Kinachotokea Iringa, Tafsiri Yangu...

Majjid ni mnafiki tu...anashindwa kumalaumu Meya wa Iringa ambaye ndie Diwani wa Mlandege sbb ni rafiki yake,na hukaa pamoja ktk vijiwe...hio hali ya kutokuwa na busara imetoka kwa Msigwa tuu...vip kuhusu Meya wa Iringa Aman Mwamwindi?....Mjengwa unafiki utakupeleka kubaya sana...tulio Iringa tunajua hali halisi
Kuwa Mbunge wa chama cha upinzani ktk nchi kama Tanzania unahitaji moyo mkuu sana..kama binadamu Msigwa anafanya kazi katika mazingira magumu sana...kuanzia mkuu wa mkoa,wilaya,mkurugenzi wa manispaa,meya hata RPC wanakuwa ni maadui na wanamkwamisha...Mashine Tatu ilikuwa ni sera ya mSIGWA,ILI KUONEKANA HAJATIMIZA...CCM wameamua kuwapeleka nje ya mji wamachinga..lakini hapo mashine tatu Gulio huwa ni siku moja tu nayo ni J'pili...sasa kuna shida gani?na Msigwa akawmbia kama haiwezekani basi waende viwanja vya Mwembetogwa,laikn MCCM hayataki....
Majjid acheni unafiki,mana huo unafiki haulipi...Lie has a speed to spread,but truth has induarance

ILI KUWAWEKA SAWA POLISI ELIMU INAHITAJIKA SANA.....KWA JICHO HILI LA ISHENGOMA...KAZI IPO

Attachments

• policcm.jpg
policcm.jpg
30.8 KB · Views: 58
• Thanks
Reactions: mka
Majjid,ubarikiwe,hakika chadema shetani anawatumia kuliangamiza taifa,wewe unayejiita mchungaji hebu Nijibu ni lini Huyu Yesu unedai kumtumikia alikua akihamasisha umma kupinga utawala na kuleta machafuko,wewe ni ajenti wa kuzimu,unatimiza unabii mkuu wa Mungu wa siku za mwisho,wewe ni mtumishi wa dunia hii sio wa ulimwengu ujao,acha kutumia jina la Yesu kwa tumbo lako,shetani amewakamata mmeamua kuliangamiza taifa letu,na sisi hatutawaacha ,the current state of our dear nation is fast filling up its cup of iniquity throug CHADEMA,violence and crime of political gain are filling our nation,and Satan is using Mchungaji msigwa to torn apart this innocent Nation.

The youth who walk the streets are surrounded with handbills and noice of crime and sin,their mind are educated to misbehave and crime,hatred and sin against the government,ole wenu chadema mnaodhani Mungu anazibariki kazi hizi za Ibilisi.

Mungu lete utulivu watu Wako tumalize kazi,Yesu urudi kulichukua kanisa lako,Amen

INAWEZEKANA DINI YAKO NI BORA SANA, Lakini kutukana viongozi wa dini au madhehebu yasiyokuhusu haikusaidii.. Hasa mtu unayejifanya mtetezi wa haki na amani.

Majjid amenena jambo la kweli kabisa. Tatizo la Msigwa (ambaye nina shaka na uchungaji wake), ni kwamba anataka kujipatia umaarufu kwa nguvu kubwa kwa staili ya Lema. Wahenga walisema ukimwiga tembo kunya, utapasuka msamba!

Msigwa anapaswa kujitafakari na kurejea maandiko ambayo anataka tuamini kuwa ameyasoma kiasi cha kustahili kuitwa Mchungaji. Naunga mkono hoja ya Majjid.

SIAMINI KAMA DINI YA MTU INAUHUSIANO NA TUKIO HILI!.. KAMA WEWE NI MKRISTO UNASOMA BIBLIA IPI INAYOKUFUNDISHA UNAFIKI?... UKIONA HUELEWI ULIZA TUKUPE VERSES.

ni mchungaji aliyeusomea uchungaji wa dini ambayo MSINGI wake ni MAPENDO. Mh. Msigwa amuamua kutenda the other way around. Hizi ndizo siasa zetu zisizokuwa na sheria.

DINI IMEINGIAJE HAPA?.. MBONA KILA MTU HAMUANZI KUMCHAMBUA KULINGANA NA DINI YAKE?.. Kwa nini usiwazungumzie viongozi wa dini yako?.

