Kili waja na tangazo lipya

Soulbrother

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
405
14
Bia ya Kili ilizindua tangazo lake lipya wikendi hii, shooti ikianza pale Trinity bar na mnaji moja

Tangazo hilo wanaloliita “Fikisha Tanzania Katika Hatua ya Juu Zaidi” linafanyika katika mikoa minne Tanzania na linahusisha ubebaji wa bendera ya Tanzania kutoka Dar hadi kilele cha mlima Kili. Sources wanasema wabebaji watakimbia "from Dar to the Peak of Kilimanjaro Mountain"

Nasikia kuwa tangazo hili litakuwa na majina makubwa katika riadha kama vile Samwel Mwera,Simon Marwa na Wilbrod Gidaya pamoja na wanamuziki mbali mbali na litakuwa tangazo bomba kuliko yote.

Nawatafutieni picha

Watch this space for more!
 
So what? Tuanshabikia pombe tu wakati nchi inadidimia matangazo mangapi yanayobariki pombe kila kona leo hii mtoto anayekuwa anajifunza nini? Na makaburu wametupata kweli.
 
So what? Tuanshabikia pombe tu wakati nchi inadidimia matangazo mangapi yanayobariki pombe kila kona leo hii mtoto anayekuwa anajifunza nini? Na makaburu wametupata kweli.

Nguli,

Kazi na dawa bana!ha!ha!aaa
 
TBL mna kazi kubwa sana kwa hali inavyobadilika Tanzania.

Kwanza kila mtu anafahamu kuwa ni Makaburu. Itabidi kuibadili hii sura. Pia kama wapinzani wenu wakinunuliwa na Diageo basi mfahamu kuwa hawa wazee wa John Walker nao ni Wazito sana duniani.

Kama wenzenu wamechukua timu ya Taifa ya mpira wa miguu, basi ningelishauri mfanye kitu kama Kujenga shule/kambi ya wanariadha. Maeneo kama Arusha au Morogoro kwenye Milima ni sehemu safi sana. Ila Arusha ni BOMBA na hasa Mbulu maana huko pia kuna wakimbiaji wengi sana natural. Kama mkiweza kutengeneza wakimbiaji kama 10 na wawe wanakuja na medali kwenye mashindano makubwa makubwa, basi hakutakuwa na Tangazo zuri kama hili.

Hii kukimbiza bendera hadi Kilimanjaro wala HAIUZIKI. Hamuoni siku Taifa Star wakishinda mechi? Na amini kuwa siku ikatokea Mtanzania kaleta medali kutoka mashindano makubwa duniani, basi JINA lenu litajitangaza lenyewe. Hii ndiyo inaitwa LONG PLAN na si hizo SHORT PLAN.

Kama mtaendelea kuwa na meneja wa utangazaji anayefikiri namna hiyo basi mwafa.
 
Bia ya Kili ilizindua tangazo lake lipya wikendi hii, shooti ikianza pale Trinity bar na mnaji moja

Tangazo hilo wanaloliita “Fikisha Tanzania Katika Hatua ya Juu Zaidi” linafanyika katika mikoa minne Tanzania na linahusisha ubebaji wa bendera ya Tanzania kutoka Dar hadi kilele cha mlima Kili. Sources wanasema wabebaji watakimbia "from Dar to the Peak of Kilimanjaro Mountain"

Nasikia kuwa tangazo hili litakuwa na majina makubwa katika riadha kama vile Samwel Mwera,Simon Marwa na Wilbrod Gidaya pamoja na wanamuziki mbali mbali na litakuwa tangazo bomba kuliko yote.

Nawatafutieni picha

Watch this space for more!

then wakishafikisha ml kilimanjaro kinafuata kitu gani?wanapombeka na kuparty?nchi hii bwana eti makampuni ya kulewesha(breweries), kuchunana(simu), kuiba/wezi(migodi) ndo yanaongoza kwa fwedha!!duh
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom