Kiongozi wa Al Qaeda auawa Yemen

3squere

JF-Expert Member
Aug 2, 2011
925
181
Wakuu nchini Yemen wanasema kua kiongozi
mmoja wa mtandao wa Al Qaeda ameuawa
katika kilichoelezewa kama tafauti za kifamilia.
Haya yametokea katika mkoa wa kusini mwa
nchi ambako wapiganaji wanaodhaniwa kua
na uhusiano na al-Qaeda wametumia fursa ya
vurugu za mwaka jana kujiimarisha.
Ghasia hizi zinaashiria ni kiasi gani hali ya
usalama inazidi kua tete katika maeneo mengi
ya Yemen siku chache kabla ya kufanyika
kwa uchaguzi unaokusudia kukomesha
utawala wa kiongozi mkongwe, Ali Abdullah
Saleh.
Maelezo ya mauwaji kama haya kutoka duru
rasmi na za kikabila yanatosha kufahamisha
mengi kuhusu jinsi Yemen ilivyogawanywa
kwa misingi ya matabaka na ukabila.
Tarek al-Dahab inafahamishwa kua alikua
kiongozi wa al-Qaeda, aliyeongoza
mashambulio ya hivi karibuni ya
wakereketwa katika miji ya kusini kufaidi
kutokana na vurugu zilizokua zikiendelea
huko.
Suala jingine muhimu kuhusiana na kiongozi
huyu ni kua alikua shemeji wake Anwar al-
Awlaki,mzaliwa wa Marekani mwenye
msimamo wa imani kali aliyewekwa kwenye
orodha ya Marekani ya watu wanaotakiwa
kuuawa na mwaka uliopita aliuawa katika
shambulio la ndege inayopaa bila rubani.
Imearifiwa kua Tarek aliuawa na kakake wa
kambo, Hizam, katika kile kilichotajwa kua
ubishi juu ya mapato ya kikabila. Baada ya
mzozo Hizam na wafuasi wake walizingirwa
ndani ya nyumba walimokimbilia na wafuasi
wa Tarek.
Watu 16 akiwemo Hizam, waliuawa katika
mapigano yaliyofuata. Kila siku kuna habari za
mapigano huko kusini mwa nchi
yanayohusisha wakereketwa wa Kiislamu.
Wakereketwa hawa bado wanadhibiti mji
muhimu wa Zinjibar, waliouteka katika
mazingira ya kutatanisha mwezi Novemba.
Haya ni sehemu ya vigezo vinavyoikabili
serikali ya mseto iliyoteuliwa baada ya Rais
Saleh hatimaye kukubali kujiuzulu mwaka jana.
Uchaguzi wa Rais uliopangwa ili kukomesha
enzi ya miaka 30 ya utawala wa Rais Saleh
unatazamiwa siku ya jumanne ijayo.
Kuna mgombea mmoja, ambaye ni Naibu
makamu wa Rais, Abdrabbu Mansour Hadi
ambaye picha yake ilianza kitambo kuwekwa
mahala pa Rais wa zamani.
Ushahidi zaidi ya wa hali mbovu ya usalama ni
ukosefu wa utulivu mwandishi wa BBC nchini
Yemen alishambuliwa na watu wenye silaha
siku ya jumatano, ambao BBC ina amini kua
wafuasi wa Bw.Saleh. Shirika la utangazaji la
BBC limewasihi wakuu wa Yemen
wahakikishe kua wandishi habari
wanaendesha kazi zao bila kunyanyaswa.
Alamisha hii
 
Wakuu nchini Yemen wanasema kua kiongozi mmoja wa mtandao wa Al Qaeda ameuawa katika kilichoelezewa kama afauti za kifamilia. Haya yametokea katika mkoa wa kusini mwa nchi ambako wapiganaji wanaodhaniwa kua na uhusiano na al-Qaeda wametumia fursa ya vurugu za mwaka jana kujiimarisha. Ghasia hizi zinaashiria ni kiasi gani hali ya usalama inazidi kua tete katika maeneo mengi ya Yemen siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi unaokusudia kukomesha utawala wa kiongozi mkongwe, Ali Abdullah Saleh. Maelezo ya mauwaji kama haya kutoka duru rasmi na za kikabila anatosha kufahamisha mengi kuhusu jinsi Yemen ilivyogawanywa kwa misingi ya matabaka na ukabila. Tarek al-Dahab inafahamishwa kua alikua kiongozi wa al-Qaeda, aliyeongoza mashambulio ya hivi karibuni ya wakereketwa katika miji ya kusini kufaidi kutokana na vurugu zilizokua zikiendelea huko. Suala jingine muhimu kuhusiana na kiongozi huyu ni kua likua shemeji wake Anwar al- Awlaki,mzaliwa wa Marekani mwenye msimamo wa imani kali aliyewekwa kwenye orodha ya Marekani ya watu wanaotakiwa kuuawa na mwaka uliopita aliuawa katika shambulio la ndege inayopaa bila rubani. Imearifiwa kua Tarek aliuawa na kakake wa kambo, Hizam, katika kile kilichotajwa kua ubishi juu ya mapato ya kikabila. Baada ya mzozo Hizam na wafuasi wake walizingirwa ndani ya nyumba walimokimbilia na wafuasi wa Tarek. Watu 16 akiwemo Hizam, waliuawa katika mapigano yaliyofuata. Kila siku kuna habari za mapigano huko kusini mwa nchi yanayohusisha wakereketwa wa Kiislamu. Wakereketwa hawa bado wanadhibiti mji muhimu wa Zinjibar, waliouteka katika mazingira ya kutatanisha mwezi Novemba. Haya ni sehemu ya vigezo vinavyoikabili serikali ya mseto iliyoteuliwa baada ya Rais Saleh hatimaye kukubali kujiuzulu mwaka jana. Uchaguzi wa Rais uliopangwa ili kukomesha enzi ya miaka 30 ya utawala wa Rais Saleh unatazamiwa siku ya jumanne ijayo. Kuna mgombea mmoja, ambaye ni Naibu makamu wa Rais, Abdrabbu Mansour Hadi ambaye picha yake ilianza kitambo kuwekwa mahala pa Rais wa zamani. Ushahidi zaidi ya wa hali mbovu ya usalama ni ukosefu wa utulivu mwandishi wa BBC nchini Yemen alishambuliwa na watu wenye silaha siku ya jumatano, ambao BBC ina amini kua wafuasi wa Bw.Saleh. Shirika la utangazaji la BBC limewasihi wakuu wa Yemen wahakikishe kua wandishi habari wanaendesha kazi zao bila kunyanyaswa. Alamisha hii
 
Back
Top Bottom