Hivi mbona nyie viongozi wenu wa dini hamuwatukani, ila kila siku mnakesha kutukana viongozi wa dini nyingine?

quote_icon.png
By kingukitano

Majjid,ubarikiwe,hakika chadema shetani anawatumia kuliangamiza taifa,wewe unayejiita mchungaji hebu Nijibu ni lini Huyu Yesu unedai kumtumikia alikua akihamasisha umma kupinga utawala na kuleta machafuko,wewe ni ajenti wa kuzimu,unatimiza unabii mkuu wa Mungu wa siku za mwisho,wewe ni mtumishi wa dunia hii sio wa ulimwengu ujao,acha kutumia jina la Yesu kwa tumbo lako,shetani amewakamata mmeamua kuliangamiza taifa letu,na sisi hatutawaacha ,the current state of our dear nation is fast filling up its cup of iniquity throug CHADEMA,violence and crime of political gain are filling our nation,and Satan is using Mchungaji msigwa to torn apart this innocent Nation.

The youth who walk the streets are surrounded with handbills and noice of crime and sin,their mind are educated to misbehave and crime,hatred and sin against the government,ole wenu chadema mnaodhani Mungu anazibariki kazi hizi za Ibilisi.

Dini ya kikristo wewe huifahamu hata chembe kaa pembeni. Jadili siasa. DINI yakikristo haiandai watu wanafiki.

DINI IMEINGIAJE HAPA?.. MBONA KILA MTU HAMUANZI KUMCHAMBUA KULINGANA NA DINI YAKE?.. Kwa nini usiwazungumzie viongozi wa dini yako?.

Hivi mbona nyie viongozi wenu wa dini hamuwatukani, ila kila siku mnakesha kutukana viongozi wa dini nyingine?
Mkuu mbona unajenga hoja kwa hisia?. Unajenga hoja kwa kujiaminisha kama unaifahamu dini yangu na viongozi wangu wa dini.

Kwako mtu yoyote anagusia imani ya dini ya Msigwa katika hali hasi, bali huyo ni yuko against dini ya msigwa. Hizi ni hoja mfu kama siyo za kitoto.

Kwa kukusaidia, mimi ni practising Roman Catholic na hata secondary nimesomea seminary baada ya kuwa mtumikiaji wa artare nikiwa primary school. Kwa hiyo Kardinali Pengo ni kiongozi wangu na ndiyo maana nikatumia maneno yake katika kuweka ujumbe.

Badilisha mtazamo wako na ufahamu siyo wote wanaoponda maamuzi ya Msigwa wanafanya hivyo kwa msukumo wa dini yake. Tatizo kwa sasa nchini la Watanzania wachache kama wewe, fikra zenu kisiasa zimejaa msukumo wa kidini hata kwa mambo ambayo ni PURE POLITICS.

Badilikeni.

Ndugu zangu,

Leo saa mbili na nusu asubuhi nilifika Jengo la NSSF nikitokea kufanya jogging yangu ya asubuhi. Nilifika hapo kuwahi kununua magazeti.

Hali ilikuwa shwari kama ilivyo kawaida ya Iringa Jumapili asubuhi. Kunako saa tatu asubuhi nilipokuwa nyumbani nikisoma magazeti, ndipo niliposikia mlio wa kwanza wa bomu la machozi. Idadi yake ikaanza kuongezeka.

Nikiwa na kamera yangu nikajisogeza hadi katikati ya mji kufahamu zaidi kinachotokea. Nilichokiona ni vurugu kati ya Wamachinga na Jeshi la Polisi.

Tatizo?

Ni dogo sana, lakini linakuzwa kwa vile siasa imepelekwa mbele badala ya kutanguliza hekima na busara. Kwa kufuatilia suala la Wamachinga kufanya biashara eneo la barabarani pale Mashine tatu naamini kabisa, kuwa Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa angeweza kuepusha hali inayoendelea sasa kwa kuwasihi Wamachinga watii kwanza amri ya Manispaa, na yeye, kama Mbunge wao, kujiingiza kwenye mazungumzo ya dhati na wenzake kwenye Halamshauri ya Manispaa ya Iringa katika kutafuta ufumbuzi wa suala hili. Na hiyo ndio siasa. Siasa ina maana ya majidiliano endelevu badala ya kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu pale milango ya majadiliano ingali wazi.

Kinachotokea Iringa kwa sasa ni doa kubwa kwa mji wetu wenye sifa ya muda mrefu ya utulivu. Kina athari kubwa kiuchumi pia. Pale Iringa mjini nilichokiona leo ni kama mji ulio katika mapigano ya kivita. Watu ni wachache na wenye hofu.

