Uchaguzi 2020 Kuelekelea Uchaguzi mkuu 2020: Tupe tetesi na maoni yako, unapendekeza nani agombee wapi na nafasi gani?

Kusema tu ule ukweli, jimbo letu la Kyela limekuwa kama halina Mbunge tangu aondoke Livingstone Mwakipesile mwaka 1995. Wilaya ya Kyela pamoja na kuwa ni miongoni mwa wilaya kongwe kabisa hapa Tanzania lakini ipo nyuma sana kimaendeleo, yani huwezi linganisha kabisa na wilaya kama Rungwe Mashariki au hata wilaya ya Busokelo iliyoanza juzi juzi tu.

Wilaya ya Kyela imeshindwa hata kukarabati barabara zinazozunguka katikati ya mji, huduma mbovu za maji, miuondo mbinu mibovu ya barabara utadhani wilaya haina mapato. Nakumbuka kipindi Mh Rais anafanya ziara Wilayani Kyela, uongozi wa hapo wilayani walijaribu kuziba ziba mashimo ya barabara kuu itokayo Kasumulu kwenda Kyela ili tu ionekane ni nzima wakati ukweli ni kwamba barabara hiyo ni kimeo sana.

Mbunge hana muda na jimbo lake, angalau Dr. Tulia ameonyesha moyo wa upendo kupitia Tulia Foundation wananchi wanafaidika na mikopo midogo midogo.

Hivyo basi Tunakuomba Dr Tulia uje ugombee ubunge katika wilaya yetu, tuna imani sana na wewe kwamba angalau unaweza kuleta maendeleo chanya katika wilaya ya Kyela
 
Mnambua,

Mwigulu alivyoweka siasa mbele kwenye swala la Lissu hata CCM wenyewe wanamwogopa kwa uchungu wa madaraka. Yaani Magu alisema hata ingekuwa yeye asingefanya hile. Kumtosa mbunge ndugu yako kwa siasa ndiyo matokeo yake haya siasa ni mpito. Yaani Magu anamweshimu zaidi Nyalandu kuliko Mwigulu
 
Ndugu wana jf natabiri orodha ya wagombea wa jimbo la Igalula Mkoani Tabora kutokana na tetesi nilizonazo
1. Mussa Rashid Ntimizi, Mbunge wa sasa
2. Athumani Rashid Mfutakamba
3. Habiba Tambulu
4. Hanifa Tambulu
5. Jackson Msome
6. Venant Daudi
7. Masoud Karatasi
kama una tetesi za jina lingine ongeza hapo chini
 
Mbeya mjini_Tulia Ackson (CCM),Joseph Mbilinyi (CHADEMA).
 
Back
Top Bottom