Kila aliyeelekezewa kidole na CAG asibakizwe ofisini

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,882
35,899
Tuna nchi nzuri yenye fursa nyingi iliyogeuzwa kuwa mali binafsi ya wachache wenye kufahanika kwa kutokushiba kwao.

Maisha yamekuwa magumu. Mzigo wa kodi na tozo umekuwa usiomithilika. Wakati serikali yenyewe ikiwa imelenga makusanyo tu, bila kujali kuvuja kwa mifuko yake wala kama wananchi wake wanamudu hata zile gharama msingi tu za maisha. Ni gharama za vyakula, elimu, afya nk? Ni umaskini? Hayo siyo kipaumbele cha serikali tena.

Fika kwenye mahospitali kuona pesa za NHIF zinavyopigwa. Gharama za tiba zilivyowekwa kuwa za juu pasipo kuwa na uhalisia wowote.

FtP5ui9WwAAcX6v.jpg

Ona wizi wa dawa unavyoendelea. Tambua kumbe maduka karibu yote ya ndani au kuzizunguka hospitali hizi ni mali binafsi za vigogo hawa hawa. Ona wananchi wa kawaida kupata huduma ilivyogeuka kuwa ni kwa kudra za mwenyezi Mungu. Ona rushwa ilivyotamalaki, kujuana, kubambikiziana gharama za tiba nk kulivyoota mizizi.

Kwani hata ni sekta ipi basi imenusurika kutoka kwenye mlolongo huu wa kero za rushwa kubambikiziana mambo malengo yakiwa kukusanya mapato haramu au halali kupitia faini au taratibu na sheria za kijanja janja zinazozaliwa kila siku? Ni polisi, takukuru, uhamiaji, TRA, LATRA, Tanroads, Tanesco, mahakamani nk.

Screenshot_20230411-050644.jpg

Kumbe kwa watendaji wa serikali, wananchi hawana chao. Rasmi na bila aibu watendaji wamewageuza mradi wao. Kodi wanazokamuliwa zinakwenda kuwaneemesha wachache. Haya yakiendelea wao wakitucheza shere kuwa hazina iko mikono salama.

Kwamba hapa chini ni pesa anazoona CAG kuwa tumepigwa?

1. Wizara ya Afya - Tsh. Bilioni 91
2. Wizara ya Elimu - Tsh. ilioni 33.5
3. Wizara ya Maji - Tsh. Bilioni 82.8
4. Wizara ya Maliasili na Utalii - Tsh. Bilioni 1.2
5. Hifadhi ya Jamii (TASAF) - Tsh. Bilioni 1.5
6. Wizara ya Maendeleo ya Jamii - Tsh. Milioni 141.
7. Bado bungeni kuliko na wabunge hewa.
8. Bado TAMISEMI kwenye halmashauri huko.
9. Bado madhirika ya umma.
10. Nk.

Hii haikubaliki.

Kuwaita wezi hawa stupid au kuwataka wote waliohusika kuachia ngazi wenyewe tu, haitoshi. Hawa ni wa kufurusha unceremoniously watake wasitake. Hawa ni WA kutiwa adabu na kulazimishwa kurejesha pesa zote walizofuja. Hawa makazi yao ya kudumu yanapaswa kuwa magereza siyo katika ofisi za umma kazi wizi wao ukiendelea.

Kwamba watupishe? Hawa wasiokiwa na mishipa ya aibu? Nani kasema? Ni wazi kuwa hawataondoka wenyewe eti kwa kutuonea huruma tu.

Serikali siyo mali ya mtu binafsi. Ni vyema mkuu wake akajitenga na wabadhirifu hawa wanaofahamika kwa majina. Akawachukulia hatua stahiki zenye kuonekana na bila ya kuwaangaliana usoni. Wenye nchi tunaangalia na hatutakaa kimya na hasa kama hatua za kuridhisha hazitachukuliwa kama ilivyozoeleka.

Waisijaribu kutu beep. Wanatoka wezi hawa sasa. La sivyo matumizi yetu ya nguvu ya umma yatakuwa ni haki yetu na kwa namna tutakavyoona inafaa.

Hili halina vyama, ni la wananchi na haliwezi kuwa na mswalia mtume.
 