Biashara nyingi zimesimama. Niliziona Daladala zikitoka Kituo cha Miyomboni bila hata abiria, watoke wapi? Wakati kwa sasa walio nje ya mji wameambiwa na jamaa zao walio katikati ya mji kuwa wasijaribu kufika mjini, kwamba hali imechafuka.

Nimeongea na mwuza nyama ya bucha aliyeniambia kuwa mgomo wa Daladala wa hivi karibuni ulimfanya apate hasara kubwa kwenye biashara yake ya nyama kwa vile wateja wake wengi wanatoka nje ya mji. Na anachokiona leo ni hasara nyingine kwa vile hakutakuwa na biashara nzuri. Je, ni wafanyabiashara wangapi watakaoathirika na hali hii ya leo?

Na kwa kuwa mkweli, kisiasa kinachotokea Iringa kwa sasa kinaweza kuwa na athari hasi kwa Mchungaji Msigwa badala ya kumjenga kisiasa, kwani, wengi niliozungumza nao katikati ya mji wanamwona Mchungaji Msigwa kuwa ni mtu ambaye angeweza kuiepusha hali hii kama asingeyatumia majukwaa ya siasa kuwahamasisha Wamachinga kuendelea kufanya biashara, na hivyo, kutokutii amri ya Manispaa.

Mchungaji Msigwa ni rafiki yangu, muda mfupi uliopita nimempigia simu. Imeita bila majibu. Mmoja wa watu wake wa karibu ameniambia yuko kwenye Harambee pale Tumaini University.

Kama Mchungaji Msigwa angejibu simu yangu, basi, ningemwambia haya ninayoyaandika hapa.

Maggid Mjengwa,
Iringa.
0754 678 252
MjengwaBlog :: Habari, Picha, Matangazo na Matukio

Hao watawala walishindwa kutumia busara kuwaacha WAMACHINGA wafanye biashara zao, kwani pangetokea nini? ungesema pande zote sawa lakini wewe unamlaumu MSIGWA na kutetetea wafanyabiashara wakubwa tu, wadogo je? hapo wewe nawe una Maslahi binafsi.

Majjid amenena jambo la kweli kabisa. Tatizo la Msigwa (ambaye nina shaka na uchungaji wake), ni kwamba anataka kujipatia umaarufu kwa nguvu kubwa kwa staili ya Lema. Wahenga walisema ukimwiga tembo kunya, utapasuka msamba!

Msigwa anapaswa kutumia weledi na busara. Hata kama Chadema wataongoza nchi hii, lazima wafuate taratibu za mazungumzo na kuheshimu sheria. Kumbuka, kuondolewa kwa machinga hapo walipo ni kutokana na kuonekana kunaweza kutokea maafa ya ajali na kupoteza vijana/watu wengi. Sioni kosa la Manispaa kuchukua hadhari mapema kabla ya kufikwa na maafa.

Siasa nyepesi na kutafuta umaarufu haraka haraka ni mambo yasiyoweza kuisaidia tanzania. Siasa za kina Gandhi na kina Martin Luther King Jr, hata kina Mwalimu Nyerere za kutumia nguvu za hoja bila vurugu, zina tija kubwa sana. Msigwa anapaswa kujitafakari na kurejea maandiko ambayo anataka tuamini kuwa ameyasoma kiasi cha kustahili kuitwa Mchungaji.

Naunga mkono hoja ya Majjid.

Manyerere Jackton unapajua Iringa vizuri au povu tu?

Last edited by a moderator:
Ndugu yetu Maggid kwanza tunashukuru kwa kuwa bado uko huru baada ya kukiepuka kile kikombe!
hebu ni jibu haya maswali
1. ulitambuaje na kuhakiki kuwa miliyo uliyokuwa ukiisikia ilikuwa ni ya "mabomu ya machozi" ilhali ulikuwa hujafika kwenye eneo la tukio?? Au ulihudhurishwa kwanye mafunzo maalumu? na nani? ili iweje?
2. Umeonesha concern kubwa sana kwa muuza nyama na wenye daladala na kutoa dukuduku lako kuwa watakosa faida za bihashara zao. Hujaona haja kabisa ya umuhimu wa Machingas nao kufanya bihashara zao ilikujikimu na maisha, ukizingatia kwamba bihashara zao imebeba vijana wengi ambao wasipojengewa mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao nahisi hata huo usalama unaohuzungumzia hautakwepo, na hata hiyo jogging yako ya alfajiri haitakuwa salama. kwako wewe mmchinga asipofanya bihashara ni sahihi kabisa, ila mwenye bucha hahaa!!!??

