"Kuagana"

majuti ni mjukuu, babu yangu aliniasa
nenda wangu mjukuu, uachane na anasa
ukaweke lango kuu, ukafunge na vitasa
kama imekuwa fasheni, nani wa kulaumiwa?

vionjo unavitaka, ndoa unaitaka
wafanana na maji taka, yangu ndio mashaka
hata utoe zaka, milele una mashaka
kama hukuwa tayari, uliharakia nini?
Uko fiti aisee
 
Baada ya kuongea na rafiki zangu kadhaa, nimegundua kwamba ''Kuagana" imekuwa fasheni siku hizi.....Labda nawahukumu bure....

Ndoa ni kitu tukufu, misahafu ni shahidi,
Yataka moyo mkunjufu, hakuna mlio wa bundi,
Zawadi kama mikufu, tuzo njema kwa ushindi,
Kuagana na wa zamani, siku hizi imeshakuwa fasheni?

Zamani likuwa sifa, heshima liwekwa mbele,
Binti alifundwa vyema, katu sipige kelele,
Uwanja safi daima, watoto sipate upele,
Kuagana na wa zamani, siku hizi imeshakuwa fasheni?

Ndoa meingia doa, leo kuna kuagana,
Siku muhimu ya ndoa, wa zamani anapewa,
Penzi kama kukohoa, ni tabu kwa waungwana,
Kuagana na wa zamani, siku hizi imeshakuwa fasheni?

Kama wa zamani mzuri, kwanini hakukuoa,
Ka anukia uturi, nenda kapeleke posa,
Kwao huyu umekiri, kwa yule nataka poza,
Kuagana na wa zamani, siku hizi imeshakuwa fasheni?

Fungate haina mvuto, viungo vimelegea,
Ndoa sasa ni kipato, na bado utamegewa,
Ni moto pia fukuto, la upate ngekewa,
Kuagana na wa zamani, siku hizi imeshakuwa fasheni?

Mkuu hongera ....
 
Hili jambo ni la kweli ila ndoa nyingi ambazo wadau wameptia huo mchakato ziko ICU au tayari ni RIP.

Mzee DC
 
:confused2:
Kuagana yumkini,si jambo baya jamani,
Tatizo ni timing,na malengo yaliyo ndani,
Huyo wako mwafulani,ni busara aganeni,
Kabla usajili mpya,aganeni kwa amani.

Zilikuwamo hasara,kwenye penzi mlozama,
Mkaona ni busara,kuachana kwa salama,
Sipeperuke ki-tiara,tulieni ninasema,
Kabla usajili mpya,aganeni kwa amani.

Ukishakuwa mwenyewe,bila mpenzi hakika,
Utajipenda mwenyewe,kutafuta muafaka,
Usiruke kama mwewe,kwa wapenzi kuzunguka,
Kabla usajili mpya,aganeni kwa amani.

Ukijisoma mwenyewe,matatizo tagundua,
Usipatwe na kiwewe,suluhisho tafutia,
Ujipe muda mwenyewe,kisha hatua chukua,
Kabla usajili mpya,aganeni kwa amani.

Huyo mpya uanzapo,yalopita elezea,
Uwe wazi kwa mwenzako,misimamo jiwekea,
Asomapo tabia zako,na za kwake chungua,
Kabla usajili mpya,aganeni kwa amani.

Tabia ukiridhia,usajili fatilia,
Mpe wako maridhia,ulomnyima tangia,
Mbona alikungojea,muda mrefu twasikia?
Kabla usajili mpya,aganeni kwa amani.

Mapenzi yakishamiri,ndoa mkaitamani,
Alopita ni shubiri,kwake wafata nini?
Kumre-call sishauri,utakuwa hayawani,
Kabla usajili mpya,aganeni kwa amani.

Wana JF semeni,mnaaga wara ngapi?
Mi nimefika pomoni,hii staili ya wapi?
Nasema tafakarini,mbeleni twaenda wapi?
KABLA USAJILI MPYA,AGANENI KWA AMANI.
 
siku hizi watu hawana condidence kabisaa na ndoa,kila mtu amekaa kimachale machale/anaibiwa....msifunge ndoa kama mko uncertain:majani7:
 
Mwenzangu inabidi na sie tujifunze maana kila nikitaka kutoka nakwamia njiani na cancel

Anza taratibu, jaribu hata mstari mmoja kwanza.Usi-cancel hata kama unaona hujaandika vizuri-just post it. Nakuhakikishia, baada ya muda mfupi utaweza na kufurahia. Mwanzoni, mizani unaweza ukaipotezea mpaka utakapojenga kujiamini. Ukijisomea machapisho ya kiswahili mara kwa mara unaweza ukajiongezea misamiati na hivyo kuandika kwa urahisi mashairi.
 
Big up Ngondya,hata mimi sijasomea chochote kwenye ushairi zaidi somo la kiswahili la primary school and "O" level.

Msiogope kujaribu,tena utaona misamiati na maneno yanaflow tu,ndicho kinachonitokea mimi.:smiling:
 
siku hizi watu hawana condidence kabisaa na ndoa,kila mtu amekaa kimachale machale/anaibiwa....msifunge ndoa kama mko uncertain:majani7:

Ni kama watu wanataka kutoa gundu vile. Mtu anaona rafiki zake wote wameoa/olewa basi na yeye anataka kulazimisha afunge ndoa wakati hajampata mwenza anayempenda kwa dhati. Unakutana na mtu from nowhere, baada ya miezi 6, unatangaza ndoa, hapo lazima shida itatokea.. Maisha yamebadilika, tujifunze kukubaliana na hali halisi-kama hujampata wa moyoni usilazimishe-don't be desperate!
 
Big up Ngondya,hata mimi sijasomea chochote kwenye ushairi zaidi somo la kiswahili la primary school and "O" level.

Msiogope kujaribu,tena utaona misamiati na maneno yanaflow tu,ndicho kinachonitokea mimi.:smiling:

Ni kweli kabisa, mfano mzuri ni Mjomba Mpoto, anavyoongea ni kama amekaa darasani sana kuisomea lugha hii, lakini ukweli ni kwamba amejifunza mengi kwa kujisomea mwenyewe nyumbani. Ukijifunza kuandika, unakuwa unafurahia-inakuwa kama hobby.
 
Ni kweli usemacho, labda watu wengi wanaogopa kujaribu, mimi nimekuwa inspired na mashairi humu humu JF, na sasa ninathubutu kusema naweza kuandika angalau beti moja and i'm still learning from others, kuna watu humu ambao wamebobea kwenye ushairi nafikiri pia wanaweza kutusaidia zaidi

Ni kweli kabisa, mfano mzuri ni Mjomba Mpoto, anavyoongea ni kama amekaa darasani sana kuisomea lugha hii, lakini ukweli ni kwamba amejifunza mengi kwa kujisomea mwenyewe nyumbani. Ukijifunza kuandika, unakuwa unafurahia-inakuwa kama hobby.
 
Nimeipenda hiyo: ulimwengu wa wizi na risk ya kufumaniwa
Mmmh, kuna ukweli ndani yake. Kabla ya send off anaagwa nusu, kabla ya harusi anaagwa full, baada ya ndoa anakaribishwa kwenye ulimwengu wa wizi na risk ya kufumaniwa.
 
Back
Top Bottom