Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,744
Sijui kilichosemwa mpaka ikafikia kuwa mchakato huo wa Katiba mpya usitishwe hadi baada ya uchaguzi mkuu ,suali ni jee utafutaji huo wa Katiba mpya utaanza ulipofikia au utaanza upya ?
Wananchi tunataka ukweli juu ya maoni tuliyoyatoa na kumkabidhi jaji Warioba na kundi lake ,Je ni maoni hayo ndio yatakayojadiliwa au ni makaburasha walioingia nayo Miccm ?
Tunahitaji kujua walichokubaliana ni kipi ? Hii katiba inayotafutwa si ya watu kujifungia na kutoka na heading ya maafikiano bila ya kujua kilichopelekea hata kufikia kutoa heading ni kitu gani ,Je inawezekana kuwa mchakato wa Katiba hauwezi kuanza tena upya hivi sasa kwa kuwa muda hautoruhusu au hicho kilichobakia hakiwezi kuhitimishwa japo hicho sicho kwani ahadi ya Sita ni kumkabidhi Mheshimiwa Kikwete Katiba mpya mwezi wa kumi mwaka huu.
Miccm imemaliza kasiki la Taifa na sasa wanamtwisha mzigo raisi mpya atakaekuja ,tutawafungulia mashtaka msifanye mchezo na hela ya taifa kana kwamba mnagawa visheti. Mlijua tokea mwanzo baada ya UKAWA kuchemka kuwa KATIBA haitopatikana ,ila mkaendelea kugawana hela za Taifa mkiita posho ,posho lakitatu kwa siku hata hizo nchi tajiri hazifanyi kufuru hiyo.
Wananchi tunahitaji kujua kilicho au kitakachoahirishwa na kuja tena ni kitu gani ???