Kilichoikuta kamati iliyoundwa kuchunguza kifo cha mwandishi iringa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
.

Posted: 14th September 2012 by MillardAyo in News

3


Marehemu Daudi Mwangosi.


Ikiwa ni siku moja tu baada ya kufikishwa Mahakamani kwa askari polisi anaetuhumiwa kwa mauaji ya mwandishi wa habari Iringa Daudi Mwangosi, Kamanda wa polisi Iringa Michael Kamuhanda amethibitisha kutokea kwa wizi uliofanywa kwa kamati iliyoundwa kuchunguza kifo hicho.


Namnukuu akisema "ni kweli wamefanyiwa uhalifu hotelini kwao wakiwa hawapo, imeibwa Ipad pamoja na shilingi laki tisa, bado tunamtafuta mwizi ambae bado hajajulikana"


Juzi September 12 ndio askari anaetuhumiwa kusababisha kifo cha Mwangosi alifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na baadae kurudishwa mahabusu.


Imekua ngumu kuwapata wahusika lakini millardayo.com inaendelea kuwatafuta ili kujua mazingira ya wizi na kama kuna ushahidi wowote uliopotea pamoja na mambo mengine, endelea tu kupita millardayo.com


 
Kawatafuta polisi waliowasusa au kamati inayowachunguza wahalifu?
 
RPC Kamuhanda ndiye mtuhumiwa nambari one.. kwa sababu hiyo ni lazima afanye mazingaombwe ili kwa namna yoyote ile afiche ukweli.
 
Tukumbuke kilichompata yule askari aliyewakamata wenzake walioiba shaba pale bandarini, hivyo ninaweza kusema ni kazi ngumu kuwachunguza askari!
 
yaani kamanda michael kamuhandaa hajakamtwa hadi leo hii wakati yeye aliruhusu mauaji hayo yatokee mbele yake.

mlinda usalama wa raia namba wani wa IRINGA, Leo anasimamia mauaji ya Raia asiye na hatia kinyume na maadili ya

kazi yake hajafikishwa mahakamani why why why ??? raia wa kawaida wakipigana mbele yako na mmoja kufa huku ukia

ngalia bila kuchukua hatua yoyote ni lazima utachukuliwa hatua kwani ulikuwa na uwezo wa kuwatengenisha au kutoa

taarifa kwa wahusika kuzuia uhalifu huo. Leo RPC tena na jeshi analo mbele yake na silaha anashindwa kuzuia mauaji ya

raia asiye na hatia achukuliwi hatua jamani nchi hii tunaelekea wapi??
 
Yote haya ni usanii!.. Utamchunguzaje muuaji wakati wote waliohusika kupanga mauaji hayo wapo ofisini? Bila kujiuzulu au kuondolewa ofisini hawa wafuatao: Waziri Nchimbi, RC, RCO, RPC, DC, DCO, OCD, na wale askari nane walioshiriki kupiga na kuua chochote kinachofanyika ni usanii tu!.. Hata wizi huu si rahisi kufanywa na raia. Ni wao wenyewe wanapiga usanii. Hata kesi yenyewe itakuwa ni usanii tu!.. HAKUNA KUU!..
 
Yote haya ni usanii!.. Utamchunguzaje muuaji wakati wote waliohusika kupanga mauaji hayo wapo ofisini? Bila kujiuzulu au kuondolewa ofisini hawa wafuatao: Waziri Nchimbi, RC, RCO, RPC, DC, DCO, OCD, na wale askari nane walioshiriki kupiga na kuua chochote kinachofanyika ni usanii tu!.. Hata wizi huu si rahisi kufanywa na raia. Ni wao wenyewe wanapiga usanii. Hata kesi yenyewe itakuwa ni usanii tu!.. HAKUNA KUU!..
POLISI ni idara ya Uhasama wa raia and not usalama wa raia,polisi jamii will never work
 
Back
Top Bottom