Upuuzi huu utawagharimu sana. lazima serikali na wewe pia mkumbuke kuwa hata "Mbwa Mwoga akichoka kuonewa anang'ata" tena vibaya sana! Nafikiri wewe kama kioo cha jamii wapaswa kufanya uchambuzi wa haja ili kubalance stori! sishangai tena manake baadhi ya waandishi wetu wa habari siyo tena "kioo cha jamii" bali wamegeuka kuwa "Choo cha Jamii"!!!
maggid ni vema ukajikita kujibu hoja za huyu ndugu Mjanga

Last edited by a moderator:
Majjid,ubarikiwe,hakika chadema shetani anawatumia kuliangamiza taifa,wewe unayejiita mchungaji hebu Nijibu ni lini Huyu Yesu unedai kumtumikia alikua akihamasisha umma kupinga utawala na kuleta machafuko,wewe ni ajenti wa kuzimu,unatimiza unabii mkuu wa Mungu wa siku za mwisho,wewe ni mtumishi wa dunia hii sio wa ulimwengu ujao,acha kutumia jina la Yesu kwa tumbo lako,shetani amewakamata mmeamua kuliangamiza taifa letu,na sisi hatutawaacha ,the current state of our dear nation is fast filling up its cup of iniquity throug CHADEMA,violence and crime of political gain are filling our nation,and Satan is using Mchungaji msigwa to torn apart this innocent Nation.

The youth who walk the streets are surrounded with handbills and noice of crime and sin,their mind are educated to misbehave and crime,hatred and sin against the government,ole wenu chadema mnaodhani Mungu anazibariki kazi hizi za Ibilisi.

Mungu lete utulivu watu Wako tumalize kazi,Yesu urudi kulichukua kanisa lako,Amen

Bandiko lako lina busara nyingi za kuchukua na pia linanifanya machozi yananilengalenga kwa uchungu mkuu. Ubarikiwe na wewe mkuu.

maggid huo ni unafiki kwanini usilaumu polisi kwa kutumia nguvu nyingi kwa issue dogo kama hii

Kumlaumu leo mchungaji Msigwa ni kama kusubiri maji yakauke ndipo ulaumu moto wakati yanachemka uliyaona na hukutoa moto. machinga wamekaa Mlandege kwa zaidi ya mwaka mzima, ni wakati mrefu wenye hasara na maisha magumu kwa watanzania hawa. Navyomfahamu Mchungaji Msigwa si mtu wa vurugu na inapofikia kuhamasisha riots ujue ni jambo lililoonekana kukosa haki. INGEKUWA NI MACHINGA WAMEPAMBANA WENYEWE NINGEMLAUMU MSIGWA, ILA KWA KUWA POLIS HUDHANI MABOMU NDIO DEMOCRASIA, ASILAUMIWE MSIGWA BALI TUJIULIZE NI NANI KAWATOA FFU LUGALO KITUONI NA KUWALETA MASHINE TATU KUPIGA MABOMU? Huyo ndiye adui wa haki na alaumiwe Mtoa mada wewe ni mwandishi maarufu sana, sidhani kama hukumbuki kwamba polisi walewale waliofanya unyama huu mbaya kwa Mwangosi bila hata huruma ndio haohao unaotaka kuwatetea leo. Nadhani ni vyema ukafikiri tena kwa kina kwamba ni mabomu mangapi yalirushwa na Machinga jana ndipo umjue ni nani alifanya vurugu jana na kwa malengo gani.

Mungu iponye iringa yetu maana hatukuzoea haya, BUT WHY ALWAYS IS OUR MILITARY FORCES AGAINST US, DONT WE OWN THEM? DO THEY EXIST FOR OUR DOOM, OR FOR OUR SAFETY?

Tatizo Msingwa anaiga tabia ya Lema, lakini inabidi ajue kuwa hulka ya mnyalukolo ni tofauti kabisa na hulka ya chalii.

Hizi zote ni harakati za Msigwa kujaribu kujisafisha jina lake baada ya kujidhalilisha kwa hotuba mbovu aliyotoa. Kama hotuba kashatoa, maji yameshamwagika, ajitahidi tu next time atoe hotuba yenye mashiko.

Maggid, poleni sana hapo. tafadhli jitahidi kumtafuta Msigwa muongee, afanye siasa za kujenga nchi. Naona katuma vijana wake waje kusema kashikwa na polisi kumbe yuko kwenye Harambee!!!

Mkuu,
hichi ulichokiandika nadhani hata wewe huamini. Hotuba ile ya kusema kwamba Kinana ni mwizi wa Pembe za ndovu ndo imemjenga. Kwani kinana hajaiba pembe?

Mkuu,
hichi ulichokiandika nadhani hata wewe huamini. Hotuba ile ya kusema kwamba Kinana ni mwizi wa Pembe za ndovu ndo imemjenga. Kwani kinana hajaiba pembe?

Kiongozi,
iko thread ndefu sana hapa ambayo wadau walithibitisha kukatishwa tamaa na Msigwa. Kiujumla lilikuwa jambo la aibu mno kiasi kwamba Dr. Slaa alikosa pa kuficha macho yake.

Bunge lijalo mimi nitashiriki kuhakikisha unafanikiwa kuchukua jimbo ili ukaionbgezee nguvu kambi ya upinzani. Kiujumla Msigwa mchango wake wa maana ni kuwa kuchaguliwa kwake kumeongeza idadi ya wabunge wa viti maalum. Hana machango mwingine. Tunataka wabunge kama nyinyi ambao mnaamini mambo manayosema...

Ndugu zangu,

Leo saa mbili na nusu asubuhi nilifika Jengo la NSSF nikitokea kufanya jogging yangu ya asubuhi. Nilifika hapo kuwahi kununua magazeti.

Hali ilikuwa shwari kama ilivyo kawaida ya Iringa Jumapili asubuhi. Kunako saa tatu asubuhi nilipokuwa nyumbani nikisoma magazeti, ndipo niliposikia mlio wa kwanza wa bomu la machozi. Idadi yake ikaanza kuongezeka.

Nikiwa na kamera yangu nikajisogeza hadi katikati ya mji kufahamu zaidi kinachotokea. Nilichokiona ni vurugu kati ya Wamachinga na Jeshi la Polisi.

Tatizo?

Ni dogo sana, lakini linakuzwa kwa vile siasa imepelekwa mbele badala ya kutanguliza hekima na busara. Kwa kufuatilia suala la Wamachinga kufanya biashara eneo la barabarani pale Mashine tatu naamini kabisa, kuwa Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa angeweza kuepusha hali inayoendelea sasa kwa kuwasihi Wamachinga watii kwanza amri ya Manispaa, na yeye, kama Mbunge wao, kujiingiza kwenye mazungumzo ya dhati na wenzake kwenye Halamshauri ya Manispaa ya Iringa katika kutafuta ufumbuzi wa suala hili. Na hiyo ndio siasa. Siasa ina maana ya majidiliano endelevu badala ya kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu pale milango ya majadiliano ingali wazi.

Kinachotokea Iringa kwa sasa ni doa kubwa kwa mji wetu wenye sifa ya muda mrefu ya utulivu. Kina athari kubwa kiuchumi pia. Pale Iringa mjini nilichokiona leo ni kama mji ulio katika mapigano ya kivita. Watu ni wachache na wenye hofu.

Biashara nyingi zimesimama. Niliziona Daladala zikitoka Kituo cha Miyomboni bila hata abiria, watoke wapi? Wakati kwa sasa walio nje ya mji wameambiwa na jamaa zao walio katikati ya mji kuwa wasijaribu kufika mjini, kwamba hali imechafuka.

Nimeongea na mwuza nyama ya bucha aliyeniambia kuwa mgomo wa Daladala wa hivi karibuni ulimfanya apate hasara kubwa kwenye biashara yake ya nyama kwa vile wateja wake wengi wanatoka nje ya mji. Na anachokiona leo ni hasara nyingine kwa vile hakutakuwa na biashara nzuri. Je, ni wafanyabiashara wangapi watakaoathirika na hali hii ya leo?

Na kwa kuwa mkweli, kisiasa kinachotokea Iringa kwa sasa kinaweza kuwa na athari hasi kwa Mchungaji Msigwa badala ya kumjenga kisiasa, kwani, wengi niliozungumza nao katikati ya mji wanamwona Mchungaji Msigwa kuwa ni mtu ambaye angeweza kuiepusha hali hii kama asingeyatumia majukwaa ya siasa kuwahamasisha Wamachinga kuendelea kufanya biashara, na hivyo, kutokutii amri ya Manispaa.

Mchungaji Msigwa ni rafiki yangu, muda mfupi uliopita nimempigia simu. Imeita bila majibu. Mmoja wa watu wake wa karibu ameniambia yuko kwenye Harambee pale Tumaini University.

Kama Mchungaji Msigwa angejibu simu yangu, basi, ningemwambia haya ninayoyaandika hapa.

Maggid Mjengwa,
Iringa.
0754 678 252
MjengwaBlog :: Habari, Picha, Matangazo na Matukio

Naona hapa kuna watu ambao hawajui nini kinaendelea mpaka kuanza kuandika maneno ya karaha - kuwa na mke mzungu kunaingiaje hapa? Kwani Maggid kavunja sheria yeyote? Ameanza kwa kusema kwamba "...aonavyo yeye...". He, Maggid Mjengwa, like everybody else, is entitled to his own opinion!!!

Ifuatayo ni taarifa iliyoandikwa na journalist aliyopo Iringa pia - ukiisoma hii hutashangaa kwa nini mawazo na opinion ya Maggid imelenga kumlaumu Mchungaji Msigwa. For the record mimi pia namlaumu vikali sana Mchungaji Msigwa!!!

HABARI KAMILI – Imeandaliwa na Shaaban Mwinyikayoka, aliyeko Iringa

Takriban watu 30 wanashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani Iringa, kufuatia vurugu zilizozuka mapema asubuhi ya leo zikiwahusisha wafanyibiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga na askari hao.

Vurugu hizo, ambazo zimeelezwa kuwa na msukumo wa kisiasa zaidi, zimehusisha wamachinga ambao walikuwa wakitaka kufanya biashara zao katika eneo maarufu la Mashine tatu, huku eneo hilo likiwa lilishakatazwa kutumika kwa shughuli hiyo.

Hadi tunaenda mtamboni, hakukuwa na taarifa zozote za kuuawa kwa mtu yeyote ingawa majeruhi kadhaa walikuwa wanaelezwa kuwa walikuwa wamepelekwa hospitali kupatiwa matibabu.

CHANZO CHA VURUGU:
Vurugu za leo, zimetokana na mvutano wa muda mrefu sasa ambao kwa namna moja umeelezwa kuwa umekuwa ukichochewa sana na mbunge wa Iringa, Peter Msigwa, ambaye ametuhumiwa kuendekeza zaidi maslahi yake ya kisiasa, badala ya maendeleo.

Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo, miezi kadhaa iliyopita, madiwani kupitia kikao chao ambacho mbunge huyo ni mjumbe na alihudhuria, walikuwa wamekubaliana kuwa wamachinga hao watafutiwe sehemu nyingine kwa ajili ya kuendesha shughuli zao kila jumapili.

Chanzo cha kuhamishwa kwa wamachinga hao toka eneo la Mashine Tatu, kinaelezwa kuwa ni kutokana na ukweli eneo hilo lilikuwa linatakiwa kuachwa wazi kwa minajili ya kuwezesha ukarabati wa eneo hilo ambalo limekuwa korofi na hivyo kusababisha ucheleweshwaji wa ujenzi wa barabara ya Iringa Dodoma, mradi ambao umeshika kasi hivi sasa.

"Haya yalikuwa maamuzi ya Baraza la Madiwani, ambayo yaliwasilishwa kwa wamachinga hao na walikubali kuhamia eneo la Kitwilu, ambako walifanya biashara kwa majuma kadhaa, kabla ya kuanza kulalamikia ugumu wa biashara utokanao na kukosekana wateja na uduni wa miundombinu hasa ya kiafya" kimeeleza chanzo chetu kutoka eneo la tukio.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, baada ya hapo, wamachinga hao walikubaliwa kuhamishiwa sehemu ya Mlandege, ambayo iko kando kidogo ya mji. Huko walifanya biashara kwa muda na kukawa na ukimya hali ambayo iliashiria kuwa wameridhika na wangeendelea kufanya biashara zao huko.

Hata hivyo, katika hali ya kushangaza, inaelezwa kuwa katika moja ya mikutano yake, mbunge Msigwa, aliwaambia vijana hao kuwa warejee katika eneo la Mashine Tatu, kwakuwa yeye ni mbunge wao na kwamba halmashauri haikuwa na haki ya kuwafukuza mahali hapo.

"Hili ndilo linalolalamikiwa na wananchi na wanamtuhumu waziwazi mbunge kuwa amechangia sana machafuko ya leo. Yerye ni diwani kwa nafasi yake, anaingia vikao vya Baraza la Madiwani, anajua kile walichokuwa wameamua hapo awali, haieleweki imekuwaje tena akarejea na kuanza kuwatangazia wamachinga kurudi eneo ambalo awali walitakiwa kuondoka" amesema mwananchi mmoja aliyeongea na mwandishi wa habari hizi.

Kufuatia hatua hiyo, manispaa ililazimika kutoa tamko la kuwakataza wamachinga kurejea mahali hapo, hatua ambayo inaelezwa kuwa haikuweza pia kuafikiwa na mbunge, ambaye alirudia tena kuwataka wamachinga kurudi Mashine Tatu, kufanya biashara zao.

