Kisa Cha mwanamuziki Pauline Zongo aliyewahi kutamba na kibao Cha Mateso Ya Ndoa wengine hukiita Ndoa ya Mateso

Jan 19, 2020
29
38
KISA CHA PAULINE ZONGO
Kutoka kwa Mdau wa Jamii Forum;

Pauline Zongo alitamba mwanzoni mwa miaka ya 2000 akiwa na kundi la muziki wa kizazi kipya la East Coast lililowajumisha wasanii mahiri kama King Crazy GK, MwanaFA, AY na wengine wakiwa na vibao kama nitakufaje na sister sister.

Pauline Zongo afya yake imetetereka na maisha yake yamepoteza muelekeo kama alivyoeleza mwenyewe kwenye mahojiano na mwandishi Richard Bukosi.

1774E86D-63A9-4B20-A2AF-9C4267D59076.jpeg

Pauline Zongo

Pauline Zongo: Baada ya kundi letu kusambaratika 2006, East Coast team nilijiunga na TOT. Mwaka mmoja kabla tulienda kupiga kampeni ya kwanza na Kikwete, 2010 Kikwete na 2015 na marehemu Rais Magufuli.

Baada ya hapo nikaja kupata ajali mbaya sana ya gari na nilikuwa naendesha mimi mwenyewe, niliyempakia kwenye gari alifariki palepale, kilichoniokoa mimi ni belt na Mwenyezi Mungu.

Nikavunjika miguu na meno, navaa sasa hivi meno na kuvua. Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu aliweza kuniweka japokuwa nimekaa muda mrefu bila kutembea, muda si mrefu nikakaa, nimekaa sitaki kukumbuka yale kwasababu nikayazungumzia mpaka nalia.

Isitoshe ukiangalia wewe ni single mother, una watoto wawili so mtihani flani ambao umekaa. Nilipo hapa miezi mitatu haijaisha nimetoka kufanyiwa opereshen lakini Mungu bado ananiweka ina maana ana makusudi yake

Mwandishi: Ilikuwa shida Nini?

Pauline Zongo: Nimefanyiwa opereshen nilikuwa na uvimbe tumboni, kuna baadhi ya vioo vilikaa kwa kipindi kile kumbe vilikaa, vilipasuka pasuka na vikaanza kunikata utumbo ndani kwa ndani

Mwandishi: Unaendeleaje kwa sasa?

Pauline Zongo: Bado siko sawa ingawaje nimejikongoja narekodi album yangu mpya kidogo kidogo lakini siwezi kuperform sasa hivi kwenda stejini abda kwa kuibia ibia ujaribu, unapokuwa stejini unatumia nguvu ya kuimba na kucheza.

Mtangazaji: Zimewahi kuibuka tetesi umepotea kwenye matumizi ya madawa ya kulevya!

Pauline Zongo: Mungu angekuwa binadamu, angekuja akashuka hapa akaongea, unajua kwa mfano ukasingiziwa kitu ambacho hujakifanya, inaumiza sana. Situmii Bangi, madawa ya kulevya. Pombe huwa nagusa nisiwe muongo.

Inauma sana , kwa sababu mtu anaongea kitu kama hicho. Twende tukapime si kuna maabara! Tukimaliza mtanlipa? Unanichafua. Hivyo vitu sivitumii, siwezi kumuogopa binadamu hata wakiongea si poa tu, Mungu nimemshirikisha.

Kilio cha kutelekezwa na watoto
Pauline Zongo:
Mtoto wangu wa kwanza nadhani baba yake mnamjua ambae ananisumbua kwenye matumizi ya mtoto. Mtunis Mohammed Yusuph, aliniachia yule mtoto akiwa na miaka miwili, sasa hivi ana 13 kuelekea 14, nipo nae mimi na sipati matumizi yoyote.
5FC660E2-4F94-4A2A-987D-AB5C9AD27742.jpeg

Mtunis (Nice Mohamed) mzazi mwenzake

Mtoto wangu wa pili nilizaa na mtu mwingine ambae alikuwa anamuendeleza tukapishana dini, yeye ni muislamu mimi ni mkristo lakini yupo na baba yake, baba yake alimchukua, ana miaka nane sasa. Baba yake siwezi kumtaja, amemchukua mtoto wake anaishi naye. Kwa hiyo nipo na huyu wa Mtunis.

Mtangazaji: Kipato cha pesa sasa hivi unapata wapi ukiwa katka hali kama hiyo?

Pauline Zongo: Mungu ndio anajua.
 
Ingawa alikanusha kuwa teja lakini mficha maradhi mauti umuumbuwa, kuna video yake nimeiona leo anasikitisha unga ni noma aisee, bora hao wanaosifia bia tamu ni heri watu wanywe bia unga umemzeesha huyu dada kawa kama kibibi na virasta vyake visivyo na afya.
 
Pole sana Mungu ni mwe mwemaa

Kwa jina hili huku Kinshasa..
Mama Pauline Nzongo ...mgahawa mkubwa Paris hapo unakula nzombo na matembele Ugali sado hataree
 
Unga mbaya sana maji yakishamwagika hayazoleki maisha umeyachezea sasa unajuta sister sister,pouline anajua kuimba kupiga gitaa ,kinanda ila amekisa kujitambua,ulivyotoka TOT caotsin komba alikubembeleza urudi unga ukakuzidi nguvu
 
Ina maana Unga alianza kabla hata Komba hajafa.?
 
Ingawa alikanusha kuwa teja lakini mficha maradhi mauti umuumbuwa, kuna video yake nimeiona leo anasikitisha unga ni noma aisee, bora hao wanaosifia bia tamu ni heri watu wanywe bia unga umemzeesha huyu dada kawa kama kibibi na virasta vyake visivyo na afya.

Hata mimi nadhani anatumia unga huyo
 
Ingawa alikanusha kuwa teja lakini mficha maradhi mauti umuumbuwa, kuna video yake nimeiona leo anasikitisha unga ni noma aisee, bora hao wanaosifia bia tamu ni heri watu wanywe bia unga umemzeesha huyu dada kawa kama kibibi na virasta vyake visivyo na afya.
Tuwekee hiyo video
 
Back
Top Bottom