Kikwete, Vipi wanawake wasitie Nia?

Filipo Lubua

JF-Expert Member
Nov 18, 2011
339
578
Nina swali rahisi tu kwa Mwenyekiti Wa CCM
Katika mchakato wa utiaji nia hadi sasa, bado sijaona mwanamke hata mmoja aliyejaribu kufanya hivyo. Je Rais wangu, bado mfumo wetu wa kidemokrasia haujatuwezesha kuwa na wanawake majasiri, wenye uwezo wa kutuongoza?

Mfumo wetu wa Viti-Maalumu haujatuzalishia wanawake wenye uzoefu na wawezao kufanya kazi za kiuongozi?

Jamani, wanawake mko wapi? Mbona nyinyi mnabaki wa kupiga vigelegele tu kila ifikiapo wakati wa uchaguzi? Kwanini mnaruhusu mfumo-dume kuendelea kutia mizizi?
 
Nikikumbuka ile siku yenu march 18, mlijitutumua sana kwamba hiki kipindi mnataka rais mwanamke....lakini mbona hatuwaoni ..mmebaki kuwa mashabiki
Wapi Anne kilango,tibaijuka,migiro...mnasubili uwezeshaji???
 
faizyfox gombea basi jf tukupe promo maana unaweza sana tatizo hujijui, ndio wale jk anataka tuwashawishi. mshindani wako mako najua afui dafu
 
Mtoa hoja kwanza Rais hausiki na nani atie nia, inapaswa mtu mwenyewe ajipime na kuijona kama anafaa kuchukua fomu. Ningependa sana watia nia wanawake wawe wengi sana na ninamtumaini yangu watajitokeza wa kutosha kama alivyoanza mama Amina
 
Wajinga wanangoja waambiwe( gombea) ili wapite kiulaini.safariii kila MTU anajiambia mwenyewe
 
Back
Top Bottom