Kiongozi Mfano wa Nyerere! yuko wapi tumchague?

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,429
Wakuu hivi ni nani?

Ni nani tukimchagua kuwa kiongozi anaweza kuupunguza mshahara wake mwenyewe na kuagiza mshahara wa viongozi wenzake wanaochukua mshahara mkubwa mno upunguzwe ili waongezewe wale ambao mshahara wao huishia kwenye dalala dala na kupanga chumba kimoja! ni nani ?

Ni nani ambaye tukimchagua kuwa kiongozi wetu, ataweza kuwa mwandishi wa vitabu, na vitabu vyake viwe vinakubalika kama vya Nyerere?

Nani ambaye anaweza akawa karibu na wananchi wa chini kabisa na waliosahauliwa, kama ambavyo Mwalimu alivyokuwa hata wakati fulani akawa anacheza bao na watu wa chini kabisa bila kuhofia usalama wake kwa kuwa watu wa chini ndio walikuwa kipenzi chake! nani tumchague?

Tumchague nani ambaye ataweza kutoa hotuba zitakazowagusa na kuwafurahisha watanzania kama zilivyokuwa hotuba za Nyerere? nani tumchague?

Tumchague nani ambaye atakuwa mtu wa watu kama nyerere, mtu asiye na makuu hata kidogo? nani tumchague?

Tumchague nani mwenye mabavu ya kulitunishia misuli taifa lolote (hata kama ni kubwa) pale linapotishia maslahi ya nchi? nani tumchague?

Tumchague nani ambaye haogopi mijadala na wananchi wake, na pakiwa na suala linalohitaji mjadala wa kitaifa anaweza kushiriki kujibu maswali ya uso kwa uso bila kuogopa? nani tumchague?

Tumchague nani anayeweza kuwarudisha watanzania katika hali ya uzalendo kama ilivyokuwa miaka ya 1970? yuko wapi tumchague!

Tumchague nani ambaye anaweza akawafanya watu kama hawa hapa chini nao wakajihisi ni watu?

Wanafunzi+wa+shule+ya+msingi+Etaro+wakiwa+darasani.Shule+hii+ipo+wilaya+ya+Musoma+vijijini.JPG

Nani ?ee! 2015 yupo mtu wa namna hii tumchague?
 
Nyoka wa ndimi 2 a.k.a EL (ndanda kosovo) anafaa kwani huhangaika sana na miradi mikubwa kuchumia tumbo lake huku akilia kuwa shule za kukaa chini (kata) ni maendeleo makubwa kwa taifa letu na vijana wasio na ajira ni bomu linalosubiri kulipuka. kwenye vikao vya nec ccm hayasemi haya ila akikatiza mitaani anayesema sana sijui ndo kusema ni kukua kwa kuelekea utotoni/uzeeeni? aghaaaa.... ugombea wa uraisi unamtesa na wenyewe ccm ndo chaguo lao eti???
 
Mkuu wala usihangaike , CDM kuna Lundo la watu wa mfano wa Nyerere , wale wanaotaka rasirimali za nchi hii zimfaidishe kila raia , wapo tena wengi tu .
 
kama hatuna mtu kama huyo leo hii (kwa wale wanaofikiri hivyo) ni nani ambaye anaweza kutoa sababu za msingi kwamba kwa nini hatuna ?
 
Dr.W.Slaa anafaa kuwa rais japo hakosi vikasoro vya hapa na pale. kuifanye hii chadema iwe umara hadi leo mbele ya msitu wa mbwa mwitu wenye njaa Ccm si mchezo wakuu!!!
 
Last edited by a moderator:
Mh! Mkuu hili swali ulilouliza hakuna wa kulijibu kwa sababu hakuna mtu huyo Tanzania ya leo,labda mama Maria Nyerere kama atasema anagombea urais 2015, ila tunaweza kuwapata watu wenye uchungu na mapenzi kwa Tanzania na hapo si kwingine zaidi ya CDM,maana ndani ya CCM(UKOO WA PANYA) hakuna......Nyerere atabaki kuwa Nyerere na mfanowe hautatokea leo wala kesho,japo wengine wanapinga hadharani kishabiki lkn ndani ya mioyo yao ukweli wanaujua.
 
Wakuu hivi ni nani?

Ni nani tukimchagua kuwa kiongozi anaweza kuupunguza mshahara wake mwenyewe na kuagiza mshahara wa viongozi wenzake wanaochukua mshahara mkubwa mno upunguzwe ili waongezewe wale ambao mshahara wao huishia kwenye dalala dala na kupanga chumba kimoja! ni nani ?

Ni nani ambaye tukimchagua kuwa kiongozi wetu, ataweza kuwa mwandishi wa vitabu, na vitabu vyake viwe vinakubalika kama vya Nyerere?

Nani ambaye anaweza akawa karibu na wananchi wa chini kabisa na waliosahauliwa, kama ambavyo Mwalimu alivyokuwa hata wakati fulani akawa anacheza bao na watu wa chini kabisa bila kuhofia usalama wake kwa kuwa watu wa chini ndio walikuwa kipenzi chake! nani tumchague?

Tumchague nani ambaye ataweza kutoa hotuba zitakazowagusa na kuwafurahisha watanzania kama zilivyokuwa hotuba za Nyerere? nani tumchague?

Tumchague nani ambaye atakuwa mtu wa watu kama nyerere, mtu asiye na makuu hata kidogo? nani tumchague?

Tumchague nani mwenye mabavu ya kulitunishia misuli taifa lolote (hata kama ni kubwa) pale linapotishia maslahi ya nchi? nani tumchague?

Tumchague nani ambaye haogopi mijadala na wananchi wake, na pakiwa na suala linalohitaji mjadala wa kitaifa anaweza kushiriki kujibu maswali ya uso kwa uso bila kuogopa? nani tumchague?

Tumchague nani anayeweza kuwarudisha watanzania katika hali ya uzalendo kama ilivyokuwa miaka ya 1970? yuko wapi tumchague!

Tumchague nani ambaye anaweza akawafanya watu kama hawa hapa chini nao wakajihisi ni watu?

Wanafunzi+wa+shule+ya+msingi+Etaro+wakiwa+darasani.Shule+hii+ipo+wilaya+ya+Musoma+vijijini.JPG

Nani ?ee! 2015 yupo mtu wa namna hii tumchague?

dr. peter w. slaa....
 
Dr.W.Slaa anafaa kuwa rais japo hakosi vikasoro vya hapa na pale. kuifanye hii chadema iwe umara hadi leo mbele ya msitu wa mbwa mwitu wenye njaa Ccm si mchezo wakuu!!!

asante kwa ukweli mkuu....
 
Last edited by a moderator:
Nimeamini leo kuwa watanganyika hamuwezi kufikiri zaidi ya nyerere,utumwa wa mawazo.
 
kunawatu ambao tunadhani watakuwa wagombea lakini mungu anaweza kuwachukua ngoja nisubiri wajitokeze ndipo nitajua ni yupi anafaa,
 
Back
Top Bottom