Nikiangalia hii sampling ndogo ya 2000 respondents na mkanganyiko wa parameters walokuwa wakizitafuta, I suppose we can safely label the whole thing as simply senseless, bogus and unscholarstic.
Jamani eeeh... kama alivyosema Mtanzania, tushukuru hizo polls zimeshuka kwa kiwango hicho...Siku zote tujiandae kwa habari mbaya kuliko njema na polls kama hizi ziwe kiamsho kwa wananchi kwamba vita yetu bado kabisa haijafikia ushindi..
Binafsi sipendi kabisa CCM irudi jukwaani lakini nafahamu fika Kikwete bado ana mvuto mkubwa sana kwa baadhi ya watu tofauti na wengi tunavyofikiria...Hiyo asilimia 62 imenipa moyo sana kwa sababu naamini kabisa kuwa wabunge wengi wa CCM walipita kutokana na nguvu ya Kikwete akiwa ndani ya Mtandao..NBa polls siku zote hupigwa toka mitaani na kwa idadi ndogo sana na watu.. Still, kati ya kila watu 10 haiwezekani wote mkafikiria sawa..
Sasa kama wananchi wameanza kuunganisha vitu hivi viwili tena wakati huu mbaya wa uchumi duniani nina hakika by 2010 rating ya Kikwete itakuwa chini zaidi..
Nina hakika wananchi hawataafiki sababu zozote zinazohusiana na hali ya Uchumi duniani kuwa ndio sababu bali Kikwete mwenyewe..Na laukama wapinzani wakijipanga na list ndogo tu ya Mbowe, Dr. Slaa, Lipumba na Mtu mwingine maarufu toka Zanzibar..Basi ushindi umepatikana..Kikwete can't stand alone kitaifa anaweza kushinda ndani ya CCM lakini Kitaifa itategemea na wapinzani wamejipanga vipi..
It's gonna be the Only time ya kula Turkey! -Thanksgiving day..[/QUOTEa]
Mkuu,
well said but only if wishes were horses everyone would ride one. Hata wewe leo hii ukiweza kupata pesa ya ufisadi ukawahonga NEC na CC ya sisiwehu utaukwaa urahisi bila hata kutumia sera kwenye kampeni bali ahadi kibao kama vile watu walale tu bila kufanya kazi na watapata maisha bora kwa kila mdanganyika. Uelewa wapiga kura ni karibu na hakuna.
Kuna wakati nilienda kwa babu yangu huko Sengerema nikakuta mzee mmoja pale kijijini ambaye kwa pale anaonekana ndio muelewa yuko kwenye foleni anasubiri mahindi ya mgao(msaada). Kukatokea ubishi wa kisiasa kuhusu rafu alizofanyiwa Masha na William Shija. Yule mzee mjuaji akaanza kuwasifia FFU kwa kumpiga Masha wakati inajulikana wazi kuwa masanduku yaliyokuwa yaamue hatima ya shija yalitoweka na hayakujumuishwa. Kwa baraka za msimamizi (mkurugenzi wa halmshauri) matokeo yakatangazwa Shija kashinda. Na hayo ni masanduku ya hapo Sengerema mjini ambapo shija alikuwa hatakiwi. Kwa ujumla Hata kama wapinzania wote wakiungana haki haiko upande wao. Wakazanie tu wabunge sehemu wanazokubalika.
Hapa inawezekana uko sahihi kwa kiasi fulani. Kumbuka tu kuwa karibu wote wanochangia hoja hii wamefanya huo utafiti ama kama principal researchers au research assistants. Na ukweli nikuwa dodoso hizo hujaziwa kwenye vyumba vya guest house za bei rahisi kama umeshawahi kufanya utelewa nini nasema. Watu huenda kule kupata ile posho na ili kuikoa hujaza dodoso kwa kujihoji wenyewe na kutoa majibu kadri ya mtizamo wao[/QUOTE]Ukiachilia mbali wengi wetu tanzania tunaijuwa kutoka katika mitandao na magazeti yaliyopoteza dira ya ujenzi na kuchukua mwelekeo wa kubomoa.[/QUOTE]Watanzania tujifunze kukubali kusikia tusiyoyapenda. Kukimbilia kushutumu taarifa yeyote isiyoendana na fikira na mitazamo yetu bila hata kujua undani wa zoezi zima la utafiti lilivyofanyika ni kufilisika kimawazo. Watanzania ni karibia milioni 40 na wanaowakilisha kada yetu tunaotumia mitandao hawafiki milioni moja. Sasa iweje sisi wachache hivyo tukawa tunajua mitizamo ya watanzania wenzetu walio wengi ambao inawezekana kabisa wakawa wanaangalia hayo tunayoyaona ni mapungufu ya JK kwa mtazamo mwengine kabisa.
Hapa tuko pamoja kasoro hiyo sentensi niliyo ihighlight
hii nayo haijatulia kwani sababu ni nilizokupa huko juu. Kwamba yalitokea ambayo REDET walisema haimaanishi tumekubali utafiti wao ulikuwa wa kisayansi. Ni kama sheikh Yahya kutabiri halafu ikawa hivyo huwezi kutuambia alisema tukubali tu alikuwa anaelewa. REDET walisoma upepo na hivyo wakapiaka takwimu na matokeo yake si ndiyo hayo Mkandala ni VC na anaua chuo kikuuKumbukeni wengin tulikimbilia kubeza utafiti wa REDET kabla ya uchaguzi wa 2005 kama ilivyo sasa na kuacha kuufanyia kazi kama changamoto. Matokeo ya uchaguzi mkuu yalipokuja hayakuwa na tofauti na matokea ya utafiti wa REDET kwa uponde wa urais na ubunge pia.