Miaka ya nyuma, uchumi wa nchi ulitawaliwa na serikali kupitia udhibiti wa njia za uchumi chini ya umma. Hata hivyo, kwa sasa, serikali imebakia kuwa mtunga sera na msimamizi wa utekelezaji wa sera hizo na kuwa refa wa mechi ya uchumi.
Tatizo kubwa la Tanzania ni kwamba nchi imegeuka kuwa soko kwa mataifa mengine kutokana na wananchi kutokuwekeza katika viwanda na badala yake kukimbilia matumizi mengine. Hata wakati ambapo wananchi wanataka kuwekeza katika biashara, wanapendelea biashara za uchuuzi na majengo badala ya viwanda ambavyo vingesaidia kukuza uchumi vizuri na kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje ambao unadidimiza thamani ya fedha yetu na uchumi wetu.