"Manispaa kwakuwa inajua kuwa ilishatoa tamko ambalo hata mbunge alihusika katika kuliandaa la kuwataka waondoke hapo, iliweka matangazo ya kuwakataza kufanya shughuli zao hapo, lakini pia kuweka ulinzi ili kudhihiti wale ambao wangekiuka agizo halali la kimamlaka, na walipokuja kufanya biashara leo, ndio ikawa kama hivi" ameeleza mwananchi mmoja toka eneo la tukio.

Mbunge amekamatwa?
Kwa mujibu wa taarifa ambazo zilikuwa bado hazijathibitishwa, mbunge Peter Msigwa, ambaye alikuwa akishiriki katika hafla ya kuchangia Harambee katika chuo kikuu cha Tumaini, alitembelea eneo la tukio hilo lakini ghafla akapotea tena kurejea Tumaini.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa, mbunge huyo alikuwa amejisalimisha kwa Jeshi la Polisi baada ya kuambiwa kuwa anatafutwa kufuatia kuhusika kwake kuchochea vurugu hizo.

Heshima kwako Kiongozi!

Kwanza naamini tangu siku ile ulipoitwa kuhojiwa kuhusu suala la Ugaidi na Ludovick umesha kuwa muoga na serikali hii. Vile vile ninaona hoja zako katika mabandiko mbali mbali zimekuwa za ki- muegemeo kwenye serikali.

Kiongozi! Nina hofu huenda ndio zile mbio za kuminywa uhuru wa habari zimekutembelea kwa kunyooshewa kidole, au?!

Kiongozi!

Hivi kweli inaingia akilini kusema kwamba Mh. Mch Msigwa awashauri machinga kutii amri ya kuto kufanya shughuli zao huku akijikita kwenye mazungumzo ya namna ya kuondokana na ufanyaji shughuli zao kwenye eneo la Mashine Tatu? Unataka kuniambia kwamba suala hili ni la jana au leo asubuhi? Mbona lina muda mrefu na hakuna suluhu yoyote iliyo patikana kupitia serikali kama si Halmashauri ya Iringa?

Kipi kinge stahili kuanza kati ya kutafuta eneo jipya la kufanyia shughuli za wamachinga kabla au kuwaondoa kwanza? Na wakiondoka kwanza kabla ya kujua hatima yao, je, kipato chao cha kila siku walicho kuwa wanakitegemea watakipatia wapi. Je, tegemezi wao ikiwa ni pamija na watoto wanao hitaji kugharimiwa shuleni watakuwa kwenye hali gani?
Ukizingatia kwamba hata hiyo serikali inayo wafukuza hao wamachinga,tayari ilisha wasusa watoto wetu huko mashuleni kwa kuambulia viwango vya Division 0.

Kwa serikali hii ambayo wakubwa wakivunja sheria wanaongezewa kama sio kupandishwa vyeo, ifike mahali kila tunacho dai, tukidai kwa nguvu maana wanyonge wanaonekana kukosa haki, huku wakubwa wakivunja sheria na kutunukiwa nishani na kuzidi kusifiwa.

Ukweli ndio utarudisha heshima ya nchi hii ambayo tayari imesha potea kwenye macho ya dunia ya leo.

KIONGOZI!

TUFIKE MAHALI KWA UMOJA WETU TUKIRI KWAMBA SERIKALI YETU IMEFIKIA KIWANGO CHA KUTO KUWAJALI WANANCHI WAKE. VIONGOZI WENYE MAAMUZI KATIKA NCHI HII WANAJALI MASLAHI YAO TU!!!!!

Pole kama nimekukwaza Kiongozi!
Kupanga ni kuchagua, unaruhusu umachinga au unajenga tabaka la vibaka. Na watakuja kula kwake wakati wanangoja uamuzi wa manispaa. Uamuzi kwanza vitendo baadaye sio?

Wewe kila jambo linalotokeaga huwa unatoa hicho unachokiitaga tathimini, wewe ni nani? usiwe unatupotezea muda tafadhali.

Wakati mwingine ni kazi sana kukuelewa maggid

Naamini kabisa, kuwa Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa angeweza kuepusha hali inayoendelea sasa kwa kuwasihi Wamachinga watii kwanza amri ya Manispaa, na yeye, kama Mbunge wao, kujiingiza kwenye mazungumzo ya dhati na wenzake kwenye Halamshauri ya Manispaa ya Iringa katika kutafuta ufumbuzi wa suala hili. Na hiyo ndio siasa. Siasa ina maana ya majidiliano endelevu badala ya kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu pale milango ya majadiliano ingali wazi.

