Konda Nae Kaoteshwa na Mungu -Mbagala

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MKAZI wa Mbagala jijini Dar es Salaam, ameibuka na kusema kuwa ameoteshwa na Mungu kutoa dawa kwa njia ya kikombe kutibia wagonjwa wenye maradhi sugu.
Dawa hiyo amedai Mungu amemuotesha kutoa dawa ambayo ni maji ya kisima, bomba na haichanganywi na chochote zaidi ya maji hayo.

Awali kijana huyo aliyekuwa akiabudu dini ya Ukristo na baadae kubadili dini na kuwa Muislam na ndipo ameoteshwa.

Awali imedaiwa kijana huyo alikuwa akifanya kazi ya ukonda katika daladala na hivi karibuni ameibuka na kudai kuwa ameoteshwa.

Kufuatia taarifa hiyo watu wameanza kujitokeza nyumbani kwa kijana huyo kupata kikombe cha dawa hiyo huku akiwa ameshika msaahafu mkononi.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi Temeke, wanafanya jitihada za kufanya mahojiano maalum na kijana huyo na taarifa itatolewa kwenye vyombo vya habari.

Kijana huyu ni wa saba kujitokeza na kudai wameoteshwa na Mungu na wengine wamejitokeza katika mkoa wa Mbeya, Moshi, Mbeya, Iringa, Tabora na Morogoro, Pwani wote wakidai kuoteshwa na Mungu kutoa tiba kwa njia ya kikombe.
5628798.jpg
 
wataoteshwa mpaka vikombe vya mavi hakya nani nawaambia kuweni makini mtapotea mungu alshasema mwisho wa dunia watakuja wav watumiao jna langu hovyo.so take care mtapotea
 
mbona hata mm nimeoteshwa, maji unayochambia ukitoka chooni ni dawa ila nna wasiwasi kwa sababu ndoto imesema lita nzima ndo dozi.
 
Tanzania ibadilishwe na kuitwa ima Bongolalaland au Vikombe. Maana watu wetu ni wagonjwa wa akili hakuna mfano. Si watawala wala watawaliwa wote ni majnuni. Tazama tunavyoibiwa mabilioni na wachukuaji tuwaitao wawekezaji kila uchao. Hiyo ni dhambi ya watawala. Wananchi nao kwa ujuha wao wananyweshwa kila takataka! Kama alivyosema mmoja wa wachangiaji hapo juu, mtakujalishwa mavi kwa imani hizi za kibajaj.
 
ulitegemea nini maana viongozi wenyewe ndio wa kwanza kwenda kugonga vikombe!
Tanzania ibadilishwe na kuitwa ima Bongolalaland au Vikombe. Maana watu wetu ni wagonjwa wa akili hakuna mfano. Si watawala wala watawaliwa wote ni majnuni. Tazama tunavyoibiwa mabilioni na wachukuaji tuwaitao wawekezaji kila uchao. Hiyo ni dhambi ya watawala. Wananchi nao kwa ujuha wao wananyweshwa kila takataka! Kama alivyosema mmoja wa wachangiaji hapo juu, mtakujalishwa mavi kwa imani hizi za kibajaj.
 
Awali kijana huyo aliyekuwa akiabudu dini ya Ukristo na baadae kubadili dini na kuwa Muislam na ndipo ameoteshwa.

Hapa kuna shida kubwa!
 
Kaazi kweli kweli nchi inapotea sasa jamani....Watanzania kuweni macho, mi naona ni njia tu ya kujipatia VIJISENTI.
 
Babu wa Loliondo na wengine wote wanaodai kuoteshwa ili kugawa vikombe ni kazi za shetani zile zile zilizotabiriwa katika 1Tim.4:1. Watanzania tumtafuteni Mungu wa kweli na sio kukimbilia vitu rahisi rahisi namna hii
 
Yale waliyoyaigiza futuhi na mizengwe juu ya kuoteshwa kutoa tiba ya kikombe yana ukweli 100% kuna watu wanadai kuoteshwa baada ya kupigika na maisha hivyo wanatafuta mahali pa kutokea.
 
Back
Top Bottom