Kikwete awalinda Mawaziri - Asisitiza waachwe, UPEPO HUU UTAPITA!

Huyu ni kilaza zaidi ya tumjuavyo hivi anatuonaje watanzania? Kwa hili naconclude tushaonekana sie ni chura hatuwazuiii.............. Maji. Alishasema ye anajeshi sie.........., maneno tuuu.

Ndo maana Pinda huwa analia tu
 
Mh. Pinda,
Pole sana na Hongera kwa uadilifu na umakini wako. Tumeanza kuelewa kuwa kumbe kazi yako ni ngumu mno na ndio maana huwazi kuendelea nayo. Kama kweli Mh. Rais amekataa mawaziri wasijiuzulu na tayari ulishawaweka sawa kwa sababu ya moyo wako wa uwajibikaji hii ni mbaya sana.
Kwa kuwa mheshimiwa raisi hatawahi kugombea nafasi nyingine yoyote baada ya 2015 basi madhara yake kisiasa ni historia yake tu ataiacha vibaya. Kwa upande wako historia yako imekuwa nzuri hadi sasa. Ila ukweli kwa hili nakushauri ujiuzulu kama kweli mawaziri wako wametiwa moyo na Rais kutokuondoka.

Vyombo vya habari viliandika na kwa kuwa haikukanushwa wananchi wote wanaamini ni ukweli ulisimamia
mawaziri wako wakaandika barua za kujiuzulu. Hilo lilikuwa ni heshima kwako. kwao, na kwa chama na serikali yetu.

Sasa kama kuna mabadiliko hii nifedheha kwako, kwa chama, mawaziri na kwa serikali yako.
Kila mtu anaamini kutokana na uzito wa hoja basi walijiuzulu.

Japo bado sijaamini kama raisi kweli atakubali kuwaambia wasijiuzulu, lakini kwa kuwa limetajwa nimeona nikutie moyo mapema usikute kweli imetokea.
Kama imetokea basi nakushauri wewe ujiuzulu na wala usijali watakaosema umetishwa na hoja ya wabunge hilo lisikusumbue. Huwezi kuendelea kufanya kazi katika mazingira haya ya wewe kutokuwa na uwezo wa kutumia utashi, uwezo, dhamira na moyo wako katika kusimamia mambo.
Jiuzulu sio kwa kushindwa bali kwa kuilinda heshima yako. NAKUSIHI KAMA KWELI HAWAJAJIUZULU MAWAZIRI BASI JIUZULU MWENYEWE. Pia wabunge wa CCM onyesheni heshima kwa nchi yenu juu ya mambo mazito kama ufisadi unaotesa nchi hii.

Uko sahihi kabisa, Kama kweli mh. Pinda anaamini kuwa hao mawaziri wanatakiwa kung'oka na rais anagoma, kwa heshima yake inabidi yeye ajiuzuru ili raisi alazimike kuvunja baraza la mawaziri. Itakuwa ni heshima kubwa kwake.
 
Kama JK amefanya hv, hajui dhana ya accountability..kama kweli hawa mawaziri hawatojiuzulu kwa nn wananchi tusiingie barabarani
 
Mimi nina wasiwasi kuwa tanzania ilisha uzwa kitambo ila hawataki kutuambia ukweli,watanzania amkeni,hii tanzania si ya ccm ni ya watanzania.
 
Dharau kwa watanzania

Dharau kubwa sana, watu wanaiba waziwazi, wanawajibishwa wewe unasema upepo????
 
Niliweka bandiko humu kuwa anayetakiwa kuwajibishwa ni JK na sio Pinda. Watu wakaniona pimbi. Sasa hapo mwenye afadhali nani kati ya hawa wawili? Tunataka mabadiliko halafu tunamuogopa mwenye nyumba? M4C ya kweli ni kuanza maandamano nchi nzima kuelekea ikulu moja kwa moja.

Naunga hoja mkono.
 


• ASISITIZA WAACHWE, UPEPO HUU UTAPITA

na Mwandishi wetu
WAKATI taarifa ya Kamati ya wabunge wa CCM chini ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, juzi iliridhia mawaziri wote wanaokabiliwa na tuhuma za ubadhirifu kwenye wizara zao wajiuzulu, jana Rais Jakaya Kikwete aliwasili nchini akitokea Brazil akiwa na msimamo tofauti.

Taarifa zinasema kumekuwa na mazungumzo baina ya Rais Kikwete na Pinda yaliyolenga kunusuru serikali yao lakini walitofautiana kuhusu hatua inayopaswa kuchukuliwa dhidi ya mawaziri waliotakiwa kujiuzulu.

Msimamo wa Pinda inadaiwa kuwa anataka mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma waondoke ili kuleta uwajibikaji serikalini, lakini Rais Kikwete amesema mawaziri hao waachwe waendelee na kazi zao, kwa kuwa suala hili ni la upepo tu, liachwe litapita.


