Kubenea ahoji: Je, Kafulila huyu wa UDART leo ndio yule yule wa IPTL na Escrow? Yeye (Kafulila) amchana kwa hoja nzito Saba

View attachment 2967024

Na. David Kafulila

NIMELAZIMIKA kushika kalamu ikiwa ni baada ya kusukumwa na andiko la ndugu na jamaa yangu wa miongo mingi na aliyepata kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mhe Saed Swedi Kubenea.

Mhe Kubenea amejadili kuhusu mradi wetu wa BRT unaotarajiwa kuendeshwa na kampuni ya ENG ya Dubai.

Mhe Saed Kubebea ameandika Makala iliyobeba kichwa cha maneno: “ Kafulila wa Escrow ndiye huyu wa UDART? ”

Mimi David Kafulila baada ya kuisoma makala hiyo, nimejiridhisha kuwa kuna maeneo mwandishi hajanielewa au haelewi vizuri.

Mwandishi huyu amejaribu kujenga mashaka ya alichokiita " Hatari ya kampuni ya Dubai kupewa kazi ya kuendesha UDART " Shirika linalomilikiwa na Serikali na kampuni binafsi ya Simon Group Limited.

Binafsi nikiri kuwa nimependa namna mwandishi Saed Swedi Kubenea alivyowasilisha maoni yake kwani yameamsha mjadala wa Ubinafsishaji, Ubia na nafasi ya wazawa katika Umiliki na Uendeshaji wa Uchumi wa Taifa lao.

Kwakuwa mjadala huu ni mpana, naomba leo nieleze mambo Saba ( 7 ) kwa ajili ya kutoa ufafanuzi ili kuwatoa hofu Watanzania akiwemo Ndugu yangu Saed Kubenea.

Na ieleweke kwenu pia nitakayoyaeleza hapa, baadhi ni maoni yangu binafsi, hasa kuhusu dhana nzima ya Ushiriki wa Sekta binafsi ya Ndani na Nje katika kujenga Uchumi Shirikishi na Jumuishi.

Kwanza, nataka sote tuelewe kuna tofauti kubwa kati ya Ubinafsishaji na Ubia.

Mikataba yote ya Ubia duniani – Mali au Aseti zote zinamilikiwa na Serikali husika Kabla, wakati na hata baada ya mkataba vile vile Mikataba ya Ubia haihamishi umiliki wa mali au aseti.

Sikilizeni, Kwa mfano, Ubia kati ya DART na kampuni ya ENG, haimaanishi DART itakuwa imeuzwa au kuhamisha umiliki wa barabara au magari yake.

Kinachofanyika hapa muwekezaji ataleta mabasi yake na kuyaendesha kwa gharama zake huku Serikali ikipatiwa huduma kwa watu wake na masilahi mengine kulingana na mkataba husika.

Nimuulize swali Mhe Kubenea,
Kama Mbia ataleta magari yake na kuyaendesha hapo Serikali itakuwa imeuza rasilimali gani ya Taifa Kwa ENG?

Hata hivyo ni muhimu kufahamu kuwa Usafirishaji kwa njia ya barabara nchini unaendeshwa na sekta binafsi kwa miongo yote sasa, ukiondoa sehemu chache kama ilivyokuwa miradi ya UDA.

Pili, kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa DART ya wiki jana, Taratibu za Serikali kutafuta Mbia kuleta mabasi na kuyaendesha zimeanza tangu mwaka 2017.

Katika mchakato huo, zaidi ya makampuni 30 yalijitokeza lakini hakupatikana muwekezaji mwenye sifa na tija kwa Taifa.

Mchakato huo ukarudiwa tena mwaka 2020, Safari hii Makampuni takribani 40 yalishiriki na hapa ndipo ENG ikaibuka mshindi na kuanza majadiliano na Serikali ya kuendesha mradi huo na majadiliano hayo yalianza mwaka 2022 hata mimi nilipoipewa nafasi hii mwaka 2023 mradi huu upo.

