Kuanzia sasa Ubunge iwe kazi ya kujitolea(wito)

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
Kwa hali ninavyoiona tunahitaji kupunguza matumizi ya serikali na kuongeza uwajibikaji.tujaribu kufanya kazi ya ubunge au uwakilishi wa wananchi iwe kazi ya kujitolea,hii itasaidia kutenganisha siasa na biashara na itasaidia wananchi kupata wawakilishi wenye uzalendo na wanaojua shida za wananchi hata wanapokuwa mjengoni.isitoshe wabunge sio 'productive' kama ilivyowahi kusemekana madaktari hawazalishi.nina uhakika serikali ingejipanga kabla ya kuja bungeni na hoja nyepesi!pia itapunguza wimbi kubwa la nguvukazi ya taifa(wataalamu)kukimbilia mjengoni badala ya kuhudumia wananchi na kuongeza uzalishaji.watanzania tuko wengi na wengi wetu ni wazalendo tunaoweza kwenda kuwakilisha wananchi bila POSHO yoyote.
 
Wabunge mliomo humu kwa nini muendelee kulipwa maposho mengi wakati mnatambua nchi yetu ni maskini?
 
Back
Top Bottom