Kilichomuua ‘mtoto wa boksi’ chabainika; wahusika kunyongwa!

Mtoto amekufa kwa pumu (pneumonia) baada ya kufungiwa kwenye boksi na hao wendwazimu kwa miaka 4! Utasemaje kwamba hawajamuua wao? You can't be serious! Think BIG mkuu.

Hakuna nimonia ya miaka 4!!!! Huo ni uongo mkubwa sana.
 
Mimi sina imana kama amekufa.yule mlezi wa nasra pale muhimbili alikaririwa akisema na ninamnukuu..' Msinichukue mimi sitaki kwenda tena huko...' .hapa napata mawazo ya ushirikina zaidi.Wale wanaojinasibu kama wanatoa misukile mrudisheni nasra.

Huyu wa ukweli gwajima hawezi kumtoa,misukule yake ni ya dili.
 
sasa na yule baba mzaz ambaye mpaka mazishi amehudhuria vp???...hahusiki ..mbonayuko nje.kwa dhamana........

hili swali kawaulize poliCCM waliompa dhamana na kumrudisha mtaani aendelee kula bata na kuharibu ushahidi!
 
Angalau sasa unesema pneumonia japo nimonia is not chronic dzz,Lakini wengi tu wanalazwa na nimonia lakini hawafi nin kilijiri kwa nasra baada ya kupata chronic pneumonia?

hili nalo ni suala la kufuatilia. uzembe wa manesi na madaktari wa muhimbili pia utakuwa umechangia kifo cha mtoto nasra. ugonjwa wa kawaida kama pneumonia utaondoaje uhai wa mgonjwa aliyelazwa katika HOSPITALI YA TAIFA? itabidi madaktari nao wahojiwe kuhusu kifo hiki. mbona mafisadi hulazwa hapo muhimbili wakiwa na magonjwa ya kutisha lakini hawafi?
 
Huyu mtoto alikaa kwenye box miaka minne na hakufa!! Hebu madaktari watweleze kwani inasemekana ni kutokana na mabadiliko ya mazingira ya ghafla aliyopewa mtoto huyu akashindwa!

hiyo nayo ni sababu mwili wa binadamu ni kitu cha ajabu ndo maana kuna wengine wakitoka mkoa moja kwenda mwingine wanaweza umwa hata mafua au nozi kubadilika.... unaweza fikiria mwili wa huyo mtoto ulipata mabadiliko makubwa sana na mshtuko pia ndo maana akasepa aisee inaniuma sana
 
Cjui kama itakua hvo kama wauwaji wa arubino mpaka saiv uchunguz unaendelea hak dah hamna ktu
 
Hata kama kungekuwa na kitu nyuma ya pazia, sio kigezo cha kumtesa mtoto mdogo kihivyo. Watu wengine ni wakatili zaidi ya wanyama na wala hawastahili kuishi hapa duniani--ni wa kunyongwa mpaka kufa. Mijitu yenye akili za kinyama kama hii haina nafasi katika dunia hii--roho zao zinapaswa kuwa motoni tu! Hata kama ukiokota mtoto mdogo usiyemjua huwezi kumtesa namna hii--kumweka kwenye boksi na kumsababishia maradhi, ni zaidi ya ukatili. Hao MBWA wanyongwe hadharani ili liwe fundisho kwa matutusa mengine kama wao wanaowanyanyasa watoto.


Hujanielewa, sijasema kuna uhalali wowote wa kumtesa mtoto yeyote yule, tena adhabu wanastahili kubwa tu. Nilikuwa najaribu kufigureout kilichopelekea wao kumfanyia huyo mtoto ukatili ilihali ana ndugu zake akiwemo baba yake. Na huyo baba yake hovyo kabisa, miaka yote hiyo hajui mwanae anaishi vipi!!!? Bure kabisa.........
 
Duniani kuna watu wana roho mbaya ajabu!!Maskini mtoto mdogo, Malaika wa Mungu kateseka..inasikitisha sana
 
Niko pamoja na wote wanaopinga ukatili dhidi ya Binadamu especially innocent children,Inshala huyu mtoto Mungu atampokea na laana zote zitawashukia wahusika wa tukio ili.
Hata hivyo ukija kwenye upande wa sheria kesi hii ina utata mwingi sana na it may end up being Manslaughter,kwanza hao wakatili wamemuweka kwenye boksi na mateso yote kwa miaka minne hakufa,leo kachukuliwa na kupelekwa kunako huduma nzuri na tiba kafariki,je hao wazazi hawawezi kuwageuzia kibao waliomchukua kuwa ndio waliochangia kifo chake?hakuna murder ya causation,na ni ngumu sana ku-prove kuwa wakati wanamchukua alikuwa na pumu au hiyo pumu ili develop akiwa mikononi mwa rescuers,tuwe na analytical thinking.


Naona unawapa wauaji jinsi ya kujitetea vipi hili suala halijakukuzsa sana! yaani nina maana hujisikii uchungu aliopata huyo mtoto malaika?
 