Tanzania Daima Jumapili limeelezwa kuwa rais anakataa shinikizo hilo kwa madai serikali haipaswi kuyumbishwa yumbishwa.


Miongoni mwa mawaziri wanaopaswa kuondoka ni Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo; Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Cyril Chami na naibu wake, Lazaro Nyalandu; Waziri wa Tawala wa Mikoa na Serikali za Mitaa, George Mkuchika na naibu wake, Aggrey Mwanri; Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda na naibu wake, Lucy Nkya na Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu.


Wengine ni Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige.


Habari zinasema Rais Kikwete na Pinda walitofautiana juu ya hatua dhidi ya mawaziri hao, hivyo kuwafanya baadhi ya mawaziri kutamba mitaani kuwa hawang’oki madarakani kwa sababu tayari bosi wao ameonyesha kutounga mkono tuhuma zinazoelekezwa kwao na wabunge wa upinzani na CCM.


Habari hizi zinasema pia kwamba Pinda amekuwa hafurahishwi na msimamo wa ‘bosi’ wake, hasa katika kushindwa kutoa uamuzi mgumu.


Zinadai kuwa rais amekuwa na tabia ya kuacha upepo uchukue nafasi yake wakati Pinda anataka baadhi ya watu wawajibike bila kujali nyadhifa zao au ukaribu na kiongozi mkuu wa nchi ili kurejesha imani ya serikali kwa wananchi.


Pinda inadaiwa amekuwa akitaka maamuzi magumu yafanyike, kwakuwa yeye ndiye anayesulubiwa na maswali pamoja na hoja za wabunge wawapo bungeni.


Baadhi ya wabunge waliozungumza na Tanzania Daima Jumapili, wameweka wazi kuwa kama Rais Kikwete ataamua kuwalinda na kuwatetea mawaziri wake basi watawaondoa kwa mkakati tofauti utakaomlazimisha rais kukubaliana na hoja za wabunge.


Baadhi ya wajumbe waliozungumza na gazeti hili waliweka wazi hatua hiyo inahitaji muda na mipango madhubuti na wao wapo tayari kufanya hivyo, kwani nchi inazidi kudidimia kwenye umaskini huku watu wake wakikosa huduma muhimu za kijamii.


Walisema kwa muda mrefu wamekuwa wakiwalalamikia watendaji wa serikali na chama tawala lakini rais amekuwa mgumu wa kuyashughulikia matatizo hayo.


Wanasema rais ndiye kikwazo kikubwa cha maendeleo ya chama chao na serikali, hasa kwa kuwateua mawaziri, wakurugenzi na maofisa wengine bila kuangalia uwezo wao wa kiutendaji.


“Kaka kwenye Bunge la Februari kuna mbunge alitoa kauli kuwa kama tunaona mambo hayaendi serikalini tupige kura ya kutokuwa na imani na rais, watu walimshambulia. Sasa tunaona umuhimu wa kauli yake ile,” alisema mbunge mmoja.


Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa makada wa CCM wameanza kuingiwa na hofu ya kubomoka kwa chama chao hasa baada ya makada wenzao kuanza kujiunga na vyama vya upinzani.


Wanasema wakati makada wa chama hicho wakiendelea kukihama uongozi wa CCM hauonekani kuchukua hatua zinazostahiki dhidi ya viongozi wanaochangia wananchi wakose imani na chama tawala.


Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, aliweka wazi kuwa wabunge wa CCM ni lazima wakemee ubadhirifu kwakuwa Tanzania si mali ya CCM.


Mbunge huyo alikwenda mbali kwa kumtaja Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo, kuwa ni mwizi, mwongo na mbadhirifu wa mali za umma.


Mawaziri wasuasua kuwasilisha barua

Hadi jana Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema hajapokea barua ya kujiuzulu kutoka kwa waziri yeyote huku akiweka wazi kuwa kesho atatoa taarifa kamili juu ya jambo hilo.

Juzi vyombo vya habari vilipata taarifa kutoka kwenye kikao cha wabunge wa CCM kuwa baada ya wabunge kuzituhumu baadhi ya wizara kukithiri kwa ubadhirifu mawaziri wake wameamua kujiuzulu.


Taarifa hizo zilidokeza kuwa mawaziri hao walishinikizwa kuachia nyadhifa zao ili kukinusuru chama na serikali dhidi ya hasira za wananchi wanaokerwa na ufisadi.


Chami atoboa siri

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, amejitetea kuwa wizara yake haimlindi Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Charles Ekelege, kama alivyotuhumiwa na baadhi ya wabunge.

Alisema amesononeshwa na taarifa ya ukaguzi wa CAG juu ya TBS iliyotolewa kwa waheshimiwa wabunge bila yeye mwenyewe au wizara kupewa nakala kwa kipindi cha wiki nzima.


Alisema kuwa baada ya kusikia kuwa waheshimiwa wabunge wengi wanayo taarifa hiyo na hata naibu wake kukiri bungeni kwamba taarifa imetoka wakati yeye hana nakala, alikwenda kwa Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashillilah na kuiomba nakala ya taarifa hiyo.


