Kitendo cha "jinamizi mimba za watoto wa shule" kushika kasi kinatufunza kuwa, viongozi tusiongee kila jambo hadharani

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,881
Wanafunzi wa kike wakishapata mimba walikuwa wanakabiliwa sana na mazingira magumu ya kurudi shule tangia enzi za Kikwete. Na katika kipindi chote hicho hakukuwa na tatizo.

Shida ni maneno ya kejeli yaliyotolewa na viongozi wa awamu ya tano juu ya jambo hili. Maneno ambayo hayapaswi kamwe kuzungumzwa hadharani na kiongozi wa umma.

Niitahadharishe tu serikali kuwa kitendo cha baadhi tena wengi wao kusema sema hovyo hadharani kunafanya kuzushwa mijadala ambayo madhara yake ndiyo kama hayo ya world bank! Alikuja Makonda akasema sema hovyo hapa na hatimaye amezuiwa kuingia baadhi ya mataifa ya magharibi.

Kila akienda kuomba viza anatolewa nje! Kusema sema hovyo kunabadili kabisa mtizamo wa jambo. Kwani Mzee Kikwete alikuwa hapingi ushoga? Mbona ma RC wake hawakuwa na vihere here vya kusema hovyo? Mbona mambo yalienda vizuri tu?

Unakuta Waziri wa Mambo ya Nje ni msema hovyo wa hali ya juu, sasa unajiuliza huko nje anawakilisha aina gani ya watu?
 
Back
Top Bottom