Ninachoona mimi ni kua mungu alitaka kuwaumbua wanafiki hakutaka kumuuwa huyo mtoto kwenye mikono yao kiasi kwamba wangemzika bila watu kujua wangekimbia adhabu ya mateso walompa uyo mtoto kwa mda mrefu
 
Naona unawapa wauaji jinsi ya kujitetea vipi hili suala halijakukuzsa sana! yaani nina maana hujisikii uchungu aliopata huyo mtoto malaika?

ingekuwa mimi ndiye hakimu ninayesikiliza kesi hii isingemaliza hata mwezi 1 na ningehakikisha wahusika wote wanachezea kitanzi.
 
kumbe TZ sheria ya kunyongwa mpaka kufa ipo? km ndiyo hao waliohusika wanyongwe wakifariki miili yao icharangwecharangwe vipande vidogovidogo alafu viwekwe kwnye box theni vifukiwe ..ahsanteni nilikuwa sijui km sheria ya kunyongwa ipo hapa nchini kwetu
 
NIONAVYO:
Natoa wito kwa watanzania wenzangu kutoa taarifa polisi haraka pindi waonapo ukatili wowote dhidi ya wanyonge, hasa watoto wadogo, ili sheria ichukue mkondo wake. Tatizo la watanzania walio wengi ni kwamba hatujaliani. Unaweza ukamuona mzazi/mlezi akimtesa mtoto lakini ukakaa kimya. Kufanya hivyo ni kutomtendea haki yule kiumbe anayeonewa au kunyanayaswa. Tuweni na huruma kwa viumbe hawa wa mwenyezi Mungu wanaoonewa bila sababu za msingi huku wakiwa hawawezi kujitetea kwa namna yoyote ile. Tukio la mtoto Nasra, ambaye Mungu amemuita kwake, liwe fundisho kwa watu wengine wanaofumbia macho ukatili kwa watoto na wanyonge.

Nawasilisha.
:yield:
Inanikumbusha pia maelfu ya arbotions yanayofanyika!
 
Kufuatia kifo cha mtoto Nasra, almaarufu kama ‘mtoto wa boksi’, kuna kila dalili kwamba kifo chake kimetokana na maradhi aliyoyapata wakati akiwa anaishi kwenye boksi. Kwa kuwa imethibitika kwamba mtoto alifariki kutokana na ugonjwa wa pumu—kufuatia kufungiwa kwenye mazingira machafu, kutoogeshwa na kupigwa na baridi masaa 24, na kwa kuwa wahusika waliokuwa wakimfanyia ukatili huo tayari walishakamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kula njama za kumtesa mtoto huyo mdogo asiyekuwa na hatia na asiyeweza kujitetea, mawakili wanaosimamia kesi hii watabadilisha mashitaka ya kesi na kuwa KESI YA MAUAJI YA KUKUSUDIA.

Adhabu kwa mtu anayeua kwa kukusudia ni KUNYONGWA MPAKA KUFA. Kwa hiyo, wahusika wanasubiri kunyongwa hadi kufa pindi hukumu ya kesi hii itakapotoka. Na kwa kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani hawa wanadamu wasokuwa na haya, wajiandae kupokea kitanzi ili liwe fundisho kwa washenzy wengine wenye tabia za kinyama kawa hawa wendawazimu.

NIONAVYO:
Natoa wito kwa watanzania wenzangu kutoa taarifa polisi haraka pindi waonapo ukatili wowote dhidi ya wanyonge, hasa watoto wadogo, ili sheria ichukue mkondo wake. Tatizo la watanzania walio wengi ni kwamba hatujaliani.
Unaweza ukamuona mzazi/mlezi akimtesa mtoto lakini ukakaa kimya. Kufanya hivyo ni kutomtendea haki yule kiumbe anayeonewa au kunyanayaswa. Tuweni na huruma kwa viumbe hawa wa mwenyezi Mungu wanaoonewa bila sababu za msingi huku wakiwa hawawezi kujitetea kwa namna yoyote ile. Tukio la mtoto Nasra, ambaye Mungu amemuita kwake, liwe fundisho kwa watu wengine wanaofumbia macho ukatili kwa watoto na wanyonge.

Nawasilisha.
:yield:
"Law is all about arguments", let us wait and see(am not on their side any way)
 
Kwani hoa wazazi wenyewe wanajiteteaje? Wanasema kwa nini walimweka mwana wao mpendwa kwenye boksi?
 
Enyi watanzania wenzangu!!!! tushirikiane kutokomeza ukatili Kama alofanyiwa Nasra ...na sio huo tu, bali hata hayawani Kama yule wa Dar alokua anamlazimisha house girl kumstalehesha mbwa wake...wote hawa tuwafichue ili jamii ipate kutulia......
NB: MICHEPUKO INAFAA ILI KUKWEPA FOLENI NJIA KUU........
 
Kwani hoa wazazi wenyewe
wanajiteteaje? Wanasema kwa nini walimweka mwana wao mpendwa kwenye
boksi?

walilitumia box kama baby walker, hawakuwa na fedha za kununua za dukani ambazo huuzwa ghali na hazidumu.
 
Back
Top Bottom