Kombe la Shirikisho walisema timu ni chovu vipi nako huku?

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Watanzania hasa mashabiki wa mpira tunajificha kwenye kivuli cha utani wa jadi ila uhalisia watanzania tuna roho mbaya, wivu, kijicho, mtimanyongo, unafiki, majungu...nk

Full time Yanga 4 Waalgeria 0

Nakumbuka Yanga inacheza fainali za kombe la shirikisho na kupoteza kwa faida ya magoli ya nyumbani kiliibuka kikundi cha wachambuzi uchwara na mashabiki feki wa upande ulee.

Walikuja na hoja dhaifu timu za shirikisho ni dhaifu ila wakati Simba wanachoma kiwanja cha watu kule South Afrika kwa imani cha kichawi ila wapate penalti hizo propaganda hazikuwepo hapa utajua wanafiki wengi wapo upande gani hasa hawa wachambuzi.

Leo Yanga kamla mtu bakora nne kesho sijui watakuja na propaganda gani nakumbuka kuna mchambuzi mmoja gemu ya Yanga na Rivers Utd alipiga mpaka picha na kuwatumia Caf kwamba Yanga wamewafanyia figisu Rivers utd hiyo ni mtanzania kabisa.

Kwa dizaini hii lazima kesho waje na vipropaganda uchwara vyao kubeza kwa makusudi nguvu, jitihada, bidii za viongozi wa Yanga pamoja na wachezaji uzuri viongozi wa Yanga wameamua kuwa serious kwa kuweka pamba masikioni na kuacha kusikiliza uchuro wao.

Je kama shirikisho lilikua na timu dhaifu na vipi huku kwa mabingwa semeni mapema kabisa wachambuzi uchuro.
 
B… kwa leo huna baya kusema za ukweli, ila historia inakukumbuka kama uliyetuponda sana shirikisho.

Haya, huku tena unasemaje?
Mdakuzi
 
Back
Top Bottom