Kikwete to announce stimulus for economy

Vigogo watajwa kujipa fedha zilizotolewa BoT
Kampuni ambazo zinaonekana katika orodha ya zilizopendekezwa ama zilizopata fedha hizo ni pamoja na S & C Ginning Co.Ltd (yenye makao yake Bulamba), Simon Agency Ltd (Mwanza), Fresho Investment Co. Ltd (Shinyanga), Gaki Investment Co. Ltd (ya Shinyanga), Bedugu Ginning Co. Ltd (ya Musoma), Intergrated Cotton Fields Ltd ( ya Mwanza), Igunga Cotton Company (makao yake yako Dar es Salaam), Robasika-Agroproducts Ltd yenye makao yake Kaliua, Tabora na Chesano Cotton Ginnery yenye makao yake Bariadi, Shinyanga.


Pamoja na kuishi kwangu muda wote huu Kaliua-Ushokora, ndiyo mara yangu ya kwanza kuisikia Robasika-Agriproducts Ltd. Labda wazee wa Igagala mtueleze. Duh! nimechoka kabisa na hii nchi yetu.
 
Aisee, pole baba Kikwete - naona utakapo maliza miaka yako kumi ya urais uombe kufa mapema maana utaozea jela! Simamia maslahi ya nchi vyema la sivyo umeliwa. Uliyaanzisha wewe na kama ilivyo ada mwosha naye uoshwa!
 
Sasa hao wakubwa si mtaje majina yao? Mnaogopa nini?Kampui zote zilizotajwa ni za kampuni zinazofanya biashara ya pamba.Kampuni zipi feki zilizomegewa fedha zitajeni?

Kampuni ya GAKI ilio na makao makuu Shinyanga inamilikiwa na Gasper Kileo, Mwekahazina wa CCM mkoa wa Shinyanga. Ni kweli anakusanya pamba. Ni rafiki wa watu pale mjini, viongozi karibu wote uwajuao wanamfahamu vizuri tu.
 
Unajua a Stimulus Package follows a Keynesian Economics that by introducing an injection in the economy it will have a multiplier effect towards the country economy. John Maynard Keynes alisema saa zengine private sectors zinakwama na hivyo basi a support from the public sector through monetary and fiscal policy will help to stimulate the economy.

Kama alivyosema MM anguko la uchumi US na Western Countries lilisababishwa na anguko la banking sectors. Na kwakuwa hizi banking sectors are the heart and soul of the private sectors in the country. These countries decided to inject cash (bailout) in these banks ili zisianguke kwani zinashikilia savings za watu ambao ni wananchi wa nchi ambao wameziweka katika hizo kampuni ili zizae interest au kwa matumizi ya baadae. Hivyo basi following the subprime mortgage crisis banks zilitaka kufa kifo cha mende which will led to a divastating consequences to the economy of these countries. Ndio maana hizi nchi zikaamua zisaidie hizi private sectors ziweze kuwa na msukumo wa kiuchumi. Ijapokuwa hilo sasa linapelekea nchi nyingi za western kuwa mlundikano wa madeni ambao some countries tunaona zimeanza kuanguka mfano Greece.

Sasa kituko kipo Tanzania ni hiki Kwanza the banking crisis haijawagusa hata nukta nchi za Africa. Kuna study nilifanya nikakuta while banks are struggling in US and UK, banks za Africa (egypt, Tanzania, Kenya) zilikuwa zinatengeneza faida. Swali likawa je how, utakuta kwanza nchi nyingi Tanzania ni Cash economy, Wanatumia zaidi cash instead of credits. Cash economy inamaanisha banks nyingi zilikuwa zinaautonomy katika kutoka mikopo kwani wanapata faida nzuri kwa risk ndogo. hilo likawa linawawezesha banks kugenerate faida kubwa kwani wanachaji interest ya juu. La pili nikakuta kuwa banks nyingi tanzania wanakopesha serikali, na corporate clients lakini wanabakiwa na cash kubwa kwasababu hawakopeshi. La mwisho nikakuta nchi hizi banks zake follows a prudent banking system mpangilio ambao unawafanya hizi banks zikopeshe wateja ambao wana kiwango kidogo cha risk. Banks like CRDB, NMB etc wanawekeza zaidi katika government bonds, migodi kuliko kukopesha mikopo ya nyumba ambayo ni very risk.

Swali likaja where is the bailout goes to? Kimsingi the banking crisis imetuaffect zaidi katika uchumi wetu (economic impact). Kwakuwa uchumi wa nchi ya Tanzania ni intergrated basi sekta kama utalii, uwekezaji zitakuwa affect vibaya sana kutokana na economic crisis. Likewise kilimo pia kitaathirika vibaya sana na mtikisiko wa uchumi. But maswali yanakuja je tanzania tunalima kilimo cha kuuza nje ya nchi?, Utalii unachangia kwa kiwango gani katika uchumi? Mbona bailout imeconcentrate katika Kilimo na kusahau sekta nyengine?

Sasa ukiangalia Kilimo cha Tanzania ni petty agriculture ambapo tunalima kujitosheleza wenyewe. Sasa kwakuwa hatuuzi nje impact ya uchumi wa kidunia itakuwa ndogo. Perhaps, tungelitoa pesa kuendeleza kilimo chetu ingelikuwa bora zaidi badala kudai eti wamebailout. Na tukumbuke wakati wenzetu US na UK bailout is a loan sisi tumeitransform a bailout to msaada (subsidy) sasa hili ni hatari kwa uchumi hasa ukichukulia hatuna system ya kumonitor ni hizi pesa zinaenda wapi. Ndio maana nakubaliana na wanasiasa kuwa hili ni EPA namba 2!!!!!!
 
Sitaki kuandika kuhusu hili nahofia kuandika kitu ambacho siwezi kukirudisha, yaani neno likitoka halirudi.

Tanzania sio kuwa imelohgwa nadhani imeshaoza na imekua mchanga.

Mavumbini Tanzania imesharudi
 
Sitaki kuandika kuhusu hili nahofia kuandika kitu ambacho siwezi kukirudisha, yaani neno likitoka halirudi.

Tanzania sio kuwa imelohgwa nadhani imeshaoza na imekua mchanga.

Mavumbini Tanzania imesharudi

Unajua kuiacha Tanzania ikapotea nadhani si busara lamsingi tunawasaidia kama wanataka mfano sasa hivi wanataka kuanzisha EPA ya 3 ambayokwangu mie haijakaa sawa.

Kuna hili swala la mikopo ya nyumba kwa wazawa. Kikwazo katika hili jambo ni how is it going to work. Chukulia facts zifuatazo Life expectancy ya mtanzania ni 55 years, per capital income ya mtanzania ni $1,353 ambayo ni kama $112 per month. which is roughly kama 173,071.25. na hiyo ni amount ambayo mtu wa kawaida anapata. Sasa tukija kuangalia sekta ya uchumi unakuta 60% ya population iko vijijini ambako huko hata mapato ya mwananchi hayajulikani yanapatikanaje. Na swali lengine linalokuja ni je ufatiliaji ya mikopo na udhibiti wa mfumuko wa bei za ardhi unasimamiwa na nani.

Mlalahoi mie nikienda kuomba hizo pesa za serikali nitaambiwa kuwa nijenge nyumba ya milioni 50 kama mkopo milioni 50 kwa land ambayo ni very speculative in tanzania nitanunua ardhi kwa thamani ya milioni 25 au 20. That means ni vizuri nikiwa na ardhi yangu then nikaombe hela. Likewise, nyumba za siku hizi watu wa majenzi wanasema hadi usimamishe nyumba nzuri unatakiwa uwe na si chini ya milioni 40. Sawa tuseme milioni 50 inatosha tuje katika malipo ndio utakuta ni challenging. How are we going to ensure the guy will repay the loan. Kwanza hatuna system ya kuweka mazingira ya ufatiliaji wa mikopo. Hivyo basi there will be alot of loan default ambazo sijui ufatiliaji wake utakuwa vipi. Vilevile faida itapatikanaje? Kama serikali imekusudia kusaidia wananchi na yenyewe lazima ijisaidie by charging a reasonable amount of interest. Otherwise, hili jambo litakwama kwani gharama hupanda na mahitaji pia sasa sijui likoje hili.La mwisho, Tunaambiwa life expectancy ni 55 but sijui hizo figure wamezitoa wapi? Tuassume wako sahihi unataka kunaimbia PB (Payback Period) ni 50,000,000/173,071 ni miaka 24!!! sasa tuseme jamaa anaishi kwa allowance mshahara analipia mkopo this means huyu bwana atakuwa anatakiwa alipe mkopo for about 24 years??? Na je watu wanaanza kuajiriwa lini? majority ya watu wanaomaliza vyuo vya juu ni miaka 26 na kuendelea so by the age of 50 (kama virusi havijampitia) ndio anamaliza mkopo???

