TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 5,720
- 10,218
Mwite Juma Thomas Zangira, Komando mpelelezi wa kwanza Tanzania aliyekamatwa baada ya kuwa anavujisha siri za nchi. Alikamatwa mwaka 1977 akiwa ndio amekwenda Posta kupokea barua yake ya mwisho ambayo ilikuwa imebeba maelekezo mengi na mipango ya kijasusi.
Aliyemkamata ni Afisa wa Polisi, Bwana Abdallah Mssika. Kabla ya kumkamata Jasusi huyu pia alipewa mafunzo ya namna gani ya kujihami kwa lolote lile ambalo lingetokea mbele yake,katika interview yake Mssika anaeleza alipewa somo la kumsoma kwanza yeye alivyo,namna gani anaweza kutumia miguu yake au mikono yake kwa kujihami. Hasa akaaelezwa anatumia sana mkono wa kushoto, hivyo akafunzwa kwanza namna ya mkao atakapokuwa nyuma yake,awe mwepesi kujihami. Mzee Mssika hata kuhusu mlo wa chakula chake ulibadilishwa ili tu kumjenga kufocus kwenye mission hiyo ya kumkamata Komando Zangira.
Kazi ya kumfuatilia ilichukua muda mrefu takribani miaka 6, Bwana Zangira hakuwa anajua kama anafuatiliwa. Kila barua aliyokwenda kupokea ilikuwa tayari wameshaipata kisha kuitoa copy,hata fedha alizokuwa anatumiwa walizibaini ni kiasi gani. Barua zote alizokuwa akitumiwa zilitoka South Africa, ila hapo kabla walijua zinatoka London. Kumbe London zilipitia tu ili isijulikane ni wapi zinatoka,ilikuja kufahamika baada ya kukamatwa Bwana Zangira.
Baada ya Serikali kujiridhisha kuwa ni kweli Jasusi Zangira anafanya usaliti, basi oda ikatolewa akamatwe! Ndipo Afisa huyo wa Polisi,Bwana Abdallah Mssika alipoenda yeye na wenzake wakiwa wanamfuata nyuma. Komando Zangira alipofika Posta akafungua sanduku la barua,alipoitoa tu tayari aliamuliwa anyoshe mikono juu,haraka sana magari yaliyokuwa yameandaliwa kwaajili ya ulinzi yalifika.
Komando Zangira alinyang'anywa ile barua na haraka sana akaweka ndani ya gari. Kabla ya kupandishwa ndani ya gari walifanyiwa searching na hukutwa na silaha,pia alifanyiwa searching kwenye mdomo maana Jasusi akiwa kwenye mission za kusaliti mara nyingi huwa anachukua tahadhari hata atakapokamatwa aweze kujihami au hata kujidhuru. Anaweza kuwa na kitu chochote mdomoni, akifanikisha kunga'ata tu au kukikandamiza basi habari inakuwa imekwisha hapo hapo.
Hivyo basi Jasusi Zangira alikamatwa akiwa salama na kufikishwa sehemu husika,baadae alihukumiwa kifungo cha maisha jela.