Kila kitu kwa msaada wa watu wa marekani hatuchoki???

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
Mmh
jamani yaani mpaka basi ukisikia net,msaada wa marekani.bajeti msaada wa marekani yaani kila kitu kwa msaada wawatu wa marekani hii kitu inaisha lini mkuu wetu ??tumechoka na hao wamarekani ni binadamu wanamuda watachoka na hii kutoa misaada embu tujiangalie kidogo turudi kwenye matumizi je haya matumizi kama ya safari za nje atuwezi kusaidia kununua machandarua jamani tukapunguza hii li neno msaada wa watu wa marekani....???
 
Kupokea na kuomba misaada ndio wanasiasa wetu wanachopenda.......ndio ajenda yao kuu! Hawafikirii mbadala wowote zaidi ya kupata misaada. Hata uwezo wao wa kujenga hoja haupo umeelemea kwenye misaada! Jaribu kuangalia suala la OIC kwa mfano, hoja kubwa wanasiasa watakueleza eti tutapata misaada, yaaani hawafikirii nje ya boksi la misaada!

Tuite misaada nayo janga la kitaifa (limeharibu fikra za wanasiasa nchini kwetu)
 
Back
Top Bottom