Kitabu cha Kina cha Haki

gxrenny

New Member
Apr 17, 2010
3
0
Jamani nimeandika kitabu cha simulizi ya riwaya kiitwacho KINA CHA HAKI "Shinikizo" lakini nimeshindwa kupata namna ya kukifikisha kwa hadhira husika. Nikiwa na maana kuwa bado hakijachapwa lakini uandishi wake umekamilika kwa asilimia 100. Kinachonikwamisha hapa ni mtaji kwa maana ya gharama za uchapaji wake pamoja na maswala mengine.

Kwa kifupi kitabu hii kinahusu maisha ya kipelelezi ya kachero Bruno ambaye anajitolea kwa moyo wake wote kupingana na matendo ya kidhalimu yanayolikabili taifa hilo husika kama vile rushwa, madawa ya kulevya, utekeaji, blackmailing, na mengine mengi.

Riwaya nzuri na tamu sana, ijapokuwa wanasema mwamba ngoma,......... lakini hapa ni suala tofauti kidogo. Kwale ambao wamewahi kuzisoma riwaya za WILLY GAMBA, basi hapa kiu na hamasa ya hizo riwaya ambazo tumezimisi kitambo, imepata majibu. kwani kupitia riwaya hii, utamaduni wa kupenda kusoma vitabu unaweza ukarejea.

kwahiyo kwa yeyote atakaye niwesha kufahamu nini cha kufanya kuhusiana na kukizindua kitabu hicho nitashukuru sana.

ikumbukwe kwamba, kitambu hiki kitakuja na miendelezo mitano, yaani
KINA CHA HAKI shinikizo
KINA CHA HAKI shabaha
KINA CHA HAKI mageuzi
KINA CHA HAKI hatamu
KINA CHA HAKI ukomo

email:benardigeofrey@gmail.com
 
Mimi ni mtunzi wa kitabu kinachoitwa Mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri. Nimechapisha kitabu changu mwaka 2008 kidogo kidogo nakala 1,000 kila mara hadi kufikia nakala 4,000 na nimefanikiwa kuuza vitabu 3,000 mpaka sasa na kitabu changu kinafanya vizuri sokoni. Naomba nikupe ushauri wangu kama kwa kutumia uzoefu nilioupata kama ifuatavyo; Kawaida huko Ulaya na nchi zingine zilizoendelea mfumo wa biashara ya vitabu uko hivi; kuna Mtunzi, Mchapishaji na Msambazaji (Publisher) Kazi ya Mtunzi ni kutunga kitabu akishamaliza kuandaa mswada manuscript kama ulivyofanya wewe anapeleka mswada wake kwa Publisher ambaye ataupitia akiridhika anaingia mkataba na mtunzi. Publisher atakipeleka kitabu kwa mchapishaji na kukichapisha kitabu kwa gharama zake, atasambaza, kutangaza na kuuza vitabu kisha atakupa mrabaha Royalties kwa kupiga asilimia ya faida ya kila kitabu baada ya kutoa gharama zake inaweza kuw 50% 60% au 80%. Kwa hapa Bongo hali siyo hivyo hakuna mfumo rasmi wa kulinda haki za waandishi ukikipeleka kitabu chako kwa Publisher utakuwa unafanya hivyo at your own risk. Publisher wetu siyo waaminifu ukimkabidhi kitabu chako ujue kimekuwa chake akiuza vitabu 10,000 atasema kauza vitabu 2,000 hata hivyo vitabu kulipwa ni kwa mbinde. Ushauri wangu tafuta pesa kwa nguvu yako yote kama ni kukopa fanya hivyo nenda Business Printers ni waaminufu usichapishe kitabu chako uchochoroni utaibiwa. Kwa kuanzia unaweza kuchapisha vitabu 1,000 na usiwe na chini ya Sh. 1,000,000.00 kwa sababu sijui ukubwa wa kitabu chako siwezi kusema utalipa kiasi gani ila huwa wanakupa quotation unalipa nusu kabla ya kuchapisha ukienda kuchukua vitabu vyako utamalizia. Nenda kasajili manuscript yako COSOTA usije kuibiwa kazi yako ni gharama kidogo sana mimi nililipa Sh. 15,000.00 kusajili kitabu changu. Gharama zingine wakati wa kuchapa kitabu chako ni Typesetting, Cover design na film. Mengine kuhusu namna ya kukiingiza sokoni tutashauriana nitafute. Kwa maelezo zaidi nipigie simu 0755394701.
 
Wapelekee wachapaji wakiona kinaweza kulipa lazima watakichapa wenyewe na kukiuza kisha mkubaliane malipo kwako!
 
babalao kasema kweli mzee...je babalao unasemaje kuhusu FILM au kuuza screenplay yangu inauzika bongo?na how is it?
 
Magulumangu Naomba tuwasiline ili nikushauri nipigie simu namba 0755394701
 
Another suggestion:
Option #1
Aanze kwanza na wateja kichwani. So he design his imagination and creativity around satisfying a customer. That is not going to be his book, it a for others. It is therefore, let the publisher help him how to better served his customers. What most us can do is to help him in the area of copyrights, financial planning for the investment at hand and his own financial planning, what is he gonna do with the money? and what is really important to him, what is his dream.

Publishing is easy, Google independent publishers. I hope you be seccessful
 
Jamani nimeandika kitabu cha simulizi ya riwaya kiitwacho KINA CHA HAKI "Shinikizo" lakini nimeshindwa kupata namna ya kukifikisha kwa hadhira husika. Nikiwa na maana kuwa bado hakijachapwa lakini uandishi wake umekamilika kwa asilimia 100. Kinachonikwamisha hapa ni mtaji kwa maana ya gharama za uchapaji wake pamoja na maswala mengine.

Kwa kifupi kitabu hii kinahusu maisha ya kipelelezi ya kachero Bruno ambaye anajitolea kwa moyo wake wote kupingana na matendo ya kidhalimu yanayolikabili taifa hilo husika kama vile rushwa, madawa ya kulevya, utekeaji, blackmailing, na mengine mengi.

Riwaya nzuri na tamu sana, ijapokuwa wanasema mwamba ngoma,......... lakini hapa ni suala tofauti kidogo. Kwale ambao wamewahi kuzisoma riwaya za WILLY GAMBA, basi hapa kiu na hamasa ya hizo riwaya ambazo tumezimisi kitambo, imepata majibu. kwani kupitia riwaya hii, utamaduni wa kupenda kusoma vitabu unaweza ukarejea.

kwahiyo kwa yeyote atakaye niwesha kufahamu nini cha kufanya kuhusiana na kukizindua kitabu hicho nitashukuru sana.

ikumbukwe kwamba, kitambu hiki kitakuja na miendelezo mitano, yaani
KINA CHA HAKI shinikizo
KINA CHA HAKI shabaha
KINA CHA HAKI mageuzi
KINA CHA HAKI hatamu
KINA CHA HAKI ukomo

email:benardigeofrey@gmail.com

tunaomba feedback ndugu yetu.. ulifanikiwa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom