Kipa mpya wa simba ni majeruhi

Nahisi kwenye mazoezi ameonekana ni Kipa kimeo. Na kocha wa makipa amemkataa, hivyo ili isijulikane kuwa walisajili kimeo, wanataka kutudanganya kuwa alikuwa mgonjwa.

Hii nafasi ya kipa mpya, ongeeni na Singida Big stars ili Beno Kakolanya arudi, au endeleeni kuwatumia hawa waliopo hadi Manula atakapopona. Kisha Peter Banda abaki Msimbazi.
Hata akiwa majeruhi kweli bado upumbavu utakuwa mkubwa sana.Kuna watu wamegeuza kuiba kama haki.
 
Huwezi kuwa na jamii iliyojaa watu wa hovyo halafu eti miongoni mwao ukapata viongozi makini, Never!!
Hivi mlivyotangaziwa hili jina mkuu si mlikuja hapa povu kama lote, sio nyie mliokuwa mnasema mmepata kipa anadaka mpaka mawazo ya mpigaji, sio nyie mliokuwa mnasema mmepata kipa anadaka hadi nzi akipita golini, anadaka hadi upepo?

Kweli makolo ni makolo tu
 
Nafikiri lilikuwa pendekezo la kocha Robertinho, kwa maana napata shida kuwalaumu viongozi wa simba kwakuwa sidhani kama walishamuona popote, isipokuwa wanatakiwa walaumiwe kwa kuruhusu scout kuingiliwa majukumu yake, suala la vigezo vya uyo kipa kutokidhi na bado uongozi ukaruhusu asaini mkataba alafu baadae unakuja kusema ni injury ni aibu ya karne!
Yule kipa sio majuruhi bali usajili umegoma. Uongozi na Micky wanachofanya ni deception ili kukwepa lawama.
Yule kipa sio mbaya na Mpaka hapo Sioni kosa la kocha. Yeye kaleta mchezaji ilikuwa ni wajibu wa viongozi kuzingatia vigezo vya usajili.
 
Hivi mlivyotangaziwa hili jina mkuu si mlikuja hapa povu kama lote, sio nyie mliokuwa mnasema mmepata kipa anadaka mpaka mawazo ya mpigaji, sio nyie mliokuwa mnasema mmepata kipa anadaka hadi nzi akipita golini, anadaka hadi upepo?

Kweli makolo ni makolo tu
Ficha Utopolo wako. Kosa la mashabiki ni lipi? Kwani huyo mchezaji ni mbovu? Hata kama kapata injury, haya huyo Manula aliye na injury ni mbaya?
 
But mi nahisi hilo la majeraha yaweza kua ni kupoza tu mashabiki ila tatizo laweza kua TFF imegoma kumuingiza kwenye mfumo wa usajili kwa kutokukidhi vigezo.

Kipindi cha leo cha Sports Am cha azam nao wameliongelea hilo
Hii ndio sababu. Wameona wazuge mgonjwa kuficha uzembe wao.
 
Nahisi kwenye mazoezi ameonekana ni Kipa kimeo. Na kocha wa makipa amemkataa, hivyo ili isijulikane kuwa walisajili kimeo, wanataka kutudanganya kuwa alikuwa mgonjwa.

Hii nafasi ya kipa mpya, ongeeni na Singida Big stars ili Beno Kakolanya arudi, au endeleeni kuwatumia hawa waliopo hadi Manula atakapopona. Kisha Peter Banda abaki Msimbazi.
Wamesikia kuna timu imekula 10-0 huku, wanaanza kujamba jamba huko kambini.
 
Dah! Simba ina wahuni wengi aisee! Kila mwaka lazima wampige mwekezaji tukio. Sasa unaenda kumsajili golikipa kutoka Brazil, halafu eti anacheza ligi daraja la 4!! Kama siyo uhuni ni nini!!

Tanzania ina walinda mlango kibao tu na wazuri wa ligi kuu! Afrika nayo imejaa walinda mlango wazuri wanaocheza mpaka kwenye timu zao za Taifa! Bado wahuni wakaenda kumleta mlinda mlango wa ligi daraja la 4 kutoka Brazil!! Tena usikute alisajiliwa kwa dau kubwa tu.
Au walisikia Yanga inataka kumsajili wakamteka Airport? Tehe tehe teheeee.
 
Back
Top Bottom