Kikwete amteua Peter Noni Mkurugenzi mpya TIB!

mwana siasa

Senior Member
Aug 28, 2007
119
6
Jamani wana jamii wenzangu samahanini kwa kutokuwepo mtandaone kwa muda kidogo.

Hivi ina maana Muungwana haoni kelele zote hizi wanazopigiwa hawa mafisadi.Yule aliyekuwa mkurugenzi BOT na aliyefacilitate wizi pale BOT kapewa ulaji bada ya kuiba BOT .Soma chini -

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bw. Peter Efraim Mayunga Noni, kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) kuanzia tarehe 27 Mei, 2009.

2. Hadi uteuzi wake Bwana Noni alikuwa Mkurugenzi wa Mipango, Mikakati na Utendaji (Director of Strategic Planning and Performance Review) katika Benki Kuu ya Tanzania.

3. Uteuzi huu ni kufuatia Bw. William A. Mlaki aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji kustaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria.

TAARIFA HII IMETOLEWA NA MSEMAJI

Source website ya wizara ya fedha-

http://www.mof.go.tz/mofdocs/anouncement/UTEUZI TR.pdf
 
Last edited by a moderator:
Mnapompa mtu kula za kuwa raisi maanayake mmempa nguvu ya kuteua amtakaye. akitumia vibaya mnamsubiri kwenye kula tena au impechment! yote haya yapo ndani ya uwezo wetu
 
Vetting Tz hakuna! Raisi anaweza kuteua swahiba wake ktk cheo chochote! Hakuna wa kumuuliza!

Taabu pia Bunge la kufanya vetting ni la CCM- ila basi Bunge as Institution angalau hata upinzani basi watapiga kelele wakati wa vetting!

Hivi hoja ya vetting imefikia wapi??
 
Last edited:
this is when RA anawapeperushia "kidege" mbele ya nyuso zenu! Shahidi wa serikali ni lazima atunzwe bwana..!
 
Nakubaliana na MMK. Ni vitu vya RA -- the Kingmaker -- na JK inabidi akubali kwani si yuko mfukono mwake? Alimuagiza kumuajiri Salva huko Ikulu -- na akafata amri. bado tutaendelea kuona uchafu mwingi tu.
 
Kwani lile changa la macho tulilopigwa kuwa fedha zilizorudishwa za EPA zimewekwa TIB mlitegemea nini????? Ngoja muone miujiza sasa!!!!!
 
Yaani hii concept ya kupewa kazi kuwa kupewa "ulaji" imehalalishwa kabisa siku hizi au?
 
Nakubaliana na MMK. Ni vitu vya RA -- the Kingmaker -- na JK inabidi akubali kwani si yuko mfukono mwake? Alimuagiza kumuajiri Salva huko Ikulu -- na akafata amri. bado tutaendelea kuona uchafu mwingi tu.

jk kumpoint noni ni uchafu?acha kushikiwa akili...usifikiri hiyo ni nafasi ya kisiasa,noni ameenda shule,angalia record yake na nafasi alizoshika toka ameingia BOT
 
jk kumpoint noni ni uchafu?acha kushikiwa akili...usifikiri hiyo ni nafasi ya kisiasa,noni ameenda shule,angalia record yake na nafasi alizoshika toka ameingia BOT

kwelii kabisa.. ndiyo alikuwa anasimamia EPA na kwa elimu yake aliweza kuzuia wizi mkubwa kabisa uliowahi kutokea. Na atazuia upotevu wa fedha kuliko TIB
 
Masikini watanzania eti kuna wengine bado wanategemea kuvuna wakati nzige wametanda shambani wanakula wakilindwa 24/7. Thubutu ujaribu kuwapulizia DDT, utashukiwa kwa nguvu zote za dola.
 
kwani kuwa msimamizi ndio kukaa na kapu la fedha nyumbani?tumwombe MWENYEZI MUNGU atuletee malaika waje kutuongoza tz,maana mtu akiwa shahidi tayari naye keshakuwa mtuhumiwa/mwizi
 
kwani kuwa msimamizi ndio kukaa na kapu la fedha nyumbani?tumwombe MWENYEZI MUNGU atuletee malaika waje kutuongoza tz,maana mtu akiwa shahidi tayari naye keshakuwa mtuhumiwa/mwizi

Mtu anayeshuhudia wizi ukifanyika, na ana uwezo wa kuzuia wizi huo au kwa namna fulani ananufaika na wizi huo huyo ni sehemu ya wizi. Peter Noni ni mnufaika wa wizi wa EPA.. anatakiwa awe miongoni mwa wanaotiwa pingu lakini kwa vile ni amekuwa mbia wa mastermind wa EPA anachofanya ni kuzawadiwa.
 
Qualifications ni kitu gani??? Utakuta the most qualified ndo wezi wakubwa!

Record ndo muhimu: haswa uadilifu na usafi wa mtu!

Maana hata Balali nae alikuwa kichwa sana and he actually studied in one of best places!

Je Prof. Mahalu je hakuwa kichwa?
 
najua hujui wasifu wa NONI,mtafute mfanyakazi yeyote wa BOT akupe wasifu wa huyu jamaa ndio utajua jamaa yupo kwenye kundi gani,NONI hakuwa na uwezo wa kuzuia ule wizi,na kwa kushuhudia kwake ndio maana leo hii ni shahidi wa serikali na naweza kukwambia kuwa NONI si mnufaika wa EPA....
 
jamaa kwenye uadilifu na usafi hapo ndio nyumbani kwake
 
najua hujui wasifu wa NONI,mtafute mfanyakazi yeyote wa BOT akupe wasifu wa huyu jamaa ndio utajua jamaa yupo kwenye kundi gani,NONI hakuwa na uwezo wa kuzuia ule wizi,na kwa kushuhudia kwake ndio maana leo hii ni shahidi wa serikali na naweza kukwambia kuwa NONI si mnufaika wa EPA....

kiasi gani cha fedha aliwekeza kwenye kampuni ya Planetel na kule Vodacom?
 
Back
Top Bottom