kapotolo
JF-Expert Member
- Sep 19, 2010
- 3,727
- 2,214
JK kwenye kampeni zake leo Songea, kwa kujisahau au makusudi kwa kujua watanzania ni majuha, amezidi kutoa ahadi kwa mambo ambayo bunge limeshayapitisha. Leo anasema akiwa rais ataipandisha hadhi hospitali ya Peramiho- Songea. Hospitali hii imeshapandishwa hadhi na ilitangazwa na waziri wa afya na ustawi wa jamii katika bunge lililopita (Hospitali za jiji Dar zapandishwa hadhi).(Hii link pia inataja hospitali za mikoani zilizopandishwa hadhi toka July mwaka huu - Peramiho ikiwa mojawapo)
Hii inakuwaje tena ni ahadi? Hii kama si kuwahadaa wananchi na kutufanya majuha ni nini? Ili aje aseme tuliahidi na tumetimiza.
Tumuogope mtu huyu kama ukoma, yeye mwenyewe amesema ukimuona mtu mzima anasema uongo, kuna mawili, either yeye mwenyewe ana matatizo au anawaona majuha wale anaowaongopea, kwa hiyo JK labda ana matatizo au anatufanya sisi majuha. Tukatae kuwa majuha ndugu zangu nawaomba sana. Mungu awabariki.