Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,048
- 144,454
New CCM Secretariat:
Secretary General: Kinana;
Deputy Secretary General: Mwigulu;
Deputy Secretary General: Ali Vuai;
Foreign: Migiro;
Finance: Meghji;
Organisation: M.S.Khatib;
Publicity: Nape
Previously:
Secretary General: Kinana;
Deputy Secretary General: Mwigulu;
Deputy Secretary General: Ali Vuai;
Foreign: Migiro;
Finance: Meghji;
Organisation: M.S.Khatib;
Publicity: Nape
Previously:
- Mukama kung'olewa, nyota ya Nape yang'ara
WAKATI mjadala wa nani anatoka katika uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na nani anaingia, hususan katika sekretariati mpya ya chama hicho ukiwa umeshika kasi, jina la Abdulhaman Kinana limetajwa kuwa huenda akateuliwa kushika nafasi hiyo.
Kitendawili cha mjadala huo ulio gumzo ndani na nje ya CCM, kinatarajiwa kinateguliwa leo na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Rais Jakaya Kikwete.
Tayari Rais Kikwete ameshamteua Katibu Mkuu wa zamani, Philip Mangula, kuwa Makamu Mwenyekiti, akirithi mikoba ya Pius Msekwa, mwanasiasa mkongwe na mzoefu akiwa na rekodi ya kuwahi kuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa kwanza wa CCM.
Hii ni mara ya pili kwa jina la Kinana kuchomoza kuwa mtu anayefaa kushika nafasi hiyo kwani miaka miwili iliyopita wakati Rais Kikwete alipovunja Kamati Kuu (CC) na sekretarieti na kuziunda upya, Kinana alitajwa kuwa angeteuliwa kushika wadhifa huo.
Hata hivyo, Rais Kikwete alimteua Willson Mukama, akirithi mikoba ya Mzee Yusuf Makamba.
Duru za siasa kutoka ndani ya CCM, zinasema kuwa kwa sasa Mukama anaonekana kushindwa kumudu uendeshaji wa siasa za sasa, ikiwa ni dhahiri ameshindwa kumudu siasa za jukwaani.
Habari za ndani ya CCM ambazo gazeti hili imezipata, zilisema kuwa jina la Kinana ni moja ya majina yaliyopendekezwa na Makamu Mwenyekiti mpya, Mangula, ambaye anaelezwa kumpa masharti Rais Kikwete ya kufanya kazi na Katibu Mkuu atakayesimamia maamuzi yake.
"Jina la Kinana limetokana na masharti ya Mangula ambaye alimwambia Jakaya kwamba anataka kufanya kazi na katibu atakayeweza kusimamia maamuzi yake hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2015," kilisema chanzo chetu cha habari.
Sifa moja kubwa anayotajwa kuwa nayo Kinana ni msimamo mkali dhidi ya masuala ya ufisadi na kubwa zaidi anatajwa kuwa bingwa wa mikakati ya kisiasa ndani ya chama hicho.
Itakumbukwa kuwa Kinana ndiye aliyeongoza kampeni za Benjamin Mkapa mwaka 1995, dhidi ya Augustine Mrema, aliyekuwa mwanasiasa maarufu na aliyekubalika kwa wakati huo.
Tangu wakati huo, Kinana amekuwa akiongoza kampeni za urais. Ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM anayetajwa kusimamia mawazo anayoamini ni sahihi, lakini akiwa tayari kuunga mkono hoja zenye lengo la kukijenga chama hicho.
Hata hivyo, Kinana alipata kukaririwa kwamba anang'atuka siasa baada ya kuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) kwa miaka 25 mfululizo.
Mbali ya Kinana, jina lingine linalotajwa kushika nafasi hiyo ni la Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Nyota ya Nape Nnauye ndiyo inayong'ara zaidi akitajwa kuchangamsha siasa za jukwaani na za kiutendaji za chama hicho.
Nape anapewa nafasi kubwa kutokana na uwezo wake kisiasa, lakini pia ni kutokana na kuungwa mkono na vijana wengi hata nje ya chama hicho, ambao kimsingi, ndio wanaobeba jahazi la kisiasa nchini.
Mabadiliko mengine yanatajwa katika nafasi ya Katibu ya Uchumi na Fedha ambayo kwa sasa inashikiliwa na Mwigulu Nchemba.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, naye anatajwa kuweza kumng'oa Mwigulu.
Mwigulu anatajwa kushindwa kukiwezesha chama hicho kuacha kutegemea ruzuku kuendesha shughuli zake.
Tangu ashike wadhifa huo, Mwigulu anatajwa kuendesha shughuli nyingine za kisiasa na kusahau jukumu la msingi la kufufua uchumi wa chama hicho chenye rasilimali nyingi nchini.
Kwenye nafasi ya Itikadi na Uenezi, ambayo jina la Nape nalo linatajwa, linaweza pia kuchukuliwa na William Ngeleja, William Lukuvi na Katibu wa Vijana wa CCM (UVCCM), Martine Shigela.
Katika hatua nyingine, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, amelazima kutumia nguvu ya ziada kuwalainisha wajumbe wa mkutano mkuu waliopanga kupiga kura za hapana kwa Rais Kikwete.
Mzee Makamba akitumia vitabu vya dini alimwelezea Kikwete kama mtu wa watu aliyeletwa na Mungu kuwaongoza wengine.
Hadi jana jioni majira ya saa moja kura za Mwenyekiti (Kikwete) na Makamu wake wawili (Mangula) na Dk. Ali Mohamed Shein, zilikuwa zinahesabiwa.
Chanzo: Tanzania Daima