Tatu, Ni bahati mbaya kwamba majadiliano haya yamechukua muda mrefu kutokana na changamoto za kisheria kwani DART & ENG walikuwa wakivutana kuhusu namna bora ya kuhitimisha makubaliano yao kwa masilahi mapana ya Taifa la Tanzania na Watanzania.

Mara zote, tumeendelea kupata ushauri kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kwa lengo la kuhakikisha tunafikia Mkataba wenye masilahi mapana kwa taifa letu na unaolindwa na sheria zetu.

Nne, mradi wa BRT una njia sita, Njia ambayo inajadiliwa na kampuni ya ENG ya Dubai, ni ya kwanza ( Phase I ) ambayo inahusisha kuwapo mabasi 177 yatakayonunuliwa na kampuni hiyo ya ENG.

LAZIMA pia tufahamu, Mabasi yote haya yatakayonunuliwa baada ya mkataba kumalizika, yatakabidhiwa kwa Serikali kabla hayajachoka na kisha wao kuingiza mengine mapya.

Lengo la Serikali na Rais Samia ni kuhakikisha kunakuwa na ubora wa huduma kwa Wanadalesalaam hasa Wapenzi wa Mwendokasi.

Hata hivyo, ujio wa ENG hauindoi UDART bali utaipa kampuni hii ya Serikali na wazawa changamoto katika ubora wa huduma ( a competitive business )

Tano, njia zingine tano bado DART wataendelea na mchakato wao wa kupata wawekezaji kwa utaratibu. wa aina hiyo hiyo.

Njia ya pili ( Phase II ) itahitaji uwekezaji mkubwa zaidi kwani kunatakiwa mabasi 770.

Hii ni fursa kwa wawekezaji wote na hususan wa ndani.

Nakubaliana na hoja ya umuhimu wa kampuni za ndani kupewa fursa hii.

Nakubaliana na hoja ya kuzisaidia kampuni za ndani kupata fursa hii na hata hivyo, ni muhimu tukubaliane kusiwe kwa gharama kubwa. kwa wananchi wanaotumia usafiri huu.

Asilimia 43 ya wakazi wa Dar es Salaam wanafanya kazi maeneo ambayo wanatembea kwa mguu kwa sababu ya changamoto ya nauli.

Hii inawanyima fursa wao binafsi, lakini pia uchumi kwani nguvu kazi hiyo inaweza kuzalisha zaidi ikimudu kufanya kazi zaidi ya umbali huo.

Unafuu wa nauli na ubora wa huduma ni muhimu sana ili kuhakikisha nguvu kazi ya Dar es Salaam inazalisha na jiji linaunganishwa kwa Usafiri wa Uhakika.

Sita, Napenda kutoa wito kwa kampuni za wazawa zenye nia ya kuwekeza eneo hili, waoneshe nia na tuwasaidie kuwekeza kwenye fursa hizi za BRT hata kabla ya DART kutangaza.

Sheria inaruhusu wawekezaji kuleta mapendekezo kabla ya zabuni kutangazwa.

Anachopaswa kukizingatia, ni kwamba anapaswa kuleta mapendekezo yake kama UNSOLICITED.

Njia hii inatumika kwa miradi yote mwekezaji anapoona Serikali haiwezi kuendesha kwa ufanisi, anaruhusiwa kuomba kazi hiyo na atasaidiwa kwa mujibu wa sheria.

Lengo ni kuhakikisha serikali inavutia mitaji, teknolojia na weledi.

Kwamba, Sekta binafsi inatumika kutekeleza baadhi ya majukumu ya serikali kwa ufanisi ili yenyewe ibaki na majukumu muhimu ya kuhudumia wananchi.

Lazima watu waelewe, Sheria ya PPP na hata ile ya manunuzi, zinatoa upendeleo kwa wazawa zaidi.

Serikali inatoa upendeleo wa kisheria na inazijengea uwezo kampuni hizo, ili ziweze kusimama zenyewe, kutokana na kutambua mchango wake kwa uchumi wa taifa Kwa muktadha huo,

Saba, Baada ya ufafanuzi huu wa kina naomba nisisitize kwamba David Kafulila huyu ni yule yule wa Jana, Juzi na Leo,

Kafulila huyu wa UDART ni yeye yule aliyekuwa Mbunge machachari toka Jimbo la Kigoma Kusini ( 2010 - 2015 ).