Unakuta mazingira haya yanatengeneza mikopo ambayo itakuja baadae idefault. Likewise, usimamizi mbovu wa mikopo, sera mbovu zitachangia kutofanikiwa kwa mikopo hiyo je kwanini serikali inashikia bango? Jibu ni simple ni kwasababu katika sera hii ni rahisi sana kupitisha njia za ufisadi. Kwanza Kampuni hewa ambazo hazijulikani kichwa wala miguu zinaweza kupewa hela zikafa kifo cha mende ikabakia tunawatafuta warejeshe pesa za nchi, Pili inflated prices za ujenzi ni njia nyengine ya kuvuta hela, tatu kushindwa kulipa wakopaji ni njia nyengine inayoweza kusababisha pesa zikapotea kiza kiza.

Ushauri wangu kwanza kuwepo na usimamizi mzuri wa pesa, pia kabla hawajatoa mikopo kwanza waakikishe mradi kuandikisha vizazi na vifo (jina nimelisahau ) unasimamia vizuri, vitambulisho vya utanzania na kuandikishwa namba za simu na Tax identifier namba ziwe zimeshafanikiwa. nia na madhumuni ni kuweka mfumo ambao utajiendesha wenyewe na sio rahisi umazishi ukatokea. Tatu ipitishwe sheria ya kusimamia mfumuko wa bei ya ardhi.
 

  • Gavana BoT aruka kiunzi, amtupia mpira msaidizi wake

SAKATA la matumizi yenye kutia shaka ya fungu la fedha lililopitishwa na Bunge kwa ajili ya kuhami uchumi, maarufu kama stimulus package , sasa limemrudia Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Beno Ndulu, ambaye baada ya baadhi ya kampuni za ununuzi wa pamba kukosa mgawo huo katika mazingira yanayozua maswali zilimtaarifu naye akawajibu kuwa Serikali haina fedha.

Hata hivyo, wakati Gavana akitoa majibu hayo kuwa “Serikali haina fedha” si fedha zote Sh. trilioni 1.7 zilizoidhinishwa na Bunge la Tanzania ndizo zilizotumika katika mpango huo wa kunusuru uchumi uliotikiswa baada ya uchumi wa dunia kuyumba.

Wiki hii Gavana Ndulu amekwepa kuzungumzia suala hilo, akidai kwamba kwa sasa linashughulikiwa na mtu maalumu chini yake anayepaswa kutafutwa kuzungumzia suala hilo.

Raia Mwema ilipozungumza na Profesa Ndulu, ambaye alieleza kuwa yuko mkoani Mwanza kwa ajili ya mkutano, alisema masuala ya ‘‘stimulus package’’ yamekabidhiwa mtu maalumu ndani ya benki hiyo, na kwamba si yeye anayeweza kuyazumngumzia.

“Haya masuala ya stimulus package tumempa mtu maalumu ambaye ni mkuu wa kitengo cha sera na utafiti, mimi siwezi kuyazungumzia,” alijibu Ndulu hata alipotakiwa kujibu yale yanayomhusu moja kwa moja katika sakata hilo pia hakuwa tayari kuzungumzia.

Uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kuwa fedha zilizokwishakutumika ni sehemu tu ya Sh trilioni 1.7 zilizopitishwa na Bunge, ambazo ni takriban Sh bilioni 870.8. Fedha hizo Sh bilioni 870.8 kwa mujibu wa taarifa zilizopo ndizo zilizokwishakutolewa na Benki Kuu (BoT), chombo ambacho kimepewa mamlaka ya kutoa fedha hizo.

Kwa mujibu wa utaratibu wa BoT, fedha hizo hutolewa kutoka benki hiyo kwenda katika benki ambazo zilikopesha kampuni zinazostahili kufidiwa, ambazo zimeathiriwa na mtikisiko wa uchumi duniani.

Raia Mwema limepata kuripoti kuhusu utata uliopo katika benki hizo katika kufidia kampuni husika ikibainika kuwa baadhi ya michanganuo ya hesabu za kampuni husika inaonyesha hazikupata hasara lakini baadhi ya benki zilipendekeza kampuni hizo zilipwe fidia ya mabilioni.

Mbali na baadhi ya kampuni kulipwa fidia pasipo kupata hasara kwa mujibu wa taarifa zao za kihasibu zilizowasilishwa katika benki husika, zipo kampuni nyingine ambazo zimebainika kupata hasara ndogo lakini ikipendekezwa zilipwe fedha nyingi zaidi kama fidia.

Taarifa zaidi zinabainisha kuwa sehemu ya fedha hizo zimepelekwa kwa kampuni zinazohusika na mazao ya kahawa zao ambalo pia huuzwa katika soko la dunia kama ilivyo kwa pamba.

Nyraka ambazo gazeti hili limepatiwa zinazoonyesha taarifa za benki na michanganuo ya kampuni husika, Benki ya CRDB ikipendekeza kampuni 26 zilipwe mabilioni kadhaa na mbili zikitupwa nje ya mgawo, wakati benki ya TIB ikiidhinisha malipo kwa kampuni moja ya Al-Adawi, kupewa fidia ya Sh milioni 405.6 ambazo mapendekezo ya awamu ya pili hayakuridhia malipo hayo.

Benki nyingine zilizohusika ni Kenya Commercial iliyokagua mchanganuo wa kampuni ya Birchand Oil Mills Ltd, iliyopendekeza kampuni hiyo ifidiwe Sh bilioni 1.66, lakini mapendekezo mbadala ya watalaamu yalitaka kampuni hiyo ifidiwe Sh bilioni 4.642, Exim Bank Tanzania Ltd imependekeza kampuni ya Bio Sustain kufidiwa Sh milioni 597.7 lakini baada ya uhakiki mwingine kampuni hiyo ikapendekezwa kulipwa milioni 458.1 na Stanbic Bank ilipendekeza kampuni ya S & Ginning Co. Ltd kufidiwa Sh bilioni 5.69, lakini ikabainika inastahili kufidiwa Sh bilioni 2.86.

Katika Benki ya CRDB utata unazidi miongoni mwa kampuni ambazo zimeomba fidia kupitia benki hiyo. Kampuni ya Badugu Ginning ya Musoma, ambayo hesabu zake zinaonyesha katika shughuli zake imetumia Sh bilioni 4.41, ikipata mapato ya Sh bilioni 2.94 kwa mauzo ya pamba na Sh milioni 727.6 kutokana na mauzo ya mbegu za pamba na pato lake la jumla ni Sh bilioni 3.7, ikiwa imetengeneza hasara ya milioni 742.2.

Licha ya mchanganuo huo unaoonyesha kampuni hiyo kupata hasara ya Sh milioni 742.2 ilipendekezwa na Benki ifidiwe Sh bilioni 1.4, hata hivyo mapendekezo ya awamu ya pili yalipinga taarifa hizo na kutaka kampuni hiyo ifidiwe Sh milioni 742.2 tu.

Kampuni ya Chesano Cotton Ginning Ltd ya Bariadi, Shinyanga imebainisha CRDB kuwa matumizi yake (ununuzi na uendeshaji) ni Sh bilioni 2.6, mapato yake kutokana na uuzaji nyuzi za pamba ni bilioni 1.99 (bilioni 2), mauzo yaliyotokana na uuzaji mbegu za pamba ni Sh milioni 586 na kwa hiyo mapato yake ya jumla ni sh bilioni 2.6.

