Kiongozi wa Sokwe Kigoma ajiuzulu kwa hiari yake

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,894
155,916
1687355673404.jpg

Kiongozi Mkuu wa Sokwe hapa Kigoma Kajiuzuru

Huu ni utamaduni na maadili ya Sokwe ni marufuku kufanya mapenzi na Sokwe ndani ya familia.

Sasa mkasa huo umefanya Kiongozi Mkuu wa Sokwe huko katika hifadhi ya Taifa ya Mahale iliyopo Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma kujiuzuru uongozi baada ya kupata kashifa ya kumbaka dada yake.

Mkuu wa Idara ya Utalii katika Hifadhi ya Mahale, Evance Magomba amesimulia kwa kifupi kuhusu utawala wa Sokwe na baadhi ya mila, utamaduni na desturi zao zinavyoshabihiana na binadamu alipokutana na mwandishi Jacob Ruvilo.

Evance Magomba ameeleza kwamba Binaadamu tunashabihiana na sokwe karibu asilimia 98.8, ubongo wa sokwe ni sawa sawa na ubongo wa mtoto wa miaka mitano yaani uwezo wake wa kupambanua jambo

Alpha male (Mkuu wa masokwe) kwa hapa mahale anaitwa TEDDY (dume), ni sokwe mkubwa lakini hawezi kutumia ubabe wake, yeye aliwezeshwa na mama yake katika kuyatwaa madaraka kwasababu mama yake alikua na ushawishi mkubwa kwa sokwe wengine.

Teddy alichukua uwongozi mwaka 2021, ilifikia wakati akawa amelewa madaraka kwasababu ili uwe kiongozi kwenye Sokwe lazima uhakikishe Sokwe wenzako watakula wapi kwa wiki, kwa mwezi, na mpaka kwa mwaka. Lakini TEDDY aliwaacha wenzake katika hilo hakuwajibika vyema na kuwaweka pamoja katika swala la chakula.

Lakini jambo lingine ambalo liliwaudhi sana wafuasi wake, alifanya tukio la ajabu sana la kumbaka dada yake wa kuzaliwa, hilo ni kosa kubwa sana alilolifanya kwasababu Sokwe hawajamiiani kifamilia.

Kutokana na hilo sokwe wenzake wakaona hafai tena kuwa kiongozi, na ndipo hapo yeye mwenyewe kutokana fedheha hiyo akaachia ngazi bila vurugu, kwasababu katika jamii ya sokwe ili upate uongozi ni lazima utumie nguvu, wafuasi wake walivyomtenga akaona basi uongozi wake umefika mwisho na akaachia madaraka mwenyewe bila matumizi ya nguvu.

....
Jamii za sokwe huongozwa na dume aitwae 'alpha male' ambaye maslahi yake makuu ni ngono na nguvu; viongozi wanafurahia kupata wanawake wenye rutuba na baba watoto wengi zaidi. Sokwe hawa wakuu hulinda amani kwa kuzuia migogoro katika kikundi na kudhibiti rasilimali kama vile chakula.
 
Gombe Na Mahale Kigoma Kuna Watu Wanafuatilia Maisha, Mienendo Ya Sokwe Saa 24/7
Nilifika Gombe Nikashangaa Kuna Hospital, Na Maisha Mazuri Kwaajili Ya Tafiti Tele Za Sokwe. Kulala Na Kuamka Kwao

Yaani hao nyani mmewawekea cctv ili kujua kila siku wanafanya nini?
 
Gombe Na Mahale Kigoma Kuna Watu Wanafuatilia Maisha, Mienendo Ya Sokwe Saa 24/7
Nilifika Gombe Nikashangaa Kuna Hospital, Na Maisha Mazuri Kwaajili Ya Tafiti Tele Za Sokwe. Kulala Na Kuamka Kwao
I must be there one day
 
Back
Top Bottom