Kafulila huyu baadae akateuliwa kuwa Katibu Tawala wa mkoa Songwe, aliyesimamia kisawa sawa nidhamu ya Fedha za Umma, Kuichukia rushwa na uwajibikaji kwa halmashauri zake zote.

Ni huyu Kafulila aliyekuwa Katibu Tawala wa kwanza kuvunja mkataba wa Mshitiri wa usambazaji dawa kwenye Mkoa wa Songwe kufuatia kuibuka kwa madai ya udanganyifu.

Mtakumbuka piq, Baada ya kuvunjiwa mkataba ule, muhusika alikwenda hadi Mahakama kuu ambako nako alishindwa kesi zote.

Ni Kafulila yule yule ambaye akiwa mkuu wa mkoa wa Simiyu, mkoa ambao asilimia 70 ya Pamba ya Tanzania inatoka huko.

Niyeye Kafulila aliyeweza kudhibiti vyama vya ushirika na mfumo mzima wa ununuzi na uuzaji wa pamba,

Utaratibu wake ndio ambayo uliwafanya wakulima kuuza pamba yao bila kukopwa na hata kuuzwa wanakotaka na Udhibiti huu ulisaidia pamba kuuzwa kati ya TZS 1,800 kwa kilo hadi TZS 2,200.

Bei hizi hazijawahi kutokea tangu uhuru wa nchi yetu ( No Cash No Cotton )

Kafulila huyu huyu akiwa mkuu wa Mkoa wa Simiyu alimrudisha mkandarasi wa Kichina kurudia barabara ya Mwigumbi- Maswa, yenye zaidi ya urefu wa kilomita 20 kwa zaidi ya TZS 40 bilioni baada ya kujengwa kinyume na mkataba halafu mtu anauliza Je, ni Kafulila yule yule!?

Kafulila huyu huyu alimnyang’anya mwekezaji umiliki wa Soko la madini kisheria na kulikabidhi kwa halmashauri ya mji wa Bariadi nendeni mkawaulize.

Hata hivyo, Mimi Kafulila nimekuwa kamishna wa PPP ndani ya wizara ya fedha kwa mwaka mmoja wa 2023.

Sasa ni Mkurugenzi wa kituo cha UBia ambacho kinajitegemea kiutendaji ( PPP Center ) hapa namshukuru Mhe Rais Samia pamoja na Wasaidizi wake kwa kuendelea kuniamini nami kamwe sitowaangusha Watanzania.

Kama Mkurugenzi niiliahidi kuhakikisha ndani ya mwaka mmoja, miradi ya PPP kwa Sera na Sheria ya PPP inaanza kupatikana baada ya kukwama kwa zaidi ya miaka 15 ya Sera ya mwaka 2009.

Na taarifa njema kwa Taifa ni kuwa kabla ya kufunga mwaka huu wa fedha – Juni 24, tutakuwa tayari tumesaini miradi mitatu mikubwa ya UBia,

Hakika Mama amelifungua Taifa kazi yetu Sisi Wazawa ni kuchagua fursa tunazozitaka na kuzimudu.​

2010-2015 Kafulila alikuwa moto mkali.
Namwombea apate tena Ubunge 2025 tukapate Bunge vibrant
 
David Kafulila, David Silinde, John Mnyika, Halima Mdee, John Heche na Zitto Kabwe hivi vichwa ambavyo vimepikwa vizuri sana kisiasa na kiutawala, hawa wote wana weledi wa kutosha na sidhani kama kuna yoyote anaweza kuja kushindwa popote iwe chama tawala au upinzani..

Hiki ni kizazi cha dhahabu kilichowahi kutokea na kupikwa na Mhe. Freeman pale chadema, si ajabu kuendelea kuona hata Kafulila bado ni mtendaji mzuri.
 