Utata unaojitokeza ni kwamba kwa mchanganuo huo wa Benki ya CRDB kampuni hiyo imepata faida ya Sh milioni 6.4, lakini benki hiyo hiyo ikapendekeza kampuni ifidiwe Sh milioni 580. Hata hivyo, ukaguzi zaidi wa hesabu ulipofanyika, kampuni hiyo haikupendekezwa kulipwa chochote. Kampuni nyingine ambayo fidia yake inaonyesha utata ni Gaki Investment Ltd ya Shinyanga.

Gaki Investment Ltd imebainika kununua kilogramu takriban milioni 19.8 za pamba, ikitumia Sh bilioni 12.9, mapato yake baada ya biashara ya nyuzi za pamba ni Sh bilioni 12.15, mapato yaliyotokana na kuuza mbegu za pamba ni Sh bilioni 1.727 na kwa hiyo mapato yake ya jumla kwa msimu husika ni Sh bilioni 13.9, ikijizolea faida ya Sh bilioni 1, lakini ukaguzi wa kibenki (CRDB) ukionyesha imepata hasara milioni 146 na ifidiwe kiasi hicho, lakini ukaguzi wa pili huru ukapendekezwa kampuni hiyo kutolipwa chochote.

Kampuni ya Igunga Cotton Ltd yenye makao yake makuu Dar es Salaam, hesabu zake zilizowasilishwa CRDB ambazo gazeti hili limepata mchanganuo wake zinabainisha ilinunua kilogramu milioni 2.8, ikitumia Sh bilioni 1.9, mapato kutokana na mazao ya pamba iliyonunua Sh bilioni 1.43, mapato kutokana na mauzo ya mbegu za pamba ni Sh 300.5, mapato yake ya jumla ni Sh bilioni 1.7, ikitajwa kupata hasara ya Sh milioni 205.

Lakini licha ya kampuni hiyo kupata hasara ya Sh milioni 205, ilipendekezwa na watalaamu wa benki ya CRDB ifidiwe Sh milioni 839, hata hivyo uhakiki huru wa awamu ya pili ulipofanyika, kampuni hiyo ikatakiwa ifidiwe hasara yake halisi ya Sh milioni 205.

Ipililo AMCOs Ltd ambayo katika msimu husika ilinunua pamba kilogramu milioni 101, ikitumia Sh milioni 82, na mauzo yake ya nyuzi za pamba yakiwa Sh 54.5 na mauzo ya mbegu za pamba yakiwa Sh milioni 10.8, mapato yake ya jumla yakiwa Sh milioni 65.35, ikitajwa kupata hasara ya Sh milioni 16.7 lakini ikapendekezwa na benki ifidiwe Sh bilioni 51, ukaguzi wa pili ulipofanyika ikapendekezwa ifidiwe hasara halisi tu, ambayo ni Sh milioni 16.7.

Jambo Oil & Ginneries Ltd ya Shinyanga, katika msimu husika ilinunua kilogramu milioni 22.08, kwa gharama ya Sh bilioni 13.9. Mapato ya kampuni hiyo katika uuzaji wa nyuzi za pamba ni Sh bilioni 12.51, mauzo kutokana na mbegu za pamba yameiingizia kampuni hiyo Sh bilioni 2.4 na kwa hiyo mapato yake ya jumla ni Sh bilioni 14.9, ikijipatia faida ya Sh milioni 927.1, utata unaibuka pale benki baada ya kupitia mchanganuo huo wa hesabu kupendekeza ifidiwe Sh bilioni 1.06.

Kahama Oil Mill Ltd ya Kahama yaShinyanga, ilinunua kilogramu milioni 24.9 na mchanganuo wa kampuni hiyo uliowasilishwa benki ukionyesha kuwa imetumia Sh bilioni 19.8, ikipata Sh bilioni 14.6 kutokana na mauzo ya nyuzi za pamba na Sh bilioni 2.7 za mauzo ya mbegu za pamba na kujipatia mapato ya jumla, Sh bilioni 17, ikipata hasara ya Sh bilioni 2.3, lakini benki ikipendekeza ifidiwe Sh bilioni 4.4.

Kampuni ya Kisumwa Machinery Ltd, ambayo nyaraka zilizopo hazibainishi kama imewasilisha mchanganuo wake lakini wakati huo huo imependekezwa ilipwe fidia ya Sh milioni 377. Mbali na kampuni hiyo, kampuni nyingine ambayo ingawa mchanganuo wake haukubainishwa lakini ikipendekezwa kulipwa fidia ni Morogoro Canvas Mills (1998) Ltd, iliyopendekezwa na benki ilipwe fidia ya mtikisiko wa uchumi duniani, Sh bilioni 1.612.

Sakata la fedha hizo lilianza mwaka jana wakati Serikali ilipowasilisha bungeni suala la ‘stimulus package’ ambapo Kiongozi wa Upinzani, Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed, alisema fedha hizo hazina tofauti na fedha zilizoibwa BoT kutoka Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA) kwa kuwa hazijawekewa utaratibu unaowezesha kuwapo uwazi na uadilifu.

Akizungumza katika hotuba yake bungeni mwaka jana Hamad, kwa niaba ya wabunge wenzake kutoka vyama vya CUF, CHADEMA na UDP, alihoji masuala mbalimbali kuhusu matumizi ya fedha hizo za stimulus package, zipatazo Sh. trilioni 1.7, zilizokuwa zimetangazwa awali na Rais Jakaya Kikwete.

“Tunataka sheria ya Appropriation Act iwe na Schedule maalumu ya Stimulus Package na iseme waziwazi nani atapata nini, kamati ya Fedha na Uchumi ya Bunge iwe inapata taarifa kila miezi mitatu ya utekelezaji wa hiyo stimulus package.

“Ni ukweli uliowazi kuwa stimulus package inazinufaisha benki tu, kwa kuzipa mwanya wa kufanya biashara nzuri na Serikali kwa kutumia fedha za Serikali yenyewe, na ndiyo maana katika nchi nyingine Serikali imelazimika kuwa na hisa ili kuhakikisha kuwa fedha iliyotolewa ambayo inatokana na kodi za wananchi inadhibitiwa na kurudi kwa walipa kodi na wapiga kura,” alisema.

Hamad alisema katika bajeti ya mwaka 2007/08 na ile ya 2008/09 Serikali ilijizuia kukopa kwenye mabenki, kwa kigezo kikubwa kuwa mabenki yaweze kufanya biashara ya kukopesha sekta binafsi na kuwa zuio hilo liliongeza ufanisi kwa mabenki kukopesha sekta binafsi kwani mikopo kwa sekta binafsi ilipanda hadi kufikia asilimia 40.

Alisema Hamad: “Serikali imeamua kufidia vyama vya ushirika na kampuni zinazonunua mazao ya wakulima na kuyauza kwa hasara. Katika soko huria kuna kupata faida na kupata hasara. Wafanyabiashara makini wa mazao hupanga bei zao za kununulia mazao kwa kuzingatia bei walioipata katika soko la baadaye.

“Hata hivyo wengine hawapendi kuchukua tahadhari kwa kutegemea kwamba bei itapanda na kwa hiyo watapata faida kubwa. Bei imeshuka kwa hiyo wamepata hasara. Je, hakuna wafanyabiashara wa mazao waliolipa mikopo waliokopa kwa kujibana. Serikali ina uhakika gani kuwa mikopo hii ilitumiwa vizuri?”

Aliongeza: “Serikali imeamua kutoa udhamini wa madeni ambayo wakopaji kwa sababu ya msukosuko wa uchumi wa dunia wanapata matatizo kulipa kwa wakati. Serikali imeamua madeni haya yadhaminiwe kwa miaka miwili na si mwaka mmoja ili shughuli za Uchaguzi Mkuu wa 2010 ziwe zimemalizika. Hii itatoa mwanya kwa wanaodhaminiwa madeni wachangie kwenye kampeni na baada ya uchaguzi mzigo wa madeni ubebwe na Serikali.