Alibainisha kuwa baada ya kufanya ufuatiliaji katika ofisi ya CAG ilikiri kuigawa kwa wabunge na kusahau kuipeleka kwa wizara hiyo ambayo ndiyo inayohusika.


“Hapa wasomaji wapime wenyewe. Inawezekanaje taarifa ya CAG iliyoandikwa kutokana na takwimu zilizotolewa na wizara yangu, iwafikie wabunge huku wizara yangu itakayotakiwa kuifanyia kazi taarifa yenyewe haipewi nakala, eti kwa kughafilika?


“Ni ukweli ofisi ya CAG walighafilikiwa, au jambo hili limesukwa ili kuniaibisha mimi mbele ya Watanzania, rais aliyeniteua na hasa wapiga kura wangu wa Moshi Vijijini?” alihoji.


Nundu ajitetea

Naye Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, alisema tuhuma dhidi yake zilizoelekezwa na baadhi ya wabunge, hazina ukweli na zimelenga kumchafua.

Alisema kilichoelezwa na Kamati ya Miundombinu ni uongo na uzushi, kwani nyaraka walizozitumia kuorodhesha tuhuma dhidi yake si halali.


Kuhusu kuingilia utendaji wa Mamlaka ya Bandari kwa masilahi binafsi, alisema si kweli, akaongeza kuwa kinachomponza ni kuipinga kampuni inayotetewa na menejimenti isipewe zabuni ya kufanya upembuzi yakinifu peke yake na kwenda kukopa na baadaye iruhusiwe kujenga gati namba 13 na 14.


“Wanasema namtaka mwekezaji ambaye makubaliano yanaonyesha atamiliki gati hilo kwa miaka 45. Nachelea kusema ni uongo na uzushi,” alisema Nundu.


Mkuchika apata kigugumizi

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika, alipoulizwa juu ya suala hilo alishindwa kukubali wala kukataa iwapo ataandika barua ya kujiuzulu. Alimtaka mwandishi amuulize Katibu wa Kamati ya Uongozi

Kweli uraisi Tanzania ni RAHISI
 
Ninalo tegemea hapo kesho ni mh.Pinda kuweka wazi msimamo wake bila kujali shinikizo lolote.Atatangaza heshima yake na dhamira yake kweli yeye ni mtoto wa mkulima na yuko kwa maslahi ya wanyonge.Sitegemei ataandika historia chafu katika uongozi wake uliotukuka kwa miaka yote ukizingatia ni kijana wa mwalimu aliyekaa muda mrefu ikulu kuliko mtu yeyote yule.Maadili na hekima aliyonayo ndiyo chachu pekee iliyomsababisha kudumu ndani ya nyumba yetu takatifu mpaka alipoamua kuchukua uamuzi wa kuwa mwanasiasa.Kama bwana mkubwa ana wakingia kifua basi ni dhahiri mawaziri wanatekeleza kile alichowaagiza katika kuifilisi nchi.Cha muhimu mh .Pinda jiuzuru kulinda heshima yako.
 
Yaani Kikwete, JK, Vasco da Gama, Ba Mwa'asha, Wabunge wanalalamikia Wizi wa wazi unaofanywa na hawa Mawaziri na kuipeleka nchi pabaya, sasa kistaarabu tu wanataka wapishe wenye Uadilifu waingie, wewe unakejeli na kuuita eti ni UPEPO tu! Kweli umewadharau Watanzania! Umeona pamoja na Udhaifu wako wote bado 2010 kuna waliokupigia kura, isikufanye ukawadharau uwezo wao wa kuelewa mambo. Angalia Ghadafi, hata yeye alijidanganya anapendwa lakini mwisho wake amekufa na vijiti. Sisemi kwamba haya ndiyo yatatokea na huku vilevile lakini hayatashangaza dunia kama yatatokea.
 
Kwani tulitegemea changes hata 1? ccm na kikwete simply can't change even to save their skins!

The reason is they're from reality.
 
Hii ni taarifa ya kupikwa from Tanzania Daima. Tuache kutumia hisia kutawala katika mambo mazito ya namna hii.The situation is too worse Rais hawezi kuwa mjinga kihivyo.Source ya information iliyotolewa hapa ni too ambitious to predict.Tusubiri Pinda jtatu hapo ndipo tutajadili na sio hizi habari za hisia.
 
Pepo ya mabwegeee!!!! Wachache wanaonja pepo wengi tupo Jehunum . Falsafa za mapinduzi ya Ufaransa zifanye kazi mapema. Nawakumbuka Jacobins movement, Rousseau, Blanc, Thiers, Robinpiers. Mashine ya kunyongea waovu itayarishwe. Sura ya Ufaransa karne ya 19 na 18 ndo iliyopo Tanzania saa hizi! Ahsanteni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom