Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
- Thread starter
- #21
Mh. Halima mdee amemaliza kuongea.
Kwa ufupi amezungumzia mchakato mzima wa upitishwaji wa muswaada kuanzia kwenye kamati ya bunge ambapo spika alikiuka kanuni za bunge na kuongeza wajumbe watano baada ya hoja ya kutaka muswada usomwe kwa mara ya kwanza kuelekea kukubaliwa na wajumbe wa kamati ya sheria na katiba. Pia amezungumzia spika alivyopora madaraka ya kamati na kufanya maamuzi na watu wake wachache ili kuhakikisha muswada unapita.
Pia amefichua siri kwamba baada ya yeye na mh. Lisu kuainisha mapungufu ya sheria ya mchakato wa katiba, wabunge wa ccm walikiri mapungufu hayo lakini wakadai wameelekezwa kuupitisha muswada kama ulivyo.
Ameeleza sababu ya kuweka kipengele cha adhabu kwa mtu mwingine yeyote atakayetoa elimu ya uraia juu ya mchakato wa katiba ni kwa nia ya kuwadhibiti chadema baada ya kugundua kwamba chadema watatumia mapungufu ya sheria hii kuwaelimisha wananchi na huenda katiba ''mpya'' wanayotaka wao isipitishwe.
Amemalizia kwa kusema chadema tuko tayari kwa lolote maadam tunatekeleza wajibu wetu wa kikatiba.