“Kuna hatari ya EPA nyingine kuzinduliwa. Ukaguzi wa kina wa mahesabu ya makampuni husika ufanywe na CAG (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali) kwa gharama za mabenki yaliyokopesha kabla ya Serikali kuyadhamini makampuni haya,” alionya Hamad wakati huo.
 
who cares!!! tuliwaambia toka mwanzo..hawakusikia..

Kuna Kilimo kwanza

kuna Kashfa ya Pembejeo..

na watu bado katika akili zao timamu wataendelea kuchangia ili kiendelee kuwa madarakani!!!
 
Masikini Ndulu, ningekuwa yeye nisingesubiri kuitwa Dodoma. Atakimbiwa tu na mwisho wa siku atajikuta peke yake, peke yake kabisa. Hayo ndiyo malipo ya kumtumikia mlafi - ni kama vile kula ule wewe lakini kushiba ashibe yeye, yale yale yalomkuta Balali.
 
Naweza sema tunaongozwa na NSYUKA hawa watu hawana tofauti na pepo NSYUKA yaani mtu alieinadi kwa nguvu na kuitetea pale bungeni huku akicheka kumbe alikua anatucheka sisi wadanganyika hii ni hatari. Sasa tushamjua lakini je wote tunaona? au wengine ndo mimacho vidondaa? Lakini kama huyu mtetezi wa stimulus package si mroho wa madaraka anatakiwa ajiuzuru kila kitu kilicho mikononi mwake ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji, vinginevyo natilia shaka huu mtandao wa mafisadi unaweza kuwa mkali kuliko hata ule wa mihadarati ulioongozwa na CARLOS.
 
This was expected.
Ila chakusikitisha ma-architecture wa ufisadi Tanzania ni wale wale kina Kimei (CRDB) na wenzake. Nakumbuka siku hii stimulus plan inasomwa na JK niliona wazi kabisa anayoyasema yote hayana utafiti wa kuridhisha ila ni mpango wa kunufaisha watu kwa vigezo vya kuyumba kwa uchumi. Kimsingi, hizi plan pamoja na mabilioni ya jk na mengineyo lengo lake hasa ni kuboost uchumi, ila kwa Tanzania ni vice-versa. Benki kuu kwa ujumla imejidharilisha na kuonyesha ni jinsi gani haina watu makini, na hii inatia mashaka sana uwezo wa BOT kusimamia sekta ya fedha nchini. Kashfa zinaibuka kila kukicha, mara watu wameiba kupitia mtandao wa malipo (TISS), EPA, minara pacha, sasa na hili la stimulua package n.k. Tanzania inahitaji overhaul ya khali ya juu, na sijui how to go about it with the current generation!

 
Mimi kila siku nasema hawa wezi woteeeee ni wa KUUWA HAKUNA MJADALA MTU ALIYEIBA NA KUNA USHAHIDI WA KUTOSHA APIGWE REISAS AFE, WATU WATASHIKA ADABU, KUWAFUNGA NA KESI ZA KILA SIKU HAISAIDII KITU, PESA ZA WALIPA KODI ZINAZIDI KUPOTEA TUUUUU, MAANA WAKIWA HUKO JELA WALISHWE, WALINDWE NA TUNATUMIA PESA ZA WALIPA KODI, hakuna haja dawa ni moja tuuuuuu piga risasi wezi woteeeeeee uwa uwa uwa wezi woteeeeeeeee. Wabaki wachache wasafi tuendelee kujenga nchi yetu

Tatizo corruption nchi hii iko sooooooo deeeeeep dawa is kill all these bastards..
 
Most of the money will find route back into CCM for campaign. And into individuals accounts. One of these days tutaambiwa pia kuhusu EPA nyingine, lets wait and see. We will always be doing mactime. No forward movement we can achive execpt for few scripulous individuals protected by politicians.
 
It is so sad to see things like these happening in our poor country. The president is the one to blame, undisputable!!!. All those who are involved shall one day pay when the payback time arrives, they will never get away with it. Cause the one who fights for us is stronger than them all, and this is Allah.
 
Back
Top Bottom