Nafikiri Bw. Kafulila anachanganya mambo kuhusiana na suala la UBIA. Sidhani kama anaielewa vyema dhana ya neno Ubia, kuanzia maana yake, aina zake na namna jinsi unavyofanya Kazi. Namshauri akasome Sheria ya Mikataba ya Tanzania,hususani ile sehemu inayohusika na masuala haya ya UBIA ili Aelewe vizuri kuhusiana na suala hili.
Vile vile, asome Sheria ya Masuala haya ya UBIA ya Tanzania ili aelewe vizuri zaidi kuhusu suala hili.
Wewe ndiye hufahamu lolote kuhusu ubia maana haujaeleza chochote kuhusu maana ya ubia
 
Naona ashatengeneza exit door mambo yakienda kombo, kuwa huo mchakato wakati ukianza hakuwepo

Ila bado sijaona hoja nzito alizojibu badala yake ameishia kujisifia tu

Ila ili habari iwe balance tungeletewa na hoja za Kubenea
Habari ya kubenea huijui alafu unasema hajajibu hoja. Tanzania wajinga ni wengi aisee
 
Hakika Mama amelifungua Taifa kazi yetu Sisi Wazawa ni kuchagua fursa tunazozitaka na kuzimudu.

Hii kauli ya mama amefungua taifa, kidogo inanipa shida.
hivi ni nani aliyefunga? serikali ya chadema? au ccm?
Kwani si ni ninyi nyinyi mlio kuwa mkiimba nyimbo za pambio na kusifu kipindi kile kama mfanyavyo sasa?
Mimi pia hii kauli na za namna hiyo huwa zinanitia kichefuchefu sana hata kama ufafanuzi wa hoja zake ulikuwa na facts, hizi ni kauli za kubeza utawala uliopita wakati yeye ni shahidi na mnufaika wa utawala uliopita alipoanza kuteuliwa RAS Songwe akitokea upinzani. Pamoja na usmart alionao hizo kauli za kukashifu utawala uliopita eti nchi ilikuwa kama imefungwa how&why.....huu ni uchawa usiokuwa na maana kwa mtu smart km Kafulila. Hoja zake zimeshaeleweka.
 
Angalizo
Pamoja mwekezaji/mbia ENG kukidhi taratibu/sifa za kiushindani, ni vizuri serikali ikachukua tahadhari za kila sekta za kiuwekezaji/PPP kuwapa wawekezaji wa kutoka nchi Moja husisani falme za kiarabu kama ilivyo kwa Sasa ENG na DP world wote kutoka uarabuni. Hii ikiendelea kutamalaki ktk sekt nyingi nadhani ni hatari kwa usalama wa nchi lkn pia harufu ya rushwa kubwa kubwa/mega corruptions. Ni vzr serikali ikachukua tahadhari hii.
 
Kama unakubali kuwa Kafulila ni smart amini pia anapokwambia kuwa Mama ameifungua nchi .
 
Angalizo
Pamoja mwekezaji/mbia ENG kukidhi taratibu/sifa za kiushindani, ni vizuri serikali ikachukua tahadhari za kila sekta za kiuwekezaji/PPP kuwapa wawekezaji wa kutoka nchi Moja husisani falme za kiarabu kama ilivyo kwa Sasa ENG na DP world wote kutoka uarabuni. Hii ikiendelea kutamalaki ktk sekt nyingi nadhani ni hatari kwa usalama wa nchi lkn pia harufu ya rushwa kubwa kubwa/mega corruptions. Ni vzr serikali ikachukua tahadhari hii.
Mkuu nadhani Ndio maana haya maridhiano yanachukua muda mrefu
 
Angalizo
Pamoja mwekezaji/mbia ENG kukidhi taratibu/sifa za kiushindani, ni vizuri serikali ikachukua tahadhari za kila sekta za kiuwekezaji/PPP kuwapa wawekezaji wa kutoka nchi Moja husisani falme za kiarabu kama ilivyo kwa Sasa ENG na DP world wote kutoka uarabuni. Hii ikiendelea kutamalaki ktk sekt nyingi nadhani ni hatari kwa usalama wa nchi lkn pia harufu ya rushwa kubwa kubwa/mega corruptions. Ni vzr serikali ikachukua tahadhari hii.
😍😍💪🏿💪🏿👋🏿
 
