Kilio na kicheko cha Michele

Milonji

Senior Member
May 26, 2022
153
494
Habari members wote.

Tumetangaziwa kuwa kuna watu/Kampuni binafsi wamepewa vibali vya kuagiza mchele tani 90,000. Agizo hili limekuwa ni Mwiba (Kilio) kwa upande Mmoja na Neema (Kicheko) kwa upande mwingine

KILIO
Agizo hili ni kilio kwa;

1. Wafanya biashara ambao walitegemea Mchele upande Bei wakati wa Mfungo ili wapate kujinufaisha.

2. Wakulima, ni kilio kwao kwa sababu Mchele huu ukiingia sokoni utashusha Bei ya kununulia Mchele ulio mashambani.

3. Madali, kama ilivyo kwa wafanyabiashara kwao pia ni Kilio.

KICHEKO
Wanufaika wakubwa wa Mchele huu ambao ni kicheko kwao ni Pamoja na;

1. Wananchi wa kawaida.

2. Waislam watakao kuwa kwenye Mfungo.

3. Wakristu watakao kuwa kwenye mfungo.

NB:
Serikali ingeruhusu pia Sukari, Mafuta na Unga.
 
Huo mchele ufike mapema kabla wa mashambani haujaanza kuvunwa mwezi march mwishoni .Kufika kwake mapema kutawasaidia wananchi kuanza kula wali ambao siku hizi kimekuwa chakula cha anasa kutokana na bei yake ambayo wengi wameshindwa kuimudu
 
Mama Samia ashaanza kuelewa nani anamtakia heri na yupi anamuombea afeli
Hili la mchele litaleta haueni kwa nchi
 
Ngoja mlishwe mchele wa plastic. Maana mnapenda sana vya dezo.
Humuwezi letewa mchele super kwa bei poa.
Wenye hela wataendelea kula mchele bora wa Kyela na Kamsamba
 
Habari members wote.

Tumetangaziwa kuwa kuna watu/Kampuni binafsi wamepewa vibali vya kuagiza mchele tani 90,000. Agizo hili limekuwa ni Mwiba (Kilio) kwa upande Mmoja na Neema (Kicheko) kwa upande mwingine

KILIO
Agizo hili ni kilio kwa;

1. Wafanya biashara ambao walitegemea Mchele upande Bei wakati wa Mfungo ili wapate kujinufaisha.

2. Wakulima, ni kilio kwao kwa sababu Mchele huu ukiingia sokoni utashusha Bei ya kununulia Mchele ulio mashambani.

3. Madali, kama ilivyo kwa wafanyabiashara kwao pia ni Kilio.

KICHEKO
Wanufaika wakubwa wa Mchele huu ambao ni kicheko kwao ni Pamoja na;

1. Wananchi wa kawaida.

2. Waislam watakao kuwa kwenye Mfungo.

3. Wakristu watakao kuwa kwenye mfungo.

NB:
Serikali ingeruhusu pia Sukari, Mafuta na Unga.
Nitanunua huu huu wa Tz hata huo unaokuja uuzwe 1,500/-.
 
Hivi hizi tikitaka zitaisha lini mliruhusu kwa vibali nafaka kuuzwa nje then kumetokea deficit mnaruhusu tena kununua kutoka nje.
 
Hivi huo mchele huko wananunua kwa bei gani na huku wanakuja kuuza kwa bei gani ?

Kama vipi Kwanini Hizo Tani 90 tusingechukua sisi kama nchi na kuwasaidia wakulima kuongeza production ili na sisi tuweze kuuzia nchi nyingi zaidi....
 
Back
Top Bottom