri ya Mazingira yalivyo.

Pia Bunge liangalie Swala hili Kwa uzito kwakuwa Vyombo vya Dola/ Usalama vime abuse utaratibu wa kukamata watuhumiwa, vinakamata na kuwahukumu, waliopotezwa! Mwenzio akinyolewa tia maji, usipoziba ufa utajenga ukuta.

Mungu ibariki Tanzania,amsha akili/Fahamu za watanzania wafikiri kama Wana, sio watumwa.
 
Yale magari yao yenye plate namba za Mars ni ushahidi tosha kuwa polisi ni kitengo cha uhalifu
 
Back
Top Bottom