Mimi pia hii kauli na za namna hiyo huwa zinanitia kichefuchefu sana hata kama ufafanuzi wa hoja zake ulikuwa na facts, hizi ni kauli za kubeza utawala uliopita wakati yeye ni shahidi na mnufaika wa utawala uliopita alipoanza kuteuliwa RAS Songwe akitokea upinzani. Pamoja na usmart alionao hizo kauli za kukashifu utawala uliopita eti nchi ilikuwa kama imefungwa how&why.....huu ni uchawa usiokuwa na maana kwa mtu smart km Kafulila. Hoja zake zimeshaeleweka.
😍😍💪🏿💪🏿👋🏿
 
View attachment 2967024

Na. David Kafulila

NIMELAZIMIKA kushika kalamu ikiwa ni baada ya kusukumwa na andiko la ndugu na jamaa yangu wa miongo mingi na aliyepata kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mhe Saed Swedi Kubenea.

Mhe Kubenea amejadili kuhusu mradi wetu wa BRT unaotarajiwa kuendeshwa na kampuni ya ENG ya Dubai.

Mhe Saed Kubebea ameandika Makala iliyobeba kichwa cha maneno: “ Kafulila wa Escrow ndiye huyu wa UDART? ”

Mimi David Kafulila baada ya kuisoma makala hiyo, nimejiridhisha kuwa kuna maeneo mwandishi hajanielewa au haelewi vizuri.

Mwandishi huyu amejaribu kujenga mashaka ya alichokiita " Hatari ya kampuni ya Dubai kupewa kazi ya kuendesha UDART " Shirika linalomilikiwa na Serikali na kampuni binafsi ya Simon Group Limited.

Binafsi nikiri kuwa nimependa namna mwandishi Saed Swedi Kubenea alivyowasilisha maoni yake kwani yameamsha mjadala wa Ubinafsishaji, Ubia na nafasi ya wazawa katika Umiliki na Uendeshaji wa Uchumi wa Taifa lao.

Kwakuwa mjadala huu ni mpana, naomba leo nieleze mambo Saba ( 7 ) kwa ajili ya kutoa ufafanuzi ili kuwatoa hofu Watanzania akiwemo Ndugu yangu Saed Kubenea.

Na ieleweke kwenu pia nitakayoyaeleza hapa, baadhi ni maoni yangu binafsi, hasa kuhusu dhana nzima ya Ushiriki wa Sekta binafsi ya Ndani na Nje katika kujenga Uchumi Shirikishi na Jumuishi.

Kwanza, nataka sote tuelewe kuna tofauti kubwa kati ya Ubinafsishaji na Ubia.

Mikataba yote ya Ubia duniani – Mali au Aseti zote zinamilikiwa na Serikali husika Kabla, wakati na hata baada ya mkataba vile vile Mikataba ya Ubia haihamishi umiliki wa mali au aseti.

Sikilizeni, Kwa mfano, Ubia kati ya DART na kampuni ya ENG, haimaanishi DART itakuwa imeuzwa au kuhamisha umiliki wa barabara au magari yake.

Kinachofanyika hapa muwekezaji ataleta mabasi yake na kuyaendesha kwa gharama zake huku Serikali ikipatiwa huduma kwa watu wake na masilahi mengine kulingana na mkataba husika.

Nimuulize swali Mhe Kubenea,
Kama Mbia ataleta magari yake na kuyaendesha hapo Serikali itakuwa imeuza rasilimali gani ya Taifa Kwa ENG?

Hata hivyo ni muhimu kufahamu kuwa Usafirishaji kwa njia ya barabara nchini unaendeshwa na sekta binafsi kwa miongo yote sasa, ukiondoa sehemu chache kama ilivyokuwa miradi ya UDA.

Pili, kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa DART ya wiki jana, Taratibu za Serikali kutafuta Mbia kuleta mabasi na kuyaendesha zimeanza tangu mwaka 2017.

Katika mchakato huo, zaidi ya makampuni 30 yalijitokeza lakini hakupatikana muwekezaji mwenye sifa na tija kwa Taifa.

