Kreni zote zimeharibika Bandarini

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Mtakuwa mnashangaa kuona meli zimanza kujazana tena..basi ukweli ni kuwa zilishakaa muda mrefu na zikaamua kuondoka

sasa wakaongopewa na TICS kuwa zimepona kumbe zimeharibika zote

wameishia kukodi moja toka TPA kati ya 2 walizokuwa nazo na nasikia jana nalo liligoma

sasa kama ulithubutu kuagiza kontena lako basi mtasubiri mpaka mwezi wa 7

Mgawe na bodi ya Habaz bado wanakula kuku tuuu

ndio hivyo

mida basi
 
Kwani raisi aliposema bandari ifanye kazi usiku na mchana, hawakufikiria vitendea kazi! Raisi anapotoa matamko ahakikishe wanasimamiwa, na watendaje waweze kuwa na plan B basi!
 
Kwani raisi aliposema bandari ifanye kazi usiku na mchana, hawakufikiria vitendea kazi! Raisi anapotoa matamko ahakikishe wanasimamiwa, na watendaje waweze kuwa na plan B basi!

Yeah, maybe zitakuwa zimeharibika kwa kuwa hazikuwa zinapumzishwa; zilifanya kazi usiku na mchana !!!
 
Kuchelewa kulikuwa kunawapa watu kula; kwa hiyo sishangai kusikia zote zimeuawa.
 
Yeah, maybe zitakuwa zimeharibika kwa kuwa hazikuwa zinapumzishwa; zilifanya kazi usiku na mchana !!!

Nahisi mzigo wa Kreni huo watakuwa walinunua China kwa kukwepa gharama zile za Mgerman.
 
Eti wanaforum, hili linawezekana kabisa....Raisi wetu anajua analolifanya jamani.

Mkuu nyamaza hivyo hivyo ukisema ooooooh shiiiiiiiiiiii endelea kumsifia 2010 hakuna mwingine ni JK tu tuimbe na kumpamba....
 
Yeah, maybe zitakuwa zimeharibika kwa kuwa hazikuwa zinapumzishwa; zilifanya kazi usiku na mchana !!!

Tabu kweli! Mbona za wenzetu haziharibiki? Utakuta hatuna mpango wa maintanance, maintanance mpaka tuunde tume na tutafute msaada!
 
Yeah, maybe zitakuwa zimeharibika kwa kuwa hazikuwa zinapumzishwa; zilifanya kazi usiku na mchana !!!

Na labda kama kawaida yao walinunua ma-used one na yalikuwa mabovu since day 1 (Ilikuwa ni suala la muda tuu yaharibike)
 
Hamna lolote hawa ni sabotage tu! Na bado mwisho watasema na bandari ifungwe kabisa!
 
Maajabu hayo! Tunataka tuwe na maendeleo wakati hatuna mpangilio. Sasa inabidi atoke waziri aende ulaya akaombe msaada wa cranes, wataalamu wa kuzifix na pesa za kuwalipa kwa kazi yote ikiwa na fidia ya wenye mizigo inayolala hapo port. Kwa kawaida, wenye mizigo bandarini wanapaswa walipwe fidia kwa kuwa si kosa lao kwa bandari kukosa pembejeo za kufanyia kazi. Kila siku USD dola 50, hadi mzigo utapotolewa! Kumbukeni: Sheria ni msumeno!
 
Labda tuna ma-engineer ucharwa wasioelewa trouble shooting na kuzikwamua ndani ya saa au siku moja...
 
Tanzania shaghala bhaghala; siamini Bandari kuu inakodisha cranes?haina cranes zao wenyewe...na kila siku inaingiza mamilioni...wapo radhi kugharamia mashangingi; BMWs rather than infrastructure...Hapo ni sawa na kuanza kununua kabati wakati kitanda huna!
 
Yeah, maybe zitakuwa zimeharibika kwa kuwa hazikuwa zinapumzishwa; zilifanya kazi usiku na mchana !!!

Hongera kwa ufanyaji kazi wao mzuri, lakini, juhudi zao zinarudi shimoni na mlundikano utarudi kwa kushidwa kuwa na plan b. Ni jambo lililowazi kabisa kwamba ukifanyisha kazi mashine kuzidi uwezo wake itakufa! Ikifa tufanyaje? Tuazime, tuliyoazima imekwama pia! Tafuta nyingine, inawezekana wanatafuta sasa! Lakini watafute wakiwa na utambuzi, uzito wa kazi ni mara mbili zaidi ya machine kwahiyo wawe na backup plan!
 
Labda tuna ma-engineer ucharwa wasioelewa trouble shooting na kuzikwamua ndani ya saa au siku moja...

Uki troubleshoot ukawaambia New Part inahitajika, wakati huo huo Management inaamini kwamba Amchines were made to last forever, watakuelewa??!?

Preventive Maintanance na Maintanance in general ni msamiati kwenye shughuli zetu za uongozi na utawala.

Nyumba tulizo zitaifisha miaka ya 70 hazikuwahi kufanyiwa ukarabati mpaka tulizo zirudisha kwa wenyewe.

Maghari ya serikali kamwe hayafanyiwi ukarabati ila ubabaishaji ili fedha za ukarabati ziingie mifukoni.
Barabara zetu hazifanyiwi ukarabati wa maana kwa sababu viongozi wanaamini zitadumu hadi siku ya kurudi Yesu Masihi.

Mabomba ya maji na pampu za maji pia hazifanyiwi ukarabati kwa kuamini kwamba hazitapata hitilafu wala hazitachakaa, na mara nyingi zikiwa katika hali hiyo ya uchakavu tumekuwa tukiziongezea mzigo wa kuzarisha maji zaidi bila kujali ushauri wa kitaalamu.

Ofisi za serikali, Hospitali na vifaa vyake Pantony.

Pia viongozi wanaamini kwamba hata wao waliwekwa hapo wadumu milele hawatakiwi kustaafu wala kuacha wengine wenye uwezo na upeo mpya waonyeshe CHECHE ZAO ZA FIKRA.
 
Mbona kabla ya TICTS, ingawa kulikuwa na matatizo ya hapa na pale kama sehemu nyingi Tanzania, mambo hayakuwa chronic hivi?
 
Hawa watu wana usingizi usio na kikomo kwa kweli. Alikwenda kufanya nini bandarini halafu kelele nyingi ninayo majina kiko wapi. Hii nchi inaendeshwa kama michezo ya kuigiza vile.Mkuu umeshindwa kazi nchi inadidimia siku hata siku kazi kufanya ziara zisizo na mguu wala kichwa. FUKUZA KAZI WATU WOTE BANDARINI KUANZIA MENEJA MPAKA MFAGIAJI KIELEWEKE HUU NI UZEMBE ULIOKITHIRI.Halafu mnataka kusingizia uchumi uchumi hizo porojo porojo zenu zina mwisho wake.Mkuu anza kufanga virago umetuchosha
 
Eti wanaforum, hili linawezekana kabisa....Raisi wetu anajua analolifanya jamani.

Rais wetu hana tofauti na chekibudi au zembwela, yaaani yupo yupo tu. Ndo yale ya kusema ATC ipewe hela na ianze tu kurusha ndege hata kesho kisha still nasikia marubani wamegoma kisa salaries. Ama kweli Rais rahisi tunaye!!
 
hizo kreni tutatumia kwenda kunyanyua nyumba zao masaki, mikocheni,mbezi beach n.k halafu tuone kama watasema zilikuwa mbovu. hizi story wameshindwa kazi ni visingizio hawa watu wana maigizo
 
Back
Top Bottom