Mchungaji Msigwa ni rafiki yangu, muda mfupi uliopita nimempigia simu. Imeita bila majibu. Mmoja wa watu wake wa karibu ameniambia yuko kwenye Harambee pale Tumaini University.

Sijui unamlaumu kwa lipi sasa

E84A4702.JPG

Last edited by a moderator:
I real miss my Town, poor ZeMarcopolo uses a lot of forces to distort my people but I have learned something that IT'S BETTER TO GROW PHYSICALLY BUT IT'S MORE BETTER TO GROW MENTALLY.
Tatizo ni njia tunazoamini suluhu ya tatizo polisi wanakosa mbinu kutuliza ghasia sio kila siku tutumie mabomu ya machozi,virungu n.k.
Sijaona sehemu ya msigwa kumuiga Lema sisi tulimchagua jinsi alivyo na tunamwamini akiwa kama Lema inawezekana asifiti matakwa ya wanairinga na nani kasema Lema ni bora kuliko msigwa?
tusijaji tu, kuwa mbunge under control ya CCM ni kazi.

Kwa tunaoujua mji wa Iringa, Mashine Tatu wanapofanyia biashara wenzetu wamachinga ni barabarani, ni sawa na kwa DSM wafanyie pale barabara ya UHURU karibu na round about ya kariakoo. Hapa cha msingi kama c cha sekondari kabisa, ni kutafutiwa sehemu mbadala na iwe inafikika kirahisi nawateja kabla ya kuwapiga stop. si kila jambo ni siasa wajameni. :sorry:

Majjid,ubarikiwe,hakika chadema shetani anawatumia kuliangamiza taifa,wewe unayejiita mchungaji hebu Nijibu ni lini Huyu Yesu unedai kumtumikia alikua akihamasisha umma kupinga utawala na kuleta machafuko,wewe ni ajenti wa kuzimu,unatimiza unabii mkuu wa Mungu wa siku za mwisho,wewe ni mtumishi wa dunia hii sio wa ulimwengu ujao,acha kutumia jina la Yesu kwa tumbo lako,shetani amewakamata mmeamua kuliangamiza taifa letu,na sisi hatutawaacha ,the current state of our dear nation is fast filling up its cup of iniquity throug CHADEMA,violence and crime of political gain are filling our nation,and Satan is using Mchungaji msigwa to torn apart this innocent Nation.

The youth who walk the streets are surrounded with handbills and noice of crime and sin,their mind are educated to misbehave and crime,hatred and sin against the government,ole wenu chadema mnaodhani Mungu anazibariki kazi hizi za Ibilisi.

Mungu lete utulivu watu Wako tumalize kazi,Yesu urudi kulichukua kanisa lako,Amen

mm nashauri tusiwaite CDM mashetani, hawa ni watz wenzetu, haya yanayotokea leo mbona mbunge alishashauri siku nyingi hadi bungeni kuwa utaratibu mzuri uandaliwe wapi wamachinga wakiondolewa watapelekwa. kuwa miundombinu iwekwe na ikibidi stendi za daladala zihamieshiwe wanakohamia kwani wateja wao wakubwa wanatumia usafiri wa daladala. ingetakiwa tupate taarifa je ushauri huu umefanyiwa kazi kiasi gani kabla ya kulaumu

tatizo kubwa huwa tunachelewa kuufanyia kazi ushauri hadi mambo mabay yatokee ndipo tunaanza kutafuta mtu wa kumlaumu. cheki matokeo ya form four, mbatia alishauri hoja yake ikapingwa na kufutwa lakini wiki moja baadaye yakatokea matokeo ambayo hayajawahi kutokea nchini, je hapa tumlaumu mbatia au wale waliokataa kujadili hoja yake na kutafuta ufumbuzi wa tatizo?

kwenye mambo ya msingi tusiangalie nani anasema na vyama tuviweke pembeni

Article hii ya Maggid imeniumiza sana kwani ni wazi ilikuwa na lengo la kumchafua mbunge Msigwa. Mbaya zaidi, mwandishi ameandika mambo mengi ya kumlaumu Mbunge bila ya kusikiliza hadithi kutoka kwa upande wa mchungaji. Ni lazima waandishi wa habari watambue ya kuwa maandishi yao yana uzito na wakati mwingine yanaweza kuharibu sifa za watu na hata kuathiri matokeo ya kesi.

Back
Top Bottom