Kiswahili lugha ya Taifa.

Dan84

Member
Apr 3, 2012
49
24
Imekuwa ikinisikitisha, mara nyingi, kila nisomapo mada mbalimbali hapa, JF. Kuhusiana na matumizi mabovu ya lugha ya kiswahili, neno kama UDHIBITISHO, inaandikwa USIBITISHO, neno NAAMINI, inaandikwa NAMINI, neno LUGHA, inaandikwa LUGA, ah! Inasikitisha. Hivi somo la fasihi na dhima za lugha siku hizi hakuna?
 
"Udhibitisho" maana yake nini?
 
Spelling Error, Kama ilivyotokea kwako kwenye neno UDHIBITISHO badala ya UTHIBITISHO huenda ndio na wenzako huwatokea hivyo hivyo. Pole, hilo neno limekuharibia hoja yako..!
 
Sio spelling error tu bali ni mazoea, unajua lugha wakati mwingine inawafanya watu wazoee kutumia maneno flani ambayo si sahihi na kuyafanya yaonekane kama sahihi mfano HICHI badala HIKI, ANANIAMBIAGA badala ya ANANIAMBIA, nadhani mleta uzi nae amejifunza PRACTICALLY kwamba hawafanyi makusudi bali ni mazoea lakini pia kuna ambao hajui kuandika vizuri
 
Imekuwa ikinisikitisha, mara nyingi, kila nisomapo mada mbalimbali hapa, JF. Kuhusiana na matumizi mabovu ya lugha ya kiswahili, neno kama UDHIBITISHO, inaandikwa USIBITISHO, neno NAAMINI, inaandikwa NAMINI, neno LUGHA, inaandikwa LUGA, ah! Inasikitisha. Hivi somo la fasihi na dhima za lugha siku hizi hakuna?

Tafakari sababu za wewe kuandika UDHIBITISHO badala ya UTHIBITISHO ndipo uanze kusikitikia wenzako, kama hujafanya makusudi basi ujue na wenzako ni bahati mbaya kutokana na mazoea.
 
Wadau, nimekubali na kutambua kwamba mazoea na mazingira tunayoishi yanatuathiri kwa kiasi kikubwa, lakini si vibaya kuendelea kufahamishana matumizi sahihi ya lugha yetu pendwa.
 
Ametoa kauli THABITI, THIBITISHA kauli yako, DHIBITI rushwa. Kiswahili hicho!

Daaah...!Kweli kiswahili kigumu kwa hiyo maana ya THIBITISHA-Hakikisha,Ondoa shaka,Aminisha na neno DHIBITI-Zuia,kutoruhusu....Tujivunie lugha yetu jamani
 
Back
Top Bottom