Kilio cha njaa! Dodoma na tanga-handeni

NGULI

JF-Expert Member
Mar 31, 2008
4,803
637
Jana vituo vya habari vikiwemo radio na televison wametangaza wananchi wa vijiji vya DODOMA wanakula UBUYU na wa Tanga hamna hata ubuyu wanakufa, na watoto wameeacha shule na ndoa zimevunjika wanaume wao wamekimbia kwenda kutafuta chakula na hawajarudi tena labda wengine mauti yamewakuta njiani. Serekali ichukue hatua za haraka na irudishe ule msaada wa ZIMBABWE wapatiwe hao wanachi wenzetu chakula wanaokufa.
 
Na serikali hiyohiyo inatangaza jana kuwa hakuna Mtanzania atakayekufa kwa njaa?

Kwa inji yetu bottom line ni watu kufa kwa njaa, ndipo seerikali ione kweli hali ni mbaya!

Poor Us!

Duh, nimekumbuka dola zangu nilizopeleka zimbabwe, balozi nirudishie niwafae wananchi wangu wasile ubuyu. Maisha bora kwa kila mtanzania????
 
Poleni sana ndugu zangu. Bila shaka wakuu wamesikia kilio na kuona kwenye luninga sasa mtapata misaada ya chakula.
 
Hipocrisy tu imewajaa viongozi wetu. Halafu tunasema maisha bora kwa kila mtanzania.
 
Kuna tani 1500 za nafaka lakini haijagawiwa kwa sababu hakuna mil.9 za kusambazia. Wala siyo fedha anazopat Mbunge kwa Mwezi. Hii yote inakuwa tabu kwa sababu wale wanaotakiwa kufanya kazi hiyo wanaona kuwa fedha ni kidogo hivyo hawatakuwa na 10% ya maana, there will be no big cut. Serikali inatakiwa ichukuwe maamuzi mara moja na PCCB wafanye uchunguzi wa ucheleweshaji huo kama un strings za rushwa ndani yake na ikibainika wahusika wachukuliwe hatua mara moja wawe mfano.
 
Firsr of all wananchi wenyewe ni wa kulaumiwa kwani kufa njaa na hujafungwa mikono wala miguu ni uzembe, second serekali haina mkakati wowote madhubuti kwa lolote la nchi hii,kama hata umeme karne hii ni tabu unatarajia nini?ujinga mtupu
 
Poleni sana ndugu zangu. Bila shaka wakuu wamesikia kilio na kuona kwenye luninga sasa mtapata misaada ya chakula.

baru unaongea point gan? inamaana wakuu hawajui mpaka vitangazwe kwenye vyombo vya habari? hii ni kutokuwajibika kwa viongozi husika katika eneo hilo. kuanzia mwenyekiti, katibu mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya mkurugenzi, na mpaka mbunge wao, wote hawana maana, kingine unawezaje kusema hakuna mtu ataekufa na njaa wakati wanaokufa wapo? mi nashangaa nchi hii kwakweli..ghaaa boring..nauwezo naingia msituni
 
Firsr of all wananchi wenyewe ni wa kulaumiwa kwani kufa njaa na hujafungwa mikono wala miguu ni uzembe, second serekali haina mkakati wowote madhubuti kwa lolote la nchi hii,kama hata umeme karne hii ni tabu unatarajia nini?ujinga mtupu
Hujafungwa mikono na miguu lakini mvua hazikunyesha na wakulima hawakupata mazao. Unataka watumie mikono na miguu waliyonayo kuteka watu na magari njiani? Unata wahame vijiji vyao? na wakihama wanakwenda wapi penye unafuu? Mjini kwenyewe kumejaa sana sasa hivi na pia ombaomba siku hizi hawapati sana, watu "wamefulie"
 
baru unaongea point gan? inamaana wakuu hawajui mpaka vitangazwe kwenye vyombo vya habari? hii ni kutokuwajibika kwa viongozi husika katika eneo hilo. kuanzia mwenyekiti, katibu mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya mkurugenzi, na mpaka mbunge wao, wote hawana maana, kingine unawezaje kusema hakuna mtu ataekufa na njaa wakati wanaokufa wapo? mi nashangaa nchi hii kwakweli..ghaaa boring..nauwezo naingia msituni
Walitangaza pia ni serikali kwani ni mkuu wa wilaya pamoja na mbunge wake.
 
Back
Top Bottom