Kipi kimetokea umejikuta hauna rafiki hata mmoja?

Utawala2025

JF-Expert Member
Oct 20, 2023
329
1,058
Habari za mchana.

Maisha yana mapito mengi sana kama tukisema kila mtu aanze kusimulia alikopita nadhani kama tukiwa kwa gari la chanika tunaweza kufika bunju tukiwa hatujamaliza kusimuliana.

Imekuaje kwenye maisha umepoteza watu wako wa karibu sana. Ulikuwa na marafiki wa shule ya msingi, sekondari na chuo.

Ukabahatika kufanya kazi sehemu mbalimbali. Ila kwa sasa umejikuta Hauna rafiki hata mmoja tu.

Kwenye contact ya watu 500 hauna hata mmoja unaeweza kumpigia simu na kumueleza kumuomba hata laki moja.

Leo hii watoto wameenda shule,umejenga nyumba umenunua gari. Umepata mke mzuri.

Ila una inakuja kutambua hauna tena mtu hata mmoja wa maana katika circle yako.

Kwanini hauna rafiki hata mmoja maishani?
 
Marafiki na ndugu ni watu wanafiki sana wenye roho chafu ambao wanakuchekea usoni lakini wanatamani kukuona unaangamia. Hasa hasa ndugu, ni wabaya sana.

Tangu nilipolijua hili nimeweka ukuta wa chuma, sitaki pua ya mtu inisogelee vinginevyo nakata panga pua inaangukia kule.

Tena wengine wanakuroga kabisa wanakutumia na mapepo kwa namna ya kichawi, wanajifanya wanacheka kumbe ni maadui namba moko.

Ukiishi mwenyewe kuna raha ya ajabu, hakuna mambo ya uchawi na maroho machafu.

FYEKELEA MBALI. Hakuna cha classmate wala bibi ake na classmate.
 
🤔🤔🤔🤔🤔+😚😚😚=😠😠
Maisha ni wewe mwenyewe,hao wengine ni wakukusindikiza kufika utakapo.
Wanakuja na kupotea katika mazingira ya kutatanisha.
Rafiki anamzidi ndugu,ndugu anamzidi rafiki,rafiki anakuwa adui,pia adui anakuwa rafiki,vile vile ndugu anakuwa snichi+adui mtu from nowhere anakuwa msaada kwako gafla binivuu!.
So,umdhaniaye ndie,unakuta sie.Na unaedhani sie Kumbe ndiye.
All in all,ishi Kama KINYONGA.
 
Marafiki na ndugu ni watu wanafiki sana wenye roho chafu ambao wanakuchekea usoni lakini wanatamani kukuona unaangamia. Hasa hasa ndugu, ni wabaya sana.

Tangu nilipolijua hili nimeweka ukuta wa chuma, sitaki pua ya mtu inisogelee vinginevyo nakata panga pua inaangukia kule.

Tena wengine wanakuroga kabisa wanakutumia na mapepo kwa namna ya kichawi, wanajifanya wanacheka kumbe ni maadui namba moko.

Ukiishi mwenyewe kuna raha ya ajabu, hakuna mambo ya uchawi na maroho machafu.

FYEKELEA MBALI. Hakuna cha classmate wala bibi ake na classmate.
Am too young to understand this.

Kwa upande wangu sio mtu wa kua na marafiki wengi, Hususani kama hatuna kitu kinachotuunganisha.

Katika pita pita zangu, Nimebahatika kubaki na rafiki mmoja wa Sekondari, Rafiki mmoja wa Advance, na Rafiki wa wili wa chuo kikuu.

Hao atleast naweza nikaongea nao my personal issues.

Upande wa ndugu. Sijui sana. Ila niko na kaka wa2 ninao wapenda sana. Hua tunatofautiana mambo mengi lakini siwezi kuwatoa kwenye circle yangu tunasaidiana pale inapowezekana.
 
Mi ndugu zng hata hawajui npo wp na ninafanya nn na nina maisha gani hawawajui hata watoto wng. Niliamua hvyo baada kugundua hao ndo adui zangu namba 1 na wapo kmaslahi tu. Ajabu huwa napata taarifa wapo wanaonisema kwa mabaya pamoja na kujtenga huku. Walinigombanisha na baba yng wakshrikiana na mama wa kambo. Khs marafk huwa stabiliki kbs nina rafk 1 tu tumeshbana nlisoma nae advance mpk chuo bt npo nae kwa tahadhari sn sn.
 
Habari za mchana.

Maisha yana mapito mengi sana kama tukisema kila mtu aanze kusimulia alikopita nadhani kama tukiwa kwa gari la chanika tunaweza kufika bunju tukiwa hatujamaliza kusimuliana.

Imekuaje kwenye maisha umepoteza watu wako wa karibu sana. Ulikuwa na marafiki wa shule ya msingi, sekondari na chuo.

Ukabahatika kufanya kazi sehemu mbalimbali. Ila kwa sasa umejikuta Hauna rafiki hata mmoja tu.

Kwenye contact ya watu 500 hauna hata mmoja unaeweza kumpigia simu na kumueleza kumuomba hata laki moja.

Leo hii watoto wameenda shule,umejenga nyumba umenunua gari. Umepata mke mzuri.

Ila una inakuja kutambua hauna tena mtu hata mmoja wa maana katika circle yako.

Kwanini hauna rafiki hata mmoja maishani?
Alaaniwe amtegemeaye mwanadamu
 
Kutokana na masahibu yaliyo nipata siwezi kusimulia zaidi hapa. Maisha yangu yameharibiwa kiasi kikubwa hadi wakaanza kuwadhuru watoto kwa uchawi. Mapenzi kwa binadamu awe ndugu, jirani na marafiki upendo wangu umebaki 20%.

Tuwe waangalifu na wanadamu ni wabaya sanaa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom