Mkuu EMT kuna kitu kimechanganywa kama sio english yangu ndo ipo shallow, ebu angalia tittle ya barua (reference) then soma kwa umakini sentensi ya kwanza alafu usome sentensi ya pili hapo hapo kwenye aya ya kwanza.
Halafu naomba nikupe hii mifano miwili ya transactions then nambie wapi panapaswa kukatwa kodi.
A, Mimi naitaji kununua gari nje ya nchi nitalipa kwa TT.
B, Mimi nina account ACCES BANK ninahitaji kuhamisha hela kwenye account yangu nyingine iliyopo EXIM BANK.
Kati ya A na B wapi napaswa kulipa kodi,?
Sema wewe mkuu, manake mimi nasoma hii barua mara mbili mbili nashindwa kuelewa niwalaumu TRA au mwalimu wangu wa kizungu. Kwa kutoelewa kwangu, naona kama scenario A ndio itahusika na hilo tozo. Na nilivyoelewa mimi, anayelipwa ndio atapelekewa kiasi pungufu kwa hiyo asilimia 0.15 (kuwa atakuwa amekuwa taxed at source). Lakini najikuta sielewi tena kama mtumaji bado anakatwa tena? If yes, kwa ajili ya nini? Na je, kama anayelipwa ni wa hapa hapa nchini, jamani, haya siyo ma-double taxation tena? Assuming kama ni consultant, si aliyemlipa alisha withhold tax at some point tena?
Mmh ndugu, nisikuchanganye, manake nahisi sijaelewa kitu.....au sijui ndio nashindwa ku-absorb shock?