regnaldshirima
Senior Member
- Aug 18, 2014
- 124
- 78
Mimi nilipenda Ukuti ukuti wa mnazi wa mwisho akamatwe atiwe gerezaaaaaaani....
we ulipenda mchezo gani zaidi
haaaaaaNILIKUWA NAPENDA SANA KOMBOLELA HASA LILE LA USIKU
ivi sai uka kutana na miongoni mwao umuulize kwanini alikua hataki kufa kipindikile unadhani itakujibu vipi?Kucheza kibunduki bunduki.yaani mnaviziana kama magaidi vile ukimkuta mwenzio kazubaa basi unasema "puu puu puu" kisha anaanguka chini na kufa mnaendelea hivyo hivyo hadi timu moja ishinde.ila kuna mijitu inakera yaani unaliuwa alafu halitaki kufa utaskia mi ndo nilikuwahi.
#I miss the life
Kombolela na kibaba /mama
Mimi nilipenda Ukuti ukuti wa mnazi wa mwisho akamatwe atiwe gerezaaaaaaani....
we ulipenda mchezo gani zaidi
Sasa mie nilikuwa napenda ile ya mfuniko wa ndoo unautoboa kati halafu unakuwa unauendesha na fimbo.achana na iyo moment apo nimetumwa dukani katika ubora wangu nko na vx rod
Mchezo wangu wa hatari ni kucheza kidali juu ya mti,tena kulikuwa na miti miwili mikubwa ukikimbizwa mti mmoja unahamia mwengine.Nakumbuka mtaan kwetu kila mchezo una msimu wake na kwa kwel karibia michezo yote niliipenda mfano kampuska,gololi,kutengenez vtu kwa udongo wa mfinyanz...ila kuna mchezo mwingine ulikuwa wa kikatili sana tulikuwa tuna daka vyura kisha tuna wapasua na viwembe tukijifanya n madaktar kwa kwel tuliua vyura wengi sana