Kikwete amteua Rajabu Hassan Gamalia kuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA




118px-COA_Tanganyika_1.jpg

Simu:255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz
Tovuti : www.foreign.go.tz
20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM,
Tanzania.
Nukushi: 255-22-2116600





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Balozi Rajabu Hassan Gamaha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi.

Balozi Gamaha anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Mwasi Nzagi ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.

Kabla ya uteuzi huo Balozi Gamaha alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Uteuzi huo unaanza mara moja.

-Mwisho-

Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
27 Aprili 2015






at 10:05 AM




 
Hongera Balozi Gahama. Jiandae kwa changamoto zilizoanza jana. Weka mikakati ya kusaidia kuepusha machafuko yatakayopelekea wakimbizi wengi kuja Tanzania. Kumbuka kuingia kwingi kwa silaha za kivita na ujambazi unaoendelea Tanzania kwa kiwango kikubwa umechangiwa na wingi wa silaha zilizoingizwa nchini na wakimbizi. Mshaurini huyo bw. mwenye uchu wa madaraka kuondoka nchini na kwenda kula alizovuna kwa amani.
 
Mabalozi huwa wanastaafu na umri gani, maana Abdulrahman Shimbo alistaafu jeshini akateuliwa kuwa balozi, Jack Zoka alistaafu TISS akateuliwa kuwa balozi.
 
Mabalozi huwa wanastaafu na umri gani, maana Abdulrahman Shimbo alistaafu jeshini akateuliwa kuwa balozi, Jack Zoka alistaafu TISS akateuliwa kuwa balozi.

Mkuu ubalozi ni zawadi Salva soon atapewa ubalozi halafu unategemea balozi zetu zile competitive zinabakiwa kuwa vituo vya kupokea wageni na kuratibu misafara ya viongozi
 
Tatizo ukiwa ubalozi njaa inakuwa kali zaidi maana unasubiri fungu toka wizarani (Nje na Fedha) wakikuzingua na kuchelewesha unakufa njaa...labda awamu hii watakuwa wanaenda na kazi ya JPM! Awamu iliyopita njaa ilikuwa kali zaidi!
 
Back
Top Bottom