Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 20,921
- 45,599
Zama huja na kuondoka. Lakini legacy hubaki. Hapa kuna makocha wanne tofauti ambao kwa nyakati tofauti waliongoza vilabu vyao kutwaa mataji kadhaa ya EPL. Kila kocha alikuwa na rekodi zake pamoja na mbinu zake. Ni yupi unamkubali zaidi?
1. Sir Alex Ferguson - Man Utd
Huyu ametwaa mataji 13 ya EPL akiwa Man Utd. Aliifanya Man Utd itambe na kuogopwa sana EPL. Alitwaa mataji matatu mfululizo ya EPL mara mbili tofauti. Tangu kuondoka kwake Man Utd inalegalega.
2. Arsene Wenger - Arsenal
Wenyewe the gunners walipenda kumuita “Profesa” alileta mapinduzi makubwa ya namna ya uchezaji katika EPL. Nani asiyejua jinsi alivoitengeneza Arsenal na kuwa mwiba mkali Highbury usingeweza kutoka salama. Mpaka anasatafu alitwaa mataji mawili tu ya EPL
3. Jose Mourinho - Chelsea
Kipindi chake cha kwanza pale Chelsea mwaka 2004-2007 Jose alikuwa kocha mwenye rekodi lukuki.
Msimu wa 2005 aliweka rekodi ambayo mpaka leo haijavunjwa. Clean sheet 24 za EPL katika mechi 38 sio mchezo huku Chelsea ikiruhusu magoli 15 tu katika mechi 38. Chelsea ilikuwa haishikiki. Alitwaa mataji mawili mfululizo.
4. Pep Guardiola ( Man City )
Master Pep mpaka sasa ana mataji matano ya EPL. Kwasasa ndio ameishika EPL. Ameweka rekodi ya kufika point 100 kwa msimu katika EPL. Anacheza soka la kisasa mno. Huku akileta mbinu zake ambazo zamani hazikuwahi kuwa applicable na makocha wenzake.
Nani angeweza kuleta kipa ambaye anatakiwa kuwa na footwork nzuri kuliko kudaka, nani angeweza kumfanya full back aingie ndani kucheza kama kiungo, nani angeweza kuchukua taji la EPL bila ya kuwa na natural striker namba 9
Hayo yote Guardiola kayaweza kufanya na kafanikiwa.
Kocha yupi unamkubali zaidii?