Kongamano la Jukwaa la Fikra Kuhusu Mabadiliko ya Digitali - Juni 20, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989


Mazungumzo haya yameratibiwa na Mwananchi Communications Ltd (MCL) yanajadili umuhimu wa kusudio kubwa katika mageuzi ya kidigitali na ushirikiano kati ya sekta za umma na binafsi katika kufikia kusudio hilo.

Tukio hili limewakutanisha viongozi wenye ushawishi, watunga sera, wasomi, wajasiriamali, na wavumbuzi kutoka sehemu mbalimbali ili kushiriki katika mazungumzo yenye maana kuhusu kuendesha mageuzi ya kidigitali kwa ajili ya mustakabali bora.

Mususa.jpg

Leonard Mususa
Leonard Mususa, Mwenyekiti wa bodi MCL
Amesema kuna umuhimu wa Serikali na Sekta binafsi kushirikiana na vijana katika kuchochea ubunifu wa teknolojia mbalimbali za kidijitali ili kupata matokeo chanya na bunifu zenye tija katika sekta zote.

“Tunahitaji pia kuona vipaji vinavyotokana na digitali, kuunga mkono startups na kuhakikisha teknolojia ya digitali inatumika katika nyanja zote na kusaidia kuzalisha ajira”

Mkurugenzi wa Sera za Umma (GSMA), Caroline Mbugua
Mbugua amewasilisha matokeo ya utafiti uliofanywa na GSMA, shirika la kimataifa linaloshughulikia mfumo ikolojia wa simu, ambayo yanaonesha kwamba idadi kubwa ya Watanzania bado hawajajiunganisha na huduma ya Pesa Mtandao (Mobile Money) ambayo inaweza kusaidia kuboresha biashara na maendeleo ya jamii.

Tanzania inaonekana kuwa na viwango vya juu vya ushuru kuliko nchi nyingine zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara, kwani inatoza ushuru wa asilimia 47 kwenye huduma ya Pesa Mtandao.

Tanzania ina asilimia 52 tu ya watu wazima wanaotumia Pesa Mtandao, ambayo ni kiwango cha chini ikilinganishwa na nchi kama Uganda yenye asilimia 66, Kenya yenye asilimia 79, na Afrika Kusini yenye asilimia 85.

Amesema asilimia 83 ya Tanzania imeunganishwa na huduma za mtandao na asilimia 63 ya watu ndiyo wanatumia huduma hizo

Mbugua.jpg

Caroline Mbugua

Amesema utafiti wa GSMA umeonyesha vikwazo vitano vinavyowafanya watu wasiunganishwe na huduma za intanenti ni pamoja na; gharama za huduma, kukosa elimu kuhusu umuhimu wa huduma za kidijitali. Sababu nyingine ni kutoamini huduma hizo, namna ya kuzifikia huduma hizo ikiwemo upatikanaji wa vitambulisho vya taifa.

Pia amesema unafuu wa data sio kiwango cha fedha, bali ni bei za bidhaa na uwiano wake na Kipato (Disposable income)

Philip Besiimire, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania
Amesema ili mabadiliko ya kidijitali yafanikiwe Serikali na sekta binafsi huduma zake zitolewe mtandaoni katika hatua zote.

“Tunahitaji pia kuweka huduma nyingi zitolewe kwa njia ya kidijitali, mfano sasa hivi mtu akihitaji passport anaanza mchakato kidijitali lakini bado atakalazimika kufanya hatua zingine kwa njia za kizamani sasa kama tunataka kufanikiwa katika uchumi wa kidijitali ni muhimu huduma kama hizi zipatikane kwa njia ya mtandao,”

Mafutah Bunini, Mkurugenzi wa Utafiti na Teknolojia ya Habari (TIC)
Amesema wanafanya utafiti kuijua miradi ambayo inaweza kufanyiwa uwekezaji kwenye Tehama kwa lengo la kuhamasisha wawekezaji kuingia kuwekeza kwenye eneo hilo

Bunini.jpg

Mafutah Bunini

“Tunahamasisha wawekezaji kukitumia kituo na ahadi yetu ni kuboresha huduma ili ziendane na maendeleo ya teknolojia,”

Joseph Lyimo, Mtaalam wa Kodi PWC
Amesema kupunguzwa kwa asilimia 50 ya tozo ya miamala ya simu kumekuwa na matokeo makubwa kwenye uchumi

“Hii imeongeza idadi ya miamala. Nafikiri Serikali imejifunza, ndiyo sababu inafikiria kuiondoa ili kuleta matokeo makubwa Zaidi.”

Justina Mashiba, Mtendaji Mkuu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)
Amesema fedha wanazokusanya ndizo zinarudishwa kwa watoa huduma ili wafikishe huduma za mawasiliano maeneo ya pembezoni.

UCSAF.jpg

Justina Mashiba

“Hatuwezi kupata kodi za kutosha kama kuna watu tunawaacha nyuma katika matimizi ya mtandao. Lengo letu ni kuhakikisha kila mtu anaunganishwa na huduma za mtandao bila kujali yuko katika eneo gani la kijiografia.”

Philip Besiimire, Mkurugenzi Mkuu Vodacom
Amesema ili kuwapata Watanzania ‘online’ ni lazima wawe na simu tena simu janja ameiomba Serikali kuangalia namna ya kuondoa vikwazo ikiwemo gharama za simu.

Voda 1.PNG

“Kwa sasa wapo wanaoshindwa kununua simu janja na kuishia kwenye vitochi. Kampuni za simu zimeanza kuchukua hatua zinakopesha simu. Ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi katika kuwekeza katika eneo hili ikiwezekana kiwepo kiwanda cha kuzalisha simu janja."

"Usalama wa mtandao ni jambo linalopaswa kuangaliwa hasa katika ulimwengu huu wa kidijitali kwani kuna watu wanafanya uhalifu eneo hilo"

"Kuwezesha na kuchochea maendeleo ya teknolojia na bunifu ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi unapaswa kupewa kipaumbele"
 
Back
Top Bottom