Kilichonikuta leo lodge

princewilly

JF-Expert Member
Nov 30, 2017
259
526
Leo baada ya kutoka katika mizunguko yangu nikasema ngoja niende nikamsalimie rafiki yangu yeye anafanya kazi katika lodge moja.

Nilivyomcheki akaniambia bado yuko kazini nimpitie mzee nikatimba hapo kwenye lodge anayofanyia kazi, tukiwa tumekaa pale reception tunapiga story mbili tatu akaja jamaa mmoja anataka room akaambiwa bei akalipa baada ya hapo akapiga simu huku akisema njoo hapa lodge nishalipia room nipo chumba na 112.

Kukaa kidogo mtu anayekuja kuingia kwenye chumba cha huyo jamaa ni mama yake na rafiki yangu. Kwanza yule mama hakutegemea kunikuta pale maana alishtuka balaa kutoka nje alishindwa na kuingia ndani nako ilikuwa shida na mimi bila kujivunga nikamwambia mama shikamoo akaitikia.

Ikabidi aniite nje akaniambia mwanangu naomba unifichie siri mwanangu nisiadhirike huku akitoa wekundu kadhaa akinipatia halafu akazama ndani huku akiniachia maswali huku nje

Sijui yule mama amekosa nini kwa mume wake
 
Back
Top Bottom