Mchakato huo ukarudiwa tena mwaka 2020, Safari hii Makampuni takribani 40 yalishiriki na hapa ndipo ENG ikaibuka mshindi na kuanza majadiliano na Serikali ya kuendesha mradi huo na majadiliano hayo yalianza mwaka 2022 hata mimi nilipoipewa nafasi hii mwaka 2023 mradi huu upo.

Tatu, Ni bahati mbaya kwamba majadiliano haya yamechukua muda mrefu kutokana na changamoto za kisheria kwani DART & ENG walikuwa wakivutana kuhusu namna bora ya kuhitimisha makubaliano yao kwa masilahi mapana ya Taifa la Tanzania na Watanzania.

Mara zote, tumeendelea kupata ushauri kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kwa lengo la kuhakikisha tunafikia Mkataba wenye masilahi mapana kwa taifa letu na unaolindwa na sheria zetu.

Nne, mradi wa BRT una njia sita, Njia ambayo inajadiliwa na kampuni ya ENG ya Dubai, ni ya kwanza ( Phase I ) ambayo inahusisha kuwapo mabasi 177 yatakayonunuliwa na kampuni hiyo ya ENG.

LAZIMA pia tufahamu, Mabasi yote haya yatakayonunuliwa baada ya mkataba kumalizika, yatakabidhiwa kwa Serikali kabla hayajachoka na kisha wao kuingiza mengine mapya.

Lengo la Serikali na Rais Samia ni kuhakikisha kunakuwa na ubora wa huduma kwa Wanadalesalaam hasa Wapenzi wa Mwendokasi.

Hata hivyo, ujio wa ENG hauindoi UDART bali utaipa kampuni hii ya Serikali na wazawa changamoto katika ubora wa huduma ( a competitive business )

Tano, njia zingine tano bado DART wataendelea na mchakato wao wa kupata wawekezaji kwa utaratibu. wa aina hiyo hiyo.

Njia ya pili ( Phase II ) itahitaji uwekezaji mkubwa zaidi kwani kunatakiwa mabasi 770.

Hii ni fursa kwa wawekezaji wote na hususan wa ndani.

Nakubaliana na hoja ya umuhimu wa kampuni za ndani kupewa fursa hii.

Nakubaliana na hoja ya kuzisaidia kampuni za ndani kupata fursa hii na hata hivyo, ni muhimu tukubaliane kusiwe kwa gharama kubwa. kwa wananchi wanaotumia usafiri huu.

Asilimia 43 ya wakazi wa Dar es Salaam wanafanya kazi maeneo ambayo wanatembea kwa mguu kwa sababu ya changamoto ya nauli.

Hii inawanyima fursa wao binafsi, lakini pia uchumi kwani nguvu kazi hiyo inaweza kuzalisha zaidi ikimudu kufanya kazi zaidi ya umbali huo.

Unafuu wa nauli na ubora wa huduma ni muhimu sana ili kuhakikisha nguvu kazi ya Dar es Salaam inazalisha na jiji linaunganishwa kwa Usafiri wa Uhakika.

Sita, Napenda kutoa wito kwa kampuni za wazawa zenye nia ya kuwekeza eneo hili, waoneshe nia na tuwasaidie kuwekeza kwenye fursa hizi za BRT hata kabla ya DART kutangaza.

Sheria inaruhusu wawekezaji kuleta mapendekezo kabla ya zabuni kutangazwa.

Anachopaswa kukizingatia, ni kwamba anapaswa kuleta mapendekezo yake kama UNSOLICITED.

Njia hii inatumika kwa miradi yote mwekezaji anapoona Serikali haiwezi kuendesha kwa ufanisi, anaruhusiwa kuomba kazi hiyo na atasaidiwa kwa mujibu wa sheria.

Lengo ni kuhakikisha serikali inavutia mitaji, teknolojia na weledi.

Kwamba, Sekta binafsi inatumika kutekeleza baadhi ya majukumu ya serikali kwa ufanisi ili yenyewe ibaki na majukumu muhimu ya kuhudumia wananchi.

Lazima watu waelewe, Sheria ya PPP na hata ile ya manunuzi, zinatoa upendeleo kwa wazawa zaidi.

Serikali inatoa upendeleo wa kisheria na inazijengea uwezo kampuni hizo, ili ziweze kusimama zenyewe, kutokana na kutambua mchango wake kwa uchumi wa taifa Kwa muktadha huo,

Saba, Baada ya ufafanuzi huu wa kina naomba nisisitize kwamba David Kafulila huyu ni yule yule wa Jana, Juzi na Leo,

Kafulila huyu wa UDART ni yeye yule aliyekuwa Mbunge machachari toka Jimbo la Kigoma Kusini ( 2010 - 2015 ).

Kafulila huyu baadae akateuliwa kuwa Katibu Tawala wa mkoa Songwe, aliyesimamia kisawa sawa nidhamu ya Fedha za Umma, Kuichukia rushwa na uwajibikaji kwa halmashauri zake zote.

Ni huyu Kafulila aliyekuwa Katibu Tawala wa kwanza kuvunja mkataba wa Mshitiri wa usambazaji dawa kwenye Mkoa wa Songwe kufuatia kuibuka kwa madai ya udanganyifu.

Mtakumbuka piq, Baada ya kuvunjiwa mkataba ule, muhusika alikwenda hadi Mahakama kuu ambako nako alishindwa kesi zote.

Ni Kafulila yule yule ambaye akiwa mkuu wa mkoa wa Simiyu, mkoa ambao asilimia 70 ya Pamba ya Tanzania inatoka huko.

Niyeye Kafulila aliyeweza kudhibiti vyama vya ushirika na mfumo mzima wa ununuzi na uuzaji wa pamba,

Utaratibu wake ndio ambayo uliwafanya wakulima kuuza pamba yao bila kukopwa na hata kuuzwa wanakotaka na Udhibiti huu ulisaidia pamba kuuzwa kati ya TZS 1,800 kwa kilo hadi TZS 2,200.

Bei hizi hazijawahi kutokea tangu uhuru wa nchi yetu ( No Cash No Cotton )

Kafulila huyu huyu akiwa mkuu wa Mkoa wa Simiyu alimrudisha mkandarasi wa Kichina kurudia barabara ya Mwigumbi- Maswa, yenye zaidi ya urefu wa kilomita 20 kwa zaidi ya TZS 40 bilioni baada ya kujengwa kinyume na mkataba halafu mtu anauliza Je, ni Kafulila yule yule!?

Kafulila huyu huyu alimnyang’anya mwekezaji umiliki wa Soko la madini kisheria na kulikabidhi kwa halmashauri ya mji wa Bariadi nendeni mkawaulize.

Hata hivyo, Mimi Kafulila nimekuwa kamishna wa PPP ndani ya wizara ya fedha kwa mwaka mmoja wa 2023.

Sasa ni Mkurugenzi wa kituo cha UBia ambacho kinajitegemea kiutendaji ( PPP Center ) hapa namshukuru Mhe Rais Samia pamoja na Wasaidizi wake kwa kuendelea kuniamini nami kamwe sitowaangusha Watanzania.

Kama Mkurugenzi niiliahidi kuhakikisha ndani ya mwaka mmoja, miradi ya PPP kwa Sera na Sheria ya PPP inaanza kupatikana baada ya kukwama kwa zaidi ya miaka 15 ya Sera ya mwaka 2009.

Na taarifa njema kwa Taifa ni kuwa kabla ya kufunga mwaka huu wa fedha – Juni 24, tutakuwa tayari tumesaini miradi mitatu mikubwa ya UBia,

Hakika Mama amelifungua Taifa kazi yetu Sisi Wazawa ni kuchagua fursa tunazozitaka na kuzimudu.​
Unafuu wa nauli na ubora wa huduma ni muhimu sana ili kuhakikisha nguvu kazi ya Dar es Salaam inazalisha na jiji linaunganishwa kwa Usafiri wa Uhakika.

Ila Kafulila Yuko vizuri sana huyu kijana anastahili kulitumikia Taifa kwa nafasi ya juu.
 
Back
Top Bottom