Maisha yamekuwa magumu. Mzigo wa kodi na tozo umekuwa usiomithilika. Wakati serikali yenyewe ikiwa imelenga makusanyo tu, bila kujali kuvuja...
Naunga mkono hoja ila sio kila alietajwa bali kila aliyehusika na ubadhirifu hata kama hajatajwa na ripoti ya CAG.

Ma KM ndio maafisa masuhuli wa Wizara zote, kama unakumbuka ile issue ya Wizara ya Maliasili, Waziri ana m bypass KM na kutapanya pesa, KM akaingia kugoma kuidhinisha, Waziri anamshitaki kwa rais kwa kumkwamisha!. Rais naye badala ya kumtaka Waziri afuate taratibu za matumizi ya fedha za umma, anawalazimisha lazima wapatane vinginevyo atawatumbua wote!. Kwenye ripoti ya CAG atakayetajwa ni Ofisa Masuhuli na sio waziri.

Kwa mfano kuna taarifa za enzi fulani Tanroad ma RM wa mikoa yote waliwajibika kupeleka kiasi fulani kwa Boss monthly!. Ripoti ya CAG itawataja ma RM na sio boss!.

Mfano mzuri ni ule ubadhirifu wa Rada ya BAE na Gulfstream, aliyetajwa ni mtu mmoja tuu, agent Vithlani, BAE wakakiri kurejesha kickbacks ila wakagoma ku disclose hiyo kickbacks wamemrejeshea nani!, hivyo wako tayari kupigwa faini ya non disclosure kuliko kuwataja, jee wangetajwa unadhani wanene wangesalimika?.

Hata Mama ni ugeni tuu, ndio maana hajui kunyamaza!.

Tozo ya Simbion ilikuwa US $ 350 millions!, Mwamba akagoma kulipa!. Tukakaa mezani tukanegotiate out of court tukakafikia makubaliano ma mdai kakubali kulipwa half US $ 175 millions. Jamaa akachomoka kabla hajalipa. Mama kaingia zikalipwa US $ 386 millions fasta fasta kimya kimya na hili kwenye ripoti ya CAG is missing!. Why ?, ni kwasababu mara baada ya malipo ukafuatia wema wa mlipwa kumfadhili mtu kwenye jambo lake lenye maslahi makubwa kwa taifa na taifa zima linashangilia!.

Yaani ametokea mfadhili kubwa la mafisadi amemfadhili Mtakatifu wetu na pale patakatifu petu, kisha sisi Watanzania kwa umoja wetu tunashangilia bila hata kumjua huyo mfadhili ni nani, ametumia kiasi gani, and what's is the motives behind ufadhili huo!. Huu kama sio uzuzu ni nini?!.
P
 
Naunga mkono hoja ila sio kila alietajwa bali kila aliyehisika na ubadhirifu!.

Naona umerejea ku edit bandiko lako na kuongeza hoja zingine mpya.

Ninakazia:

Screenshot_20230411-050644.jpg

Kama hao mamlaka ya uteuzi itapenda kuwafumbia macho, hao watakuwa ni halali yetu kama wananchi.

Kwan wewei ungependa kina nani hapo walindwe ikibidi kinyemela ndugu?
 
Umeonesha vizuri hili jambo lilivyo pana bahati mbaya linashughulikiwa kwa kudokoa kijisehemu fulani tu, ajabu wengi wanashangilia udokoaji huo kwa kigezo cha "sheria na taratibu" kufuatwa..

Pale hakuna kilichofanyika, kwangu alichofanya ametuonesha kwa vitendo alivyo mvivu wa kushughulika na kila kero inayotokea kwenye serikali yake.

Hapa hata wasaidizi wake nao wasiangushiwe lawama wanamshauri vibaya, ukweli kama hawezi kujiongeza kuendana na kila changamoto zinazotokea kwenye ofisi yake, huyu hatufai wala hatutoshi, tusidanganyane.

Wakati mwenzake alituambia halali anapekua mafaili mpaka usiku wa manane yeye alikuwa anauchapa usingizi, bahati mbaya ameendelea kuuchapa usingizi hata baada ya kukalia kiti, ni wakati wake aamke sasa, ukweli tunapigwa sana, tofauti na hatua chache na nyepesi anazochukua.
 
Naunga mkono hoja ila sio kila alietajwa bali kila aliyehisika na ubadhirifu!.

Ma KM ndio maafisa masuhuli wa Wizara zote, kama unakumbuka ile issue ya Wizara ya Maliasili, Waziri ana m bypass KM na kutapanya pesa, KM akaingia kugoma kuidhinisha, Waziri anamshitaki kwa rais kwa kumkwamisha!. Rais naye badala ya kumtaka Waziri afuate taratibu za matumizi ya fedha za umma, anawalazimisha lazima wapatane vinginevyo atawatumbua wote!. Kwenye ripoti ya CAG atakayetajwa ni Ofisa Masuhuli na sio waziri.
P
cc: Dr Kigwangalla
 
Kwan wewei ungependa kina nani hapo walindwe ikibidi kinyemela ndugu?
Mimi ni mpenda haki, na hata siku mkisikia nimeitwa, mnililie kwa kunimisi tuu, ila nakwenda straight peponi kutokana na utetezi wa haki!, ile dhambi yangu Kuu ya kuivunja ile amri repeatedly, nitaiungama kabla roho haikaacha mwili.

Mimi ningeanza na CAG mwenyewe kumuuliza mbona issue hii
Tozo ya Simbion ilikuwa US $ 350 millions!, Mwamba akagoma kulipa!. Tukakaa mezani tukanegotiate out of court tukakafikia makubaliano ma mdai kakubali kulipwa half US $ 175 millions. Jamaa akachomoka kabla hajalipa. Mama kaingia zikalipwa US $ 386 millions fasta fasta kimya kimya na hili kwenye ripoti ya CAG is missing!. Why ?, ni kwasababu mara baada ya malipo ukafuatia wema wa mlipwa kumfadhili mtu kwenye jambo lake lenye maslahi makubwa kwa taifa na taifa zima linashangilia!.

Yaani ametokea mfadhili kubwa la mafisadi amemfadhili Mtakatifu wetu na pale patakatifu petu, kisha sisi Watanzania kwa umoja wetu tunashangilia bila hata kumjua huyo mfadhili ni nani, ametumia kiasi gani, and what's is the motives behind ufadhili huo!. Huu kama sio uzuzu ni nini?!.
P
Haipo?.
Baba wa Taifa alisema "Ikulu ni mahali patakatifu". Haiwezekani akajitokeza mtu kumfadhili Mtakatifu wetu wa patakatifu petu bila maximum transparency kumjua ni nani, ametufadhili kwa kiasi gani na lengo la ufadhili huo ni nini na ulipatikanaje?.

Mimi sio mtetezi wa mafisadi bali ni mtetezi wa haki, nisichotaka ni double standards ndio maana hata Sabaya nilimtetea https://www.jamiiforums.com/threads...ing-au-tuiachie-karma-iwashughulikie.1878302/
P
 
Naunga mkono hoja ila sio kila alietajwa bali kila aliyehusika na ubadhirifu hata kama hajatajwa na ripoti ya CAG.

Ma KM ndio maafisa masuhuli wa Wizara zote, kama unakumbuka ile issue ya Wizara ya Maliasili, Waziri ana m bypass KM na kutapanya pesa, KM akaingia kugoma kuidhinisha, Waziri anamshitaki kwa rais kwa kumkwamisha!. Rais naye badala ya kumtaka Waziri afuate taratibu za matumizi ya fedha za umma, anawalazimisha lazima wapatane vinginevyo atawatumbua wote!. Kwenye ripoti ya CAG atakayetajwa ni Ofisa Masuhuli na sio waziri.

Kwa mfano kuna taarifa za enzi fulani Tanroad ma RM wa mikoa yote waliwajibika kupeleka kiasi fulani kwa Boss monthly!. Ripoti ya CAG itawataja ma RM na sio boss!.

Mfano mzuri ni ule ubadhirifu wa Rada ya BAE na Gulfstream, aliyetajwa ni mtu mmoja tuu, agent Vithlani, BAE wakakiri kurejesha kickbacks ila wakagoma ku disclose hiyo kickbacks wamemrejeshea nani!, hivyo wako tayari kupigwa faini ya non disclosure kuliko kuwataja, jee wangetajwa unadhani wanene wangesalimika?.

Hata Mama ni ugeni tuu, ndio maana hajui kunyamaza!.

Tozo ya Simbion ilikuwa US $ 350 millions!, Mwamba akagoma kulipa!. Tukakaa mezani tukanegotiate out of court tukakafikia makubaliano ma mdai kakubali kulipwa half US $ 175 millions. Jamaa akachomoka kabla hajalipa. Mama kaingia zikalipwa US $ 386 millions fasta fasta kimya kimya na hili kwenye ripoti ya CAG is missing!. Why ?, ni kwasababu mara baada ya malipo ukafuatia wema wa mlipwa kumfadhili mtu kwenye jambo lake lenye maslahi makubwa kwa taifa na taifa zima linashangilia!.

Yaani ametokea mfadhili kubwa la mafisadi amemfadhili Mtakatifu wetu na pale patakatifu petu, kisha sisi Watanzania kwa umoja wetu tunashangilia bila hata kumjua huyo mfadhili ni nani, ametumia kiasi gani, and what's is the motives behind ufadhili huo!. Huu kama sio uzuzu ni nini?!.
P

Bwana Pascal Mayalla hii style Yako ya kurejea ku edit posts zako kila iliyokuwapo inaitwa je kitalaamu?

"Au ndiyo Ile cynicism inayozaa tashwishi hasi mkuu?"

Kwamba kila majibu yanayotolewa wewe unarejea ki mugongo mugongo unaedit bandiko lako la awali ukiweka facts mpya, wakati mheshimiwa Tiganga alishamaliza kazi?

Nikurejee kwenye bandiko lako kama linavyosomeka sasa.

Ama kwa hakika kama ilivyo kwenye mada masharti na vigezo vyote vimezingatiwa:

Screenshot_20230411-050644.jpg

Mada hii haikuelekezwa kwa matarishi. Hii imeelekezwa kwa farasi mwenyewe.

ZQz7bQRc.jpeg

Muda wa kuchezana shere umepita na haupo tena. Kama hajayaona au kujifunza wa Ruto asidhani yeye hayamhusu.

Hapa tunasema naye mwenyewe kwa staha. Kama hataki kusikia, sauti ya watu isiyoshindwa kusikika inajulikana:

Yetu macho. Ngoja tuone.
 
Mimi ni mpenda haki, na hata siku mkisikia nimeitwa, mnililie kwa kunimisi tuu, ila nakwenda straight peponi kutokana na utetezi wa haki!, ile dhambi yangu Kuu ya kuivunja ile amri repeatedly, nitaiungama kabla roho haikaacha mwili.

Mimi ningeanza na CAG mwenyewe kumuuliza mbona issue hii

Haipo?.
Baba wa Taifa alisema "Ikulu ni mahali patakatifu". Haiwezekani akajitokeza mtu kumfadhili Mtakatifu wetu wa patakatifu petu bila maximum transparency kumjua ni nani, ametufadhili kwa kiasi gani na lengo la ufadhili huo ni nini na ulipatikanaje?.

Mimi sio mtetezi wa mafisadi bali ni mtetezi wa haki, nisichotaka ni double standards ndio maana hata Sabaya nilimtetea https://www.jamiiforums.com/threads...ing-au-tuiachie-karma-iwashughulikie.1878302/
P

Ni jambo la kheri kuwa hatimaye tunapiga hatua. Hii ya kurejea posts za nyuma zilizokwisha kujibiwa inaondoa flow nzuri ya mjadala.

"Itabidi kupendekeza Kwa Mod Ili mtu asiweze ku-edit tena post yake baada ya kuwa imejibiwa."

Ni jambo la msingi kumjua mbaya wetu na kukomaa naye huyo huyo Hadi kieleweke.

"CAG anapaswa kuwa huru na mwenye kuwajibika kwetu. Hapa ndipo umuhimu wa katiba mpya sasa unapozidi kujidhihirisha."

"Stupid" hawawezi kuwa wezi na matarishi wao tu. Wigo lazima uwafikie wote wanaohusika. Wanaowalinda, kuwafadhili na kuwatunuku vyeo hawawezi kupewa nafasi ya kutuponyoka. Haiwezi kuwa wa kubembelezwa kutupisha. Hao ni wa kuliwa vichwa pasipo na kuchelewa.

Tuungane sote kuwakemea mabaradhuli na kuhitaji adhabu kamili dhidi ya watu hawa na bila ya kuwaangalia usoni!

Anawashufhulikia wezi hawa sasa na bila kuchelewa, vinginevyo huyu ni wetu tena kwa namna inayotufaa sisi.

"Maendeleo hayana chama."
 
Umeonesha vizuri hili jambo lilivyo pana bahati mbaya linashughulikiwa kwa kudokoa kijisehemu fulani tu, ajabu wengi wanashangilia udokoaji huo kwa kigezo cha "sheria na taratibu" kufuatwa..

Pale hakuna kilichofanyika, kwangu alichofanya ametuonesha kwa vitendo alivyo mvivu wa kushughulika na kila kero inayotokea kwenye serikali yake.

Hapa hata wasaidizi wake nao wasiangushiwe lawama wanamshauri vibaya, ukweli kama hawezi kujiongeza kuendana na kila changamoto zinazotokea kwenye ofisi yake, huyu hatufai wala hatutoshi, tusidanganyane.

Wakati mwenzake alituambia halali anapekua mafaili mpaka usiku wa manane yeye alikuwa anauchapa usingizi, bahati mbaya ameendelea kuuchapa usingizi hata baada ya kukalia kiti, ni wakati wake aamke sasa, ukweli tunapigwa sana, tofauti na hatua chache na nyepesi anazochukua.

Inasikitisha kuwa focus inajaribu kupotoshwa tena kwa makusudi. Hili ni jambo la wizi wa wazi na mhusika ni serikali.

Zinatakikana hatua thabiti dhidi ya wezi wetu wote, tena bila ya kuchelewa.

FtW3UH_XgAEeb1R.jpeg

Wanasiasa wasitupoteze maboya hata kama wana maslahi au uswahiba wao usiotuhusu:

FsvJmEPXwAAxTEG.jpeg

Nchi yetu ni muhimu zaidi kuliko uswahiba wao hata kama ni wa chanda na pete:

FtX8OZvXoAs3PLI.jpeg
 
Naunga mkono hoja ila sio kila alietajwa bali kila aliyehusika na ubadhirifu hata kama hajatajwa na ripoti ya CAG.

Ma KM ndio maafisa masuhuli wa Wizara zote, kama unakumbuka ile issue ya Wizara ya Maliasili, Waziri ana m bypass KM .
P
Ndugu Pascal nimekosa la kusema, kama hali ndo hii ni lini nchi yetu itastawi na kuwa taifa lenye nguvu kiuchumi Afrika na Kimataifa?
 
Inasikitisha kuwa focus inajaribu kupotoshwa tena kwa makusudi. Hili ni jambo la wizi wa wazi na mhusika ni serikali.

Zinatakikana hatua thabiti dhidi ya wezi wetu wote, tena bila ya kuchelewa.

View attachment 2584027

Wanasiasa wasitupoteze maboya hata kama wana maslahi au uswahiba wao usiotuhusu:

View attachment 2584028

Nchi yetu ni muhimu zaidi kuliko uswahiba wao hata kama ni wa chanda na pete:

View attachment 2584031
Wanatuona wajinga wanadokoa dokoa tu wanapopenda wao, nasi kwa ujinga wetu "tunaridhishwa" na hatua wanazochukua.
 
Ufisadi ni ugonjwa ndugu unaoitafuna Afrika, licha ya utajiri wa kila aina ya rasilimali tulizonazo lkn Afrika ni maskini wa kutupwa, na bado wapo vijana Kwa wazee wanashangilia ufisadi huu, na maisha Yao ni hoehae bin taabani, Je nini tatizo la ngozi nyeusi?
 
Uswahiba wao hata kama ni kwenye maridhiano tusiyoyajua au mabango tusiyoyatambua ni vyema wakajua wanatukera.
 
Ufisadi ni ugonjwa ndugu unaoitafuna Afrika, licha ya utajiri wa kila aina ya rasilimali tulizonazo lkn Afrika ni maskini wa kutupwa, na bado wapo vijana Kwa wazee wanashangilia ufisadi huu, na maisha Yao ni hoehae bin taabani, Je nini tatizo la ngozi nyeusi?

Tunahitaji kina Raila wenye maono mapana kuzidi maslahi ya vyama vyao.

Bila sisi wenye nchi kuamka na kuchukua hatua itabakia kuwa kelele za chura tu.
 
Back
Top Bottom