Kilimo Kwanza: Tumethubutu, Tumewza, Tunasonga mbele!!

Laptop01

JF-Expert Member
Nov 29, 2009
1,365
796
Wana-JF tafadhali naombeni msaada wenu,

Hii kauli mbiu ya Serikali juu ya kilimo kwamba eti tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele mimi inanitatiza sana maana sijui tuethubutu lipi, tumeweza lipi kwenye kilimo ; na tunasonga mbele katika lipi lililojema katika kilimo. Hatuna zao lolote ambalo tunaongoza kwa kuuza nje ya nchi, kilimo bado ni cha jembe la mkono likisaidiwa kwa mbaaaaaaaali na jenereta iliyowekwa juu ya vyuma na kuitwa power tiller, matrekta yapo kwenye yard za maonesho katika maeneo mbalimbali ya Suma JKT, benki ya CRDB siyo ya watu wa Vijjiini tena!!

Sasa hii kauli mbiu inamaanisha nini kwa Mkulima wa Tanzania na watanzania kwa aujumla?
 
Aisee, niko kwenye maonesho ya 88 hapa Morogoro, maonesho yamedorora na kila mahali unaweza ona hiyo slogani. Kwa kweli mitaa ya town centre akina dada wamethubutu , wameweza na wanasonga mbele. Na hii baridi ya morogoro ndo usiseme.
 
ONYO: Usifikirie, kutenda na kuamua kama mbunge wa CCM
 
mapinduzi yatafanywa na Mtu mmoja mmoja, tusiisubiri hii serikali haijafanya, haitafanya. Nafahamu kuna wasomi wamewekeza kwenye kilimo and wanafanya vizuri sana, ilhali hawahudhurii haya maonyesho.

Now tuzungumze kwa mlengo tofauti, Now tusaidiane kwa wale waliofanikiwa kwa juhudi binafsi kuonyesha mwanga wale wanaotafuta means za kuwezesha shughuli zao za kilimo, else Tuwashinikize kufanya...........methodologies za kufanya mambo yatokee na si siasa kama zao hawa wafanya siasa.

Salaam
 
Hatujathubutu, hatujaweza na tunazidi kurudi nyuma,POLITICS IS POISONING OUR MIND, ukiona proposal zao katika karatasi kuhusu kilimo kwanza zimeng'aa na tunapata hope kibao ya kuvuna tani nyingi njoo kwenye uhalisia ni vituko na utani bado tunatumia BLANKET SOLUTIONS powertillers zimefanikiwa kuongeza uzalishaji wa mazao maeneo ya tambarare wakaamua walete na maeneo ya milima, wapi na wapi bwana?tumezoea kulima tumesimamia visigino powertiller ya nini?sh*****
 
Back
Top Bottom