Kilimo kwanza na makanjanja wa usambazji wa mbolea

haki na usawa

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
481
135
ANGALIA msambazaji wa mbolea hana hata ofisi lakini anapata tenda ya kusambaza mbolea!
Fedha za EPA ziliko TIB hakuna kitu zinaliwa kati ya msambazaji, viongozi wa wilaya, mabwana shamba na kidogo viongozi wale wa vijijini na si VIONGOZI kana kwamba haijulikani nini kinafanyika wanajua lakini nani wa kumfunga paka kengele
Nasema kama wanataka ukweli waite wachunguzi toka nje kwani PCCB yetu haina meno kukamata wakubwa angalia yanayototekea Rufiji je watamkamata nani? waje wafanye uchunguzi wajue je mbolea anayotakiwa kupewa mwananchi/mkulima kapata kweli?
Wanachofanya wanaenda wilayani wanaongea na mabwana shamba na wanahakikishiwa kupewa tenda wasambazaji wanapata fedha za bure na kuwapa kidogo viongozi wetu na tunasema kilimo kinakuwa!
Wanaongea na Viongozi wa vijiji na wanawadanganya kuwa kuna msaada wanaletewa wanaandikishwa na kuweka sahihi zao lakini wasambazi ndo wamesambaza mbolea tayari na wanaenda kuchukua chao
Je PCCB na Usalama wa Taifa haujui haya?
Au ndo kupozana kiaina?
Fanyeni uchunguzi wananchi wamesainishwa sana lakini hakuna kitu wanachopewa, hakuna cha mbolea wala mbegu?
Zaidi wanajua viongozi wa wilayani na matumaini yangu "KILIMO KWANZA HAKITASAIDIA KITU KWANI KIMEINGILIWANA VIRUSI" kama mna majina nendeni mkaulize nani alipewa mbegu kama si sahihi na majina yao tu walioandikishwa? JE HII HAIJULIKANI KWA WAKUBWA WETU ( VIONGOZI WA NCHI)
Kuendelea kuwafanyia wananchi usanii huu je ni vizuri?
Wasambaji wanachohitajika ni vyeti na si mtaji je TUTAFIKA KATIKA KILIMO KWANZA?
Usalama wa Taifa mlioko wilayani hamyaoni haya au na nyie bora liende? AU ATAJUA MWENYE NCHI NA WALANGUZI ANAOWATEUA KUWAMALIZA WANANCHI? kwa kuhitaji madole gumba yao tu na kuiba kilaini bila wafuatiliaji?
"HAKI ITENDEKE KUKOMESHA TABIA HII NA WOTE WALIOFANYA WACHUKULIWE SHERIA KALI ILI KUKOMESHA IKIWEMO KUFILISIWA MALI ZAO"